Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Halafu anakuja kuwajua baada ya kuwateua? Au anawajua baada ya watu kuanza kuwachambua mitandaoni? Hapa pana tatizo. Tukumbuke Rais ni taasisi.
Rais ni Samia na siyo taasisi! Ingekuwa taasisi haya makosa yasingejirudia. Urais hauna ubia kwa hiyo lawama zote kwa Samia!
 
Halafu anakuja kuwajua baada ya kuwateua? Au anawajua baada ya watu kuanza kuwachambua mitandaoni? Hapa pana tatizo. Tukumbuke Rais ni taasisi.
Yaani hii pangua pangua sasa itaonekana haina malengo maalumu, ni bora tu kubadilisha. .. Viongozi wetu sijui wanakosa vision, ndio maana hawana hakika ni mtu gani anafaa kwenda kusaidia eneo gani. Huwezi kusema flani kawe kiongozi Simiyu bila kuchanganua potentials na challenges za hilo eneo, then unaangalia nani anafaa kwenda huko.
 
Hii inaweza kuwa one of the best comments in May 2021
Rais ni taasisi ndio..watu wanaomsaidia rais kutimiza majukumu yake..wanatakiwa wafanye kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa..wajue wakikosea wao anayeambiwa amekosea ni rais..tunaomba mlinde heshima ya rais wetu.. hongera rais kwa kurekebisha makosa kwa haraka..
 
yale yale ya zakia meghji... ya kuletewa file na kuambiwa usaini, bila kujua unasaini kitu gani
Kusaini nyaraka bila kuzisoma ni tabia ya watanzania wengi, sio wa serikalini tu. Mifano:
  1. ule wosia maarufu wa tajiri hayati Reginald Mengi, wale waliousaini kama mashahidi walikiri baadaye mahakamani kuwa hawakuwa wameusoma. Na ndio waliochangia kumwangusha Klynn wao kwenye kesi ya mirathi
  2. Uliza watu waliochukua mikopo benki kama huwa wanasoma chochote kwenye ile mikataba zaidi ya kiasi cha pesa wanayokopa. Baadaye madalali wakija kuuza nyumba zao ndio wanaanza kuzunguka kutafuta mawakili
  3. Wewe mwenyewe hizo Apps na mambo mengine unayojiunga ya mitandaoni, ni mara ngapi umesoma ile mikataba mirefu unayowekewa? Mara nyingi kama sio zote unatafuta tu kile kitufe cha ACCEPT unabofya maisha yanaendelea.
Ni desturi yetu watanzania. Labda tuanze leo kujirekebisha
 
yale yale ya zakia meghji... ya kuletewa file na kuambiwa usaini, bila kujua unasaini kitu gani
Kusaini nyaraka bila kuzisoma ni tabia ya watanzania wengi, sio wa serikalini tu. Mifano:
  1. ule wosia maarufu wa tajiri hayati Reginald Mengi, wale waliousaini kama mashahidi walikiri baadaye mahakamani kuwa hawakuwa wameusoma. Na ndio walio cnangia kumwangusha Klynn wao kwenye kesi ya mirathi
  2. Uliza watu waliochukua mikopo benki kama huwa wanasoma chochote kwenye ile mikataba zaidi ya kiasi cha pesa wanayokopa. Baadaye madalali wakija kuuza nyumba zao ndio wanaanza kuzunguka kutafuta mawakili
  3. Wewe mwenyewe hizo Apps na mambo mengine unayojiunga ya mitandaoni, ni mara ngapi umesoma ile mikataba mirefu unayowekewa? Mara nyingi kama sio zote unatafuta tu kile kitufe cha ACCEPT unabofya maisha yanaendelea.
Ni desturi yetu watanzania. Labda tuanze leo kujirekebisha
 
Hapa kulikuwa na tatizo kwa kuwa elimu ya huyu Azza ni ndogo na isingekuwa vyema kwenda kuwa katibu tawala. Katibu Tawala mkoa ndio mtendaji, anahitaji mwenye elimu ni Bora ingekuwa nafasi ya mkuu wa mkoa au wilaya maana hizo hazihitaji Sana wasomi.
Mkuu, mbona kuna wabunge ambao ni darasa la saba na bado wamo ndani ya mhimili huo wa kutunga sheria?
 
Angedili vikali mno na hao wanaompelekea majina yasiyokuwa na sifa. kuna haja ya kuwa mkali sometimes!
 
Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.

Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?

Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.

Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.

Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.

Mkuu kafulila ilikuweje si bado ni mkuu wa mkoa?
 
Hivi nafasi za makatibu tawala, ambao kimsingi ni watendaji waandamizi wa serikali, nazo zimeshakuwa ni post za kisiasa siku hizi? Hawa kimsingi ndio watendaji wakuu wa tawala za mikoa.
 
Hili tuu ambalo huchukua muda kufanya kabla yasie kuja kupata taarifa linakuwa hv na hii n Mara ya tatu kwa kumbukumbu zangu vp huko Kenya na uganda alipoenda bado zile za ugen wa ikulu na ma-briefcase hamna sehemu hajasain kimakosa kweli kwaniaba yetu watanzania?
 
Lakini kwa nini na yeye hakutumia mshahara wake kujisomesha walau online/distance learning diploma/degree. Dunia imebadilika sana - unaweza kusoma ukiwa popote na ukapata elimu unayotaka.

Kiongozi mzuri ni yule anayesahihisha kosa kuliko kuliacha liendelee. Hongera Mama kwa kusahihisha haraka. Hakuna hasiyekosea labda Mungu tu.
 
Uzi mzuri ila uandishi wako una walakini..unapotakiwa kuweka herufi kubwa unaweka ndogo na kwenye herufi ndogo unaweka kubwa. Uwe unahakiki unachokiandika kabla.
 
Bado yule RAS wa Iringa ni kilaza balaa. Anashirikiana na Kasesela kufukuza bajaji Iringa. Ukimuuliza anasema zimekuwa nyingi mno, zipo Bajaji 1600 ukimuuliza Iringa ina abiria wangapi hajui.
NCHI INAONGOZWA NA VILAZA SANA HII.
 
Hizi aibu za rejareja zinaepukika kabisa. Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa Rais (personally) na kwa Taasisi nzima
 
Back
Top Bottom