Rais Samia afanya Ufunguzi wa Barabara ya Nyahua – Chanya Mkoani Tabora

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,744
11,864
Rais Samia Suluhu Hassan yupo Mkoani Tabora kwa ajili ya kushiriki Ufunguzi wa Barabara ya Nyahua – Chany, leo Mei 17, 2022.

Ikulu.jpg

Rais Samia ameanza kuongea

=====

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Lengo la Serikali ninayoiendesha inalenga kujenga miundombinu ya barabara na madaraja ili kuiunganisha mikoa na wilaya zote.

Kwa kufanya hivyo, tutachochea zaidi shughuli za uzalishaji na biashara ili kuboresha maisha ya wananchi wetu

- Utunzaji wa Miundombinu
Hata hivyo, naomba mjue ujenzi wa miundombinu hii unagharimu fedha nyingi. Na mmetajiwa hapa mabilioni yaliyotumika kujenga barabara hii. Hivyo ni rai yangu kwenu nyote kuhakikisha mnaitunza.

Nasisitiza hivi kwasababu katika maeneo mengi kumekuwa na vitendo vinavyohatarisha usalama wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Vitendo hivi ni pamoja na uchimbaji mchanga kiholela pamoja na utupaji wa taka hovyo. Zaidi yah apo wananchi wanadiriki hata kuiba alama za barabarani – hii ni hatari. Huo ni uhujumu wa uchumi wetu. Barabara lazima ziwe na alama.

Alama zinazowekwa zina maana kwa madereva.

- Usimamizi wa Viwango na Ubora
Aidha niwasisitize Wizara ya Uchukuzi kupitia TANROADS waendelee kusimamia viwango vya ubora na kasi ya utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia masharti ya mikataba

- Utekelezaji wa Ombi la Margaret Sitta
Ndugu zangu mimi nakumbuka vema, nadhani ilikuwa mwaka 2014 nikiwa Bungeni, nakumbuka tulikuwa kwenye kipindi cha kupitisha bajeti ya Serikali. Dada yangu Mama Sitta alisimama kwa huzuni kubwa kuwa “Tabora tumechangia sana kuleta Uhuru katika nchi hii lakini mpaka nasimama hapa Tabora hatuna hata kilomita moja ya lami”

Alisema kwa masikitiko makubwa, Serikali ilisikia na sasa Tabora imeunganishwa na lami kila upande.

- Changamoto za Uyui
Naomba nizizungumzie changamoto za Uyui ambazo pia kwa sehemu kubwa zinayahusu maeneo mbalimbali ya Tabora.

Kwanza, kuna tatizo la ajira za walimu. Lakini pia, natambua kuna upungufu wa walimu katika shule za msingi ambapo mahitaji ya sasa ni walimu 3384 na waliopo ni 1343, hivyo kuna upingu wa walimu kama 2041 sawa na asilimia kama 60 hivi.

Halikadhalika, natambua uhitaji wa walimu 939 wa masomo ya sayansi kwa shule za sekondari pamoja na nyumba za walimu.

Vilevile nafahamu katika wilaya hii kuna upungufu wa miundombinu katika shule za sekondari, ambapo kwa sasa kuna uhaba wa matundu ya vyoo 332, meza 707, viti 707, maabara 59 na nyumba za walimu 295. Serikali inafahamu hayo.

- Halmashauri zijikongoje
Na sitaki kusema serikali itabeba mzigo wote. Nataka kusema Serikali tutafanya na Halmashauri za wilaya hii na zenyewe zijikongoje. Zijikongoje kuonesha kweli kuna mahitaji. Kwenye ajira, serikali tutafanya.

- Ajira 32,000+ Mwaka Ujao wa Fedha
Kwa mwaka ujao wa fedha, uchumi wetu umeturuhusu kuwa na ajira 32 elfu na mia kidogo. Kiwango kikubwa cha ajira hizi kitakwenda kwenye Sekta ya Elimu na Sekta ya Afya. Kwahiyo, kwa jinsi tutakavyoajiri ndivyo tutakavyoleta na huku Tabora.

- Fedha za UVIKO
Lakini mahitaji haya ya matundu ya vyoo naomba Halmashauri zianze nasi tutakuja kuweka nguvu. Nafahamu pia Wilaya ya Uyui ilinufaika na fedha za UVIKO ambapo ilipokea jumla ya bilioni 3.7 na fedha kubwa ilielekezwa kwenye elimu. Jumla ya vYumba vya madarasa 123 vilijengwa katika shule za sekondari 27; na vyumba 57 katika shule shikizi 23.

Nimefurahi sana kwa shule shikizi kupata madarasa. Mara ya mwisho nimetembelea Uyui nilisikitishwa na aina ya shule shikizi nilizoziona.

Wakati ule DC alikuwa Gift Msuya. Alikwenda kunionesha shule shikizi ambayo ilinisikitisha sana. Nimefurahi kwamba wajukuu zangu wale sasa wamepata madarasa ya kisasa na wanaendelea kusoma vizuri.

- Mgao wa Ajira za Walimu 69 Uyui
Kwa Mwaka wa Fedha unaoendelea Uyui ilipata mgao wa ajira za walimu 69 ambapo 30 ni shule za msingi na 39 ni shule za sekondari. Tutaendelea kuajiri kwa kadiri bajeti itakavyoturuhusu na kwa kuzingatia mahitaji ya kila mkoa na kila wilaya Tanzania nzima.

- Maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za umeme Uyui
Sambamba na hilo, natambua kuwa katika Wilaya ya Uyui kuna maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za umeme kama alivyosema Mbunge hapa, ikiwemo kata za Kizengi, Iyenze, Igulungu na Shitagi. Natambua hawana umeme lakini kama mnavyoona mkandarasi yupo site kazi inaendelea.

- Uhitaji Vituo vya Afya Kata ya Kizengi
Natambua pia uhitaji wa vituo vya afya katika Kata za Kizengi na Ibelamilundi. Kazi inaendelea.

Kero nyingine kubwa ni kwa barabara kushindwa kupitika wakati wa masika. Tumeongeza fedha nyingi kwa TARURA ili waifanye kazi hii.

- Miradi yote ya Awamu ya Tano itaendelezwa
Wanaposema Serikali ya awamu ya sita imeacha kutekeleza miradi iliyoanzwa nyuma hapa tunawasuta, wanachosema ni uongo, miradi yote tuliyoianza awamu ya tano, mimi nilikuwa Makamu wa Rais tunaendelea nayo na faraja yangu ni kwamba miradi kadhaa imekamilika

Ametaja baadhi ya miradi ambayo inaendelezwa ni barabara na madaraja yaliyopo Dodoma, Tanga, Pwani, Njomb, Dar es Salaam, Lindi Mwanza na Kigoma.
 
Mama huwa ni Mzee wa short and clear hakuna haja ya blaa blaa na tantalila nyingi zisizo na maana .

Safi Sana kwake
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom