Hatuna Kiongozi ... Nawaambia kama hamjafahamu mpaka sasa. Hamna kitu pale. Ni picha tu.... Ni Tumepata Salma Mtembezi. Hakuna anachoelewa. Si wa kupambania wananchi.

Tulisema anaupiga mwingi.. sasa anaendelea kuupiga mwingi usio na faida sababu ni nje ya uwanja. Haina maana kabisa.
Anaupiga mwingi sana .... muacheni apige kazi
 
Kwa hiyo ulitaka wale wa vijijini ndio wawe na barabara mbovu? Lipa tozo kijana.

Sie watumishi tumeshajenga SGR na Stiegler Gorge kwa maumivu ya kutopandishwa mishahara,kutolipwa posho,kutopandishwa madaraja,kutumbuliwa,kuongezwa majukumu nk.

Mkaponda Sana...
Matajiri wakifanywa kitu chochote, kwakweli tulipumua! Time to payback
 
... nendeni kwenye mikutano ya kisiasa/kampeni mkasikilize na kuchuja sera na ilani - hatuna nafasi sisi!
... someni sera za vyama na ilani zao mpate mwanga wa jinsi zitakavyosaidia au kuumiza maisha yenu watanzania - hayatuhusu sisi!..
Asante ndugu kwa hili andiko wengi husema siasa haiwahusu, leo ndio wajifunze kuwa ' Ushikwapo, shikamana' ndio maana yake hii. Siasa ndio inayoamua maisha yetu ya kila siku na hivyo yatupasa kuifuatilia kwa ukaribu.
 
Nadhani unasema huna imani na huyu rais na unashindwa kujieleza kwa kuogopa midnight knock at the door. Kwa sababu sielewi hata kitu kimoja ulichoandika.
Rais huyu siyo creative,siyo mbunifu. Hakuna feeling kwamba nchi Ina rais.
Lakini ukibishana naye utaambiwa unachukia wanawake.
 
Zipo kila dalili kuwa hali ya uchumi kwenye utawala huu wa Rais Samia unaenda kuwa fyongo! Hali hii itaenda kuyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu sana.

Nimeangalia kwa mfano viwango vipya vya tozo za miamala ya kutuma fedha na kutoa fedha kupitia mitandao ya simu, Gharama zake zimeongezeka sana wakati mwingine kuwa hata mara mbili ya ilivyokuwa hapo awali.

Athari ya hii kitu, ni kuua microeconomy ambayo ilikuwa imejiintegrate na huu mfumo mitandao ya Mpesa, TiGo pesa na mingineyo, kuua mafanikio ambayo kama Taifa tulishayafikia, maana hii mitandao ilikuwa kama "Miundo mbinu" ya kurahisha biashara kuliko kuwa chanzo kikuu cha mapato ya serikali(Japo hili liligeuka kila kukicha baada ya kuona mafanikio yake).

Sasa hivi wananchi watakuwa wazito kutuma pesa, watakuwa wanatuma tu kama hawana jinsi, lakini wengi watakuwa wanajifikiria mara mbilimbili, kwa hiyo hii itaathiri biashara zilizokuwa zinategemea hii mitandao!. Maana tulishafikia hatua, unanua kitu let say ktk duka fulani liko mbali na wewe kwa kulipia kupitia Mpesa, Tigo pesa halafu unaletewa na mzigo na bodaboda wa kampuni. Sasa hivi ule urahisi na wepesi wa kufanya hivyo hautakuwepo kwa hiyo Mteja hatosumbuka kuagiza mzigo wa mbali na kulipa kupitia hiyo mitandao maana ni ghali sana.

Pia kutuma pesa kusaidia ndugu na jamaa naamini volume ya kutuma itapungua. Maana kila ukituma pesa fulani unajikuta makato ni mengi, kwa hiyo hata ule ubinaadamu wa kusaidia ndugu huko vijijini nao utapungua kidogo. Mtu utakuwa unatuma pale inapobidi sana lakini si kwa frequency kubwa.

