beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ifikapo 2025, Serikali inalenga Sekta ya Madini iweze kuchangia 10% ya Pato la Taifa. Ameeleza hayo katika Hafla ya Utiaji Saini Mikataba baina ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini.
Amesema, "Tunasikia Madini yamepenya huku na huku, jitihada zinafanyika kuzuia hali hiyo. Waliotumwa kusimamia utoroshwaji madini badala ya wao kuwa chanzo, warudi walinde Rasilimali yetu"
Ameongeza, "Hali ya utoroshwaji haikubaliki na hatutaruhusu Uhujumu huu kuendelea. Zifanyike doria za mara kwa mara ili wahusika wajulikane"