Rais Samia hatuhitaji tena ziara zako za barabarani, hazina msaada wowote kwetu

Watu mnamaneno.
Ushauri msimseme sana Rais,njia pekee msiejitokeze barabarani kwani Hamna uvumilivu kama ambavyo Magu hakuwa mvumilivu.
Mfano Shaka alimtumbua.
RC Makala vivyo hivyo.
Leo viongozi tena.Mama mvumilivu anafuta taratibu.

Hoja ya kusikiliza watu barabarani kwa mda mfupi nimeona hakumfai,siyo karama yake ya papo kwa papo.
 
Hiyo ni kwa sababu Mama ni muongeaji kuliko vitendo, akiongea unapata matumaini unaona sasa tunaelekea pazuri ila anafeli kwenye utekelezaji.
Kwahiyo hata mimi sijaona sababu kwa yeye kusikiliza hizo kero za watu maana zinahitaji utekelezaji na kuishia kusikiliza tu na hapo ndio penye udhaifu wake.

Zama za unanijua mimi ni nani zimerudi.
 
Ujinga gani? Jamni kwanini huwa hatuwezi kuvumiliana? Mtu anatoa maoni yake wewe unamtusi kweli hii ni sawa?

Anyway, ni kweli kwamba tunapaswa kuheshimu mamlaka ikiwa na pamoja na majukumu yake lakini ukweli ni kwamba kuna uonevu mkubwa mno wananchi maskini wanakumbana nao, kesi nyingi tu za kubambikizwa na viongozi wasaidizi wanakura rushwa, wengi sana wameteseka kesi zao hazitatuliwi ni kupigwa chenga tu je mnataka wananchi wafanye nini?

Mwananchi anapoenda kwa Rais ujue ameteseka sana na hakuna msaada wowote, kwa nature ya viongozi wetu hawa usishangae huyo mama hatapewa msaada wowote kumbuka mama alikataa mabango na shida za barabarani inamaana kusimama kwake ni sawa na kuwachoma wale viongozi then kesi imerudishwa kwa subordinate nini kitatukia?

Ukweli utabaki pale pale, kero za wananchi ni nyingi mno na hazitatuliwi!
Asipo kuelewa hapa,basi hawezi tena kukuelewa hadi na yeye limkute la kupiga kwata kwenye office za Umma hadi soli ya kiatu inaisha lakini bado bila bila!!
 
Kwanza kabisa napenda kukupa pole na majukumu ya kitaifa.

Vile vile tunakuombea wewe na Serikali yetu katika utekelezaji mwema wa majukumu ya nchi ili kuinua uchumi.

Mweshmiwa Rais katika muda mchache huu umeonuesha matumaini ya watanzania kupata maisha bora, Ajira na uchumi kuinuka tena hongera sana na Mungu akubariki kwa hilo.

Niende kwenye lengo husika, katika siku za hivi karibuni umekuwa ukifanya ziara na kusimama barabarani kuongea na wananchi, lakini wananchi wanapopewa maiki kusema kero zao hakuna solution yoyote zaidi ya kusema unawaachia maofisa wako.

Mbaya zaidi kuna watu wanashida za muda mrefu mfano yule mama mjane juzi anakueleza shida yake, wewe kama Rais ilibidi uitatue pale pale kwa kuwahita wahusika wajibu, matokeo yake unamwambia awaone sijui wakuu wa mkoa sijui nani, kwani unafikiri ye alikuaga hawaoni?

Hii nchi ina watu wenye viburi kesi zinafichwa hata na ma OCD lakini mtu anapokuona wewe Rais anaona kama amepata mkombozi utatue swala lake.

Kama umeamua kuendeleza style ya mtangulizi wako ya kuongea na wananchi njiani basi endeleza na kutatua kero, JPM alikua kama imetokea kero anawaita wahusika kiwahoji pale pale na anatoa maamuzi pale pale.

Sasa Rais wangu wewe hufanyi hvyo, sisi wananchi tunakutegemea ww huku Uraiani kuna uonevu mwingi sana.

Mimi nafikiri kama utaendelea na style yako hii basi ziara za barabarani achana nazo hazina tija kwetu.
Wengine tunazihitaji Sana
 
Uko sahihi 100%
Acha ujinga. Rais anapaswa kujibu hoja za kitaifa zaidi, ambazo haziwezi kutatuliwa na wasaidizi wake walioko chini huko.
Vinginevyo mtampelekea hata kesi zenu za ndoa!

Pia huwezi toa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu!
 
Matatizo ya watu milioni 60 hayawezi kutatuliwa na mtu. Hao wanaoonewa na kunyimwa haki zao wana mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kata, diwani, mbunge, mkuu wa wilaya, DED, DAS, RAS, mkuu wa mkoa, Makatibu wakuu, Mawaziri, Mahakama.
Kama huko kote hakuweza kupata haki yake au shida yake kutatuliwa basi amelaaniwa ateseke tu au mfumo ni wa hovyo sana na unapaswa ufumuliwe.
Ujinga gani? Jamni kwanini huwa hatuwezi kuvumiliana? Mtu anatoa maoni yake wewe unamtusi kweli hii ni sawa?

Anyway, ni kweli kwamba tunapaswa kuheshimu mamlaka ikiwa na pamoja na majukumu yake lakini ukweli ni kwamba kuna uonevu mkubwa mno wananchi maskini wanakumbana nao, kesi nyingi tu za kubambikizwa na viongozi wasaidizi wanakura rushwa, wengi sana wameteseka kesi zao hazitatuliwi ni kupigwa chenga tu je mnataka wananchi wafanye nini?

Mwananchi anapoenda kwa Rais ujue ameteseka sana na hakuna msaada wowote, kwa nature ya viongozi wetu hawa usishangae huyo mama hatapewa msaada wowote kumbuka mama alikataa mabango na shida za barabarani inamaana kusimama kwake ni sawa na kuwachoma wale viongozi then kesi imerudishwa kwa subordinate nini kitatukia?

Ukweli utabaki pale pale, kero za wananchi ni nyingi mno na hazitatuliwi!
 
Ni vyema huu utaratibu ukaendelezwa kwani unampa Rais nafasi ya kusikia matatizo ya wananchi moja Kwa moja.
 
Hivi Logically tu inakuingia Akilini kwa Mtu ambaye Kiserikali ni Commander In Chief na pia ndani ya Chama ndiyo Mwenyekiti Taifa halafu akatokea Mpumbavu wa Kumtisha na Kumshurutisha?

Acheni Kudanganyana huko Vijiweni Kwenu mnakoshinda na jifunzeni kuwa na Fikra pana zaidi.
Na hapo ndipo tatizo hasa linapoanza kwa watanzania. Kuamini sana habari za vijiweni na udaku wa Instagram kuliko kutumia akili zetu wenyewe. Mtu yupo radhi kuamini udaku kwa vile tu unavuma zaidi hata kama hauna mantiki kuliko kutumia logic yake mwenyewe.

Endapo kulikuwa na mtu yeyote ambae alikuwa na nguvu kwa mama ilikuwa ni kabla ya kuapishwa kwake, baada ya hapo hawana tena kauli juu yake. Sawa sawa na ilivyokuwa kwa Magu, alipopewa madaraka tu hawakumuweza tena.
 
Ki binadamu, kila mtu ana karama yake. Tusiwalinganishe kiutendaji.
 
Sawa si kumwiga mtangulizi bali kurekebisha katiba yetu ili ikidhi haja ya uwajibikaji.
 
Ujinga gani? Jamni kwanini huwa hatuwezi kuvumiliana? Mtu anatoa maoni yake wewe unamtusi kweli hii ni sawa?

Anyway, ni kweli kwamba tunapaswa kuheshimu mamlaka ikiwa na pamoja na majukumu yake lakini ukweli ni kwamba kuna uonevu mkubwa mno wananchi maskini wanakumbana nao, kesi nyingi tu za kubambikizwa na viongozi wasaidizi wanakura rushwa, wengi sana wameteseka kesi zao hazitatuliwi ni kupigwa chenga tu je mnataka wananchi wafanye nini?

Mwananchi anapoenda kwa Rais ujue ameteseka sana na hakuna msaada wowote, kwa nature ya viongozi wetu hawa usishangae huyo mama hatapewa msaada wowote kumbuka mama alikataa mabango na shida za barabarani inamaana kusimama kwake ni sawa na kuwachoma wale viongozi then kesi imerudishwa kwa subordinate nini kitatukia?

Ukweli utabaki pale pale, kero za wananchi ni nyingi mno na hazitatuliwi!
Sawa ni KATIBA
 
Mkuu !!hizo Ziara mama kalazimishwa tu na hao waliompigania aapishwe kuwa namba moja!!Mama hataki kufanya kazi za watendaji na wakuu wa wilaya sema tetesi zinasema kachimbwa biti eti kaacha Legacy na Mwendazake!!!
Sawa ni KATIBA
 
Hiyo sio kazi ya Rais.Mwenye Kazi ya kutatua matatizo yako moja kwa moja ni ya balozi au mwenyekiti wako wa kijiji.
Ni vyema huu utaratibu ukaendelezwa kwani unampa Rais nafasi ya kusikia matatizo ya wananchi moja Kwa moja.
 
Back
Top Bottom