Rais Samia hatuhitaji tena ziara zako za barabarani, hazina msaada wowote kwetu

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Kwanza kabisa napenda kukupa pole na majukumu ya kitaifa.

Vile vile tunakuombea wewe na Serikali yetu katika utekelezaji mwema wa majukumu ya nchi ili kuinua uchumi.

Mweshmiwa Rais katika muda mchache huu umeonuesha matumaini ya watanzania kupata maisha bora, Ajira na uchumi kuinuka tena hongera sana na Mungu akubariki kwa hilo.

Niende kwenye lengo husika, katika siku za hivi karibuni umekuwa ukifanya ziara na kusimama barabarani kuongea na wananchi, lakini wananchi wanapopewa maiki kusema kero zao hakuna solution yoyote zaidi ya kusema unawaachia maofisa wako.

Mbaya zaidi kuna watu wanashida za muda mrefu mfano yule mama mjane juzi anakueleza shida yake, wewe kama Rais ilibidi uitatue pale pale kwa kuwahita wahusika wajibu, matokeo yake unamwambia awaone sijui wakuu wa mkoa sijui nani, kwani unafikiri ye alikuaga hawaoni?

Hii nchi ina watu wenye viburi kesi zinafichwa hata na ma OCD lakini mtu anapokuona wewe Rais anaona kama amepata mkombozi utatue swala lake.

Kama umeamua kuendeleza style ya mtangulizi wako ya kuongea na wananchi njiani basi endeleza na kutatua kero, JPM alikua kama imetokea kero anawaita wahusika kiwahoji pale pale na anatoa maamuzi pale pale.

Sasa Rais wangu wewe hufanyi hvyo, sisi wananchi tunakutegemea ww huku Uraiani kuna uonevu mwingi sana.

Mimi nafikiri kama utaendelea na style yako hii basi ziara za barabarani achana nazo hazina tija kwetu zaidi ya kutuongezea foleni na kutupotezea muda.
 
Acha ujinga. Rais anapaswa kujibu hoja za kitaifa zaidi, ambazo haziwezi kutatuliwa na wasaidizi wake walioko chini huko.
Vinginevyo mtampelekea hata kesi zenu za ndoa!

Pia huwezi toa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu!
 
Ujinga gani? Jamni kwanini huwa hatuwezi kuvumiliana? Mtu anatoa maoni yake wewe unamtusi kweli hii ni sawa?

Anyway, ni kweli kwamba tunapaswa kuheshimu mamlaka ikiwa na pamoja na majukumu yake lakini ukweli ni kwamba kuna uonevu mkubwa mno wananchi maskini wanakumbana nao, kesi nyingi tu za kubambikizwa na viongozi wasaidizi wanakura rushwa, wengi sana wameteseka kesi zao hazitatuliwi ni kupigwa chenga tu je mnataka wananchi wafanye nini?

Mwananchi anapoenda kwa Rais ujue ameteseka sana na hakuna msaada wowote, kwa nature ya viongozi wetu hawa usishangae huyo mama hatapewa msaada wowote kumbuka mama alikataa mabango na shida za barabarani inamaana kusimama kwake ni sawa na kuwachoma wale viongozi then kesi imerudishwa kwa subordinate nini kitatukia?

Ukweli utabaki pale pale, kero za wananchi ni nyingi mno na hazitatuliwi!
 
Mshezi mkubwa wewe, zilizokuwa za maana ni zile za mwendazake (misifa), Kwa taarifa yako ni kuwa mwendazake haingiii hata robo kwa huyu mama SSH kipenzi cha Wa Tanzania..
Duh haya balaa hii!

Hii mihemko inapaswa uipeleke Kwenye draft, msomi huwezi kuandika hivi, uwezo wako wa kufikiri ni mfinyu sana.

Comment yako ina reflect jina lako la mwisho! But mjifunze kuvumiliana, si wote watakuwa na mawazo sawa, akupingae usimuone adui, jenga hoja na si matusi.
 
Mkuu !!hizo Ziara mama kalazimishwa tu na hao waliompigania aapishwe kuwa namba moja!!Mama hataki kufanya kazi za watendaji na wakuu wa wilaya sema tetesi zinasema kachimbwa biti eti kaacha Legacy na Mwendazake!!!
 
Umeongea kwa HISIA MNO.

Nimekupata sana.

Ila acha KUKARIRI.

Rais ana nia njema tu na SAFARI HIZI ZINAZOENDELEZWA.

Mathalani ulitaka AWAPOKONYE ENEO LAO POSTA NA kulitoa kwa wale wafanyabiashara wa Morogoro waliomlilia ile jana?!!!

Haiwezekani.....haiwezekani ukabatilisha ENEO LA WAMILIKI tu ili "uwasaidie" watu waliotokea baadaye.

Yako maamuzi mengine hata hayati JPM alikuwa haamui tu Kama UNAVYOTAKA IWE.

#ZiaraZaRaisZiendelee
#SheriaZaNchiZiheshimiwe
#NchiKwanza
 
Katika utatuzi wa kero JPM aling'ara sana, he was talented, it will take us decades to see that happening again, mama hajakaa kikazi yupo kimaonyesho zaidi
Marais hawafanani.

Mama pia ana ubora wake mwingi tu.

Ndio Amiri Jeshi wetu mkuu.

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Mkuu !!hizo Ziara mama kalazimishwa tu na hao waliompigania aapishwe kuwa namba moja!!Mama hataki kufanya kazi za watendaji na wakuu wa wilaya sema tetesi zinasema kachimbwa biti eti kaacha Legacy na Mwendazake!!!
Kuna Watu hapa duniani mna PhD's za Uwongo na Hongereni kwa hilo pia. Na nasikitika kuwa wapo wanaowaamini kabisa.

Hivