#COVID19 Rais Samia hili la Covid-19 bado unatuchanganya kidogo, au ungeachana nalo tu?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Rais Samia kwanza kabisa Mimi sipo upande wa CCM na naichukia sana CCM, lakini kutokana na kusema tukukosoe kwa heshima basi nitafanya hivyo kwako.

Naomba nikukosoe kwa heshima kuhusu ili suala la corona. Mara nyingi umekuwa ukituoumbusha na kutuasa kuwa corona iliingia nchini mwetu na ipo na inaua.

Na ulitumabia kuwa tuchukue tahadhari zote kujilinda na ugonjwa huu hatari na ndio maana hata serikali ikaamua kuleta chanjo ili kuponya watu wake.

Ikiwa kila siku unatukumbusha kuhusu hatari ya corona na kufuata namna ya kujikinga, alafu hapohapo na wewe mama yetu unavunja hayo masharti ya kujikinga na corona basi unatuchanganya sana.

Ziara yako ya Jana kutoka Moro kwenda Dom, huko njiani ulikuwa ukisimama kuongea na wananchi ambao walikuwa wamejikusanya bila tahadhari yoyote. Na hapo hapo Kuna magari ya serikali yalikuwa yakipita kuwaambia watu wakusanyike njiani kukusubiri uongee nao.

Mnatuchanganya sana Mh.Raisi mnatukusanya alafu mnatuambia tuepuke mikusanyiko. Kwa maneno yako kuhusu corona na kwa hali ilivyo wala hakukuwa na ulazima wewe kusimama huko njiani au kama vipi uachane nalo hili maana unachozungumza na kinachofanyika ni tofauti.

Juzijuzi ulikuwa uwanja wa taifa kwenye mechi ya Simba va yanga, watu walikuwa maelfu bila tahadhari yoyote, tofauti kabisa na ulivyosema na unavyosema kuhusu corona.

Ushauri: hili suala ninakuomba mh.Raisi uachane nalo.

#katiba mpya kwanza#
#R.I.P Charles Mbowe# pole mwenyekiti wangu#

Screenshot_20210709-092510_1.jpg
20210709_090502.jpg
Screenshot_20210709-001940_1.jpg
 
Corona ipo kama mwanza ndo imekita kwa kiwango kikubwa kwa sasa

Madaktari wawili Bugando washakufa

Mashine za Oxygen zimeongezwa kutoka Muhimbili
 
Corona inaua wa Tz kimya kimya lakini kwasababu wanasiasa wetu wanatafuta political capital en fame wameshindwa kua wawazi, hapa muhimbili vitanda vyote vya ICU vimeja na bado watu wanaletwa, na mitugi ya oxygen haipo, ila nchi yetu buana Mungu atusaidie tu wasomi wetu wamejikausha tu.
 
Corona muziki mzito. Bora mkubali kuishi nayo tu kuliko kusubiria maagizo yasiyotekelezeka.
 
Saa100 suluhu kama mtangulizi hayuko serious na kupambana na Corona, yaa third wave ina fyeka waTz yeye analeta masihara na mizaa mizaa.
 
Angalia charts za madakitari bugando watu wanakufa kimyakimya serilikali iko mute.

IMG-20210627-WA0057.jpg
 
Acha mama ajifamye anapambana na corona katika media ili ukitokea mgao wa wimbi la tatu la corona na sisi tupate sio kila siku wapate Kenya tu.

Kwa upande wa pili corona kwetu sio ishu na kama kweli ikija hatuna uwezo wa kuizuia kitakachotokea ni kama ule utabari wa mke wa billget aliyesema corona ikingia Africa maiti zitazagaa mitaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kumshinikiza Head of State Mh SHS achukue hatua kali dhidi ya wananchi wake. Yeye HOS anajua. Anaenenda kwa sayansi halisi.
Tujiulize hao wanaokufa kwa korona je, chanzo ni korona tu au ni mengineyo yamechangia. Kumbuka wanaopona ni 97. 70% ya wanaougua.

Unataka achukue hatua kali zaidi , hao wafanyakazi wakiwemo mapolisi na wanajeshi mishahara mutawalipa nyie au watu wasipolima mtawalisha waTanzania. Mijini uhalifu ukiongezeka kwa ukosefu wa mizunguko wa fedha nitarudi humu kulalamikia serikali. Mambo ya Korona yanahitaji busara sana kuyaendea kama kiongozi.
 
Vitabu vya dini vinatuasa tusijihusishe kwenye vitendo vya kuzini kabla ya ndoa wakati huo huo tunawekewa viuongo vya ndoa kabla...so hapa nashauri akili za kuambiwa uchanganye na za kwako.
 
Acheni kumshinikiza Head of State Mh SHS achukue hatua kali dhidi ya wananchi wake. Yeye HOS anajua. Anaenenda kwa sayansi halisi.
Tujiulize hao wanaokufa kwa korona je, chanzo ni korona tu au ni mengineyo yamechangia. Kumbuka wanaopona ni 97. 70% ya wanaougua.

Unataka achukue hatua kali zaidi , hao wafanyakazi wakiwemo mapolisi na wanajeshi mishahara mutawalipa nyie au watu wasipolima mtawalisha waTanzania. Mijini uhalifu ukiongezeka kwa ukosefu wa mizunguko wa fedha nitarudi humu kulalamikia serikali. Mambo ya Korona yanahitaji busara sana kuyaendea kama kiongozi.
Umeongea bila pengine kusoma nilichoandika, yeye ndio anayesema corona ipo na inaua na akasema tuchukue tahadhari ikiwepo kuepuka mikusanyiko. Hoja yangu ni kuwa kwa nini anaendelea na mikusanyiko ikiwa kila Mara anasema tuiepuke?
 
Nimesoma sana. Wewe ni kati ya Watanzania ambao aidha hufuatilii mambo yanavyokwenda ulimwenguni kuhusu korona au unameza kila taarifa kuhusu korona au huwajali wananchi wenzio ambao kula yao mpaka watoke.

Mwache Mh SHS she knows better.
 
Bado wale wanausalama waliojichanganya katikati ya huo umati ambao nao ni part ya msafara...
 
Back
Top Bottom