Rais Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye uteuzi wa Azza Hilal Hamad

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,223
Moja kwa moja nimpe mama Samia hongera kwa kurekebisha makosa yaliyofanyika kwenye teuzi za makatibu tawala na zile za wakurugenzi wa mashirika mfano ile teuzi ya DG wa TPDC.

Ni wazi Kuna majina mama anayopewa ya teuzi yakiwa na makosa. Ieleweke mama Samia hawezi kuwajua watu wote hivyo ni wazi lazima wengine awe hajui historia zao. Juzi aliteua makatibu tawala na kwa bahati mbaya kulikuwa na jina la Azza Hilal Hamad ambae aliteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa simiyu.

Hapa kulikuwa na tatizo kwa kuwa elimu ya huyu Azza ni ndogo na isingekuwa vyema kwenda kuwa katibu tawala. Katibu Tawala mkoa ndio mtendaji, anahitaji mwenye elimu ni Bora ingekuwa nafasi ya mkuu wa mkoa au wilaya maana hizo hazihitaji Sana wasomi.

Mama Samia pia angalia kwa jicho la pili aina ya majina unayoletewa maana hii ikiendelea utawapa nafasi wapinzani wako wapate upenyo wa kukutukana Sana.

Nakupongeza sana kwa kurekebisha haya makosa mapema sana, maana wengeenda huko kazini ingekuwa ni kituko. Pia Kama Kuna wengine uliletewa majina na hawapo vizuri watengue tu, ni Bora lawama kuliko fedheha.

20210531_123245.jpg
 
Hii ndo tabia ya kusaini mkataba kabla ya kuusoma na kuuelewa.

Rais hapaswi kukosea kirejareja namna hiyo. Ni vyema kukaa chini na kujiridhisha juu ya hizo vetting maana wengine ndo hupata mwanya wa kupitishia michepuko na ndugu zao.
 
Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.

Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?

Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.

Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.

Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.
 
Umeandika kombora kubwa mkuu, nadhani akiiona hii komenti yako, hatakosea tena
 
Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.
Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?
Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.
Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.
Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.

Wanarudia makosa yale yale kila wakati. Hao nao ni jipu (in mwendazake tone)
 
Kukosea ni jambo la kibinadamu hasa suala la kuongoza binadamu ambalo ni kazi ngumu sana, Mungu amsaidie awaongoze watu kwa haki na mafanikio
 
Kuna kila dalili Mama anahujumiwa kwa kiasi kikubwa. Na wahujumu wake ni wale walio karibu zaidi na yeye.
Hii pattern ya kuteua na kutengua itakuja kumgharimu mama mbeleni. Hasa kipindi cha uchaguzi. Hili swala pamoja na mengi yanayotokea kwa sasa ikiwemo wizi vitatumiwa kuhoji uwezo hasa wa mama wa kuweza kumudi nafasi yake.

Mama anapaswa kuangalia waliomzuka kwa jicho la karibu sana la sivyo ataondoka akiacha historia kuwa raisi wa ovyo kuliko wote waliopita. Maana zaidi ya kumtoa nje ya reli wana dhamira kubwa ya kumfanya Mwendazake aonekane alikuwa irreplaceable, yeye na wale aliowaweka karibu kipindi cha uhai wake.

Bado nina matumaini na mama, akizungukwa na watu sahihi nia yake njema itamfanya atende miujiza mikubwa. Tofauti na hapo tutaishia kuteua na kutengua mpaka awamu iishe.
 
Hao wanao mshauri rais wameonyesha udhaifu mkubwa na kumufanya rais aonekane siyo makini.

Hivyi si kuna sifa zimeanishwa kwa kila nafasi inayo tangazwa? Kama ni hivyo ni nani anamletea hao watu wasio na sifa?.Huyo anza naye.
Kabla ya uteuzi si wateule wote hufanyiwa vetting ya kutosha? Au wanaokwotwa tu?

Inasikitisha sana kosa lilianziwa kwa yule wa TPDC, akaja Kafulila, imekuja tena hili la katibu tawala.

Tumeona mpaka waraka toka Ikulu unatolewa umekosewa tarehe.

Watu wa Ikulu na wengine mnao husika msimvunjie heshima rais wetu.
Bora Mama akiona au kupata taarifa ya mapungufu anasahihisha. Mwendazake hata kama ametambua kuna mapungufu na watu wanaanza
kupiga kelele alikuwa habadili. Alikuwa na kamsemo kake kuwa eti yeye hapangiwi. Bora Mama aayesahihisha kuliko Mwendazake aliyekuwa anakaa na uozo.
 
Back
Top Bottom