Wakati tunaongea hayo, kuna ongezeko la kodi katika mafuta, hii imeanza kuathiri bei za vitu. Tumeona kwa mfano Mamlaka za Usafiri nchini LATRA imetoa bei mpya ya nauli za mabasi mikoani. Gharama nazo zimeongezeka, hii maana yake wafanyabiashara wanaosafiri kufuata mzigo itabidi waongeze gharama za usafiri kwenye bei ya bidhaa watakazouza, matokeo yake bei za vitu zitakuwa juu sana na maisha yatakuwa magumu zaidi.

Wakati huo Samia anaonekana anaenjoy kuendelea kukopa mihela kedekede kutoka nje, Mwezi uliopita au miwili iliyopita alipata mkopo wa Matrilion ya fedha kutoka taasisi za nje, Na sasa hivi anataka mkopo kwa ajili ya masuala ya Korona. Sasa hakuna free lunch duniani, hii mikopo ndiyo inakwenda kutunyonga sisi wananchi, maana ili ilipwe lazima afikirie kutukamua kodi.

Mishahara hujaongeza, gharama za maisha zinazidi kupanda halafu bado unafikiri kutuongezea kodi, hizo pesa tuzipate wapi sisi ewe Samia rais wetu?

Kibaya zaidi, hakuna political reform yoyote inayoendana na uelekeo huu wa maisha magumu ya wananchi. Hii itapelekea Nchi kuvimba, na Samia asipohakikisha anatoa opportunity ya nchi kupumua kiuchumi na kisiasa, atajikuta katika wakati mgumu sana kutawala nchi hii! Nimpongeze alishtukia mtego wa kuwafukuza wamachinga akaukataa, ule ungemsumbua sana, maana mwenye njaa hana cha kupoteza!

Huu ni muda muafaka Samia atafute wachumi waliobobea wamshauri namna ya kuendesha huu uchumi. Lazima awe mbunifu wa vyanzo vipya vya mapato.

Hii nchi ina ardhi kubwa, ina bahari, ina mito, ina maziwa, ina kila kitu, huo ubunifu wa kupata hela nyingi kupitia vyanzo hivyo uko wapi?. Mnawaza kuwapiga kodi wananchi doubledouble, yaani nitume pesa nitozwe kodi, nitoe pesa nitozwe kodi tena, yaani kipesa hichohicho mnanyakuanyakua mara mbilimbili cone on!

Wakati hayo yanafanyika kuna watu nchi hii mishahara yao haikatwi kodi, Rais hakatwi kodi, Wabunge hawakatwi kodi, Majaji wa mahakama zetu mishahara yao haikatwi kodi. Hii inakuwaje?, Huu ni unyonyaji!., Tunataka hawa nao waanze kukatwa kodi kwenye mishahara yao kama watu wengine.

Lakini ukiacha hilo, Juzi Jaji warioba alizungumza kuhusu serikali. kubana matumizi.

Sasa sisi tunaona rais Samia muda mwingi yuko kwenye ndege anaenda Dodoma, anaridi Dar, anaenda Dodoma anarudi Dar. Hizo gharama za kupeleka hilo li airbus anazibeba nani?

Hao wakuu wanaompokea Dar airport akija, na hao wanaomsindikiza na kumpokea tena na kumsindikiza tena watafanya kazi zao ofisini saa ngapi, ina maana watafanya kazi ya kumsindikiza na kumpokea Samia tu?

Lakini wakati hayo yakifanyika eti wanawaza kumjengea Magufuli sanamu. Mambo ya ajabu kweli yanafanyika katika nchi hii. Hizo milioni 420 wanazotaka kutumia kujenga sanamu zingetolewa kama mikopo ya ujasirimali. kwa vijana zingesaidia vijana wangapi kutoka katika limbwi la umasikini?

Hapana aisee, Samia angalia Washauri wako wa uchumi na siasa, something is wrong!
Ndogo zako zimefikia wapi mkuu? Karibia ujikojolee 😬😬
 
Magufuli aliifirisi hii Nchi, acha Samia arekebishe uchumi wa Nchi
Kweli aachwe arekebishe inchi,,
-ukienda mloganzila hospital kumwona doctor sh 20000 .
-bima ya NHIF kwa watoto ilikuwa sh 50400 kwa mwaka wakati wa Magufuli ila kwa sasa ni 340,000/

Kweli aachwe arekebishe inchi..
Inchi inaelekea pazuri
 
Back
Top Bottom