Rais Samia hawa watu usipowateua watageuka kuwa maadui zako

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Hadi sasa nimeona watu wa aina tatu wakitafuta namna yoyote ili wawe sehemu ya Serikali yako, wanatumia kila mbinu.
  • Kuna wale wabunge ambao 2020 walikatwa, wakiwemo wa viti maalum. Hawa wana Imani kubwa na wewe wakiamini kabisa utawakumbuka kwenye serikali yako.
  • Kuna wale hawamiaji, majuzi Kuna mmoja alinipigia debe mbele yako kuwa ana uzoefu wa uongozi ana yupo tayari kufanya kazi.
  • Siku ile ya Scout, nao walikuomba uwakumbuke kwenye teuzi na ukasema utawakumbuka.
Yote haya wewe umeyalea, muda utapofika na wasipate walichotarajia watageuka kuwa maadui wakubwa wa serikali.

Ulikuwa na nafasi ya kukataa haya, Ila ulikubaliana nayo. Kumbuka hawafanyi wanayoyafanya Sasa kwa bahati mbaya.

Sasa kazi kwako.
 
Sasa hao si ndio wanawaambia vijana wetu wakimaliza vyuo waende wakajiajiri? Sasa na wao wawe mfano kwa vijana wetu kwa kujiajiri badala ya kujipendekeza kungojea kuteuliwa. Mama Samia usikubali hawa jamaa wakublackmail, usiwateue tuone watakachofanya.

Mama Samia usitishike na hawa aina ya wakina Polepole wanaolalama kwa vile walivyozoea hawavipati sasa; fanya uteuzi wako kufuatana na weledi wa wahusika, usiangalie jinsia wala dini bali weledi wa wahusika. Hapo ndio utafanikisha malengo ya Serikali yako.
 
Vijana wa CCM wamezoeshwa kupewa kila kitu ndiyo maana kazi yao ni majungu.
 
Kwani ukiwa adui wa Samia sisi inatuhusu nini au unampunguzia nini Samia. Yaani lumumba mna tabu lol!!!
 
Kwani wewe upo kundi gani haswaa?
Mimi nipo kundi ambalo halipo pamoja na CCM yoyote

Mimi ni mmoja ya watu ambao naamini kabisa mbowe hajawahi na hatawahi kuwa gaidi

Mimi ni mtu ambae Nina amini magaidi wapo CCM, ndio maana Kuna akina sabaya na bashite
 
Mimi nipo kundi ambalo halipo pamoja na CCM yoyote

Mimi ni mmoja ya watu ambao naamini kabisa mbowe hajawahi na hatawahi kuwa gaidi

Mimi ni mtu ambae Nina amini magaidi wapo CCM, ndio maana Kuna akina sabaya na bashite
Shukrani kwa kujieleza kwa makini bila mihemuko
 
Ndani ya CCM bila kujikomba na kuji-promo aisee teuzi utazisikia kwa makada wenzako tu.
 
Ujinga mtupu Acha kutishatisha watu

Kazi ziko nyingi,nendeni mkalime pia

Ova
 
Kiongozi shupavu ni yule ambae haangalii makunyanzi, anafanya kazi kulingana na maono yake.(visionary leader)
 
Back
Top Bottom