Rais Samia, hili la wamachinga litawapa umaarufu wanasiasa waliopoteza mvuto. Watasema "umepiga mchache"

Ndugu zangu wanaJF!

Rais wangu SSH ninaona ugumu huko mbeleni kisiasa.Kumbuka kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka 2015 wana-CCM tulikuwa hatuwezi kukatiza mitaa ya majiji makubwa tukiwa na sare au fulana kwani tulizomewa na baadhi waliambulia vipigo.Siasa za manispaa na majiji makubwa zilitekwa na wanasiasa walioahidi neema kwa wamachinga.

Sasa naona takribani mwaka mmoja baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kabla hata ya kuandaa sehemu sahihi za kufanyia biashara wamachinga wanaondolewa mijini kwa ukatili mkubwa.Yaani KPI mpya ya Ma-RC na Ma-DC ni kudhibiti wamachinga wasitafute riziki bila ya kutoa suluhisho mbadala.

Nimalize tu kwa kusema Rais Samia kwenye hili la wamachinga tutapata tabu mbeleni kwani sasa "Serikali imeupiga mdogo" ,hatujachelewa tujisahihishe.
Kwani nyiemnafanyaga uchaguzi, ninavyojua upo uchafuzi na zaidi zaidi policccm , wanatosha kuwashindisha akiongezeka neck , karani wa vyama plus wakuruginzi biashara imekwisha. Sasa mmeanza kutishana nyau wenyewe Kwa wenyewe, vipi Tena Wakudadavua , unatuangusha kijani wenzio🤸.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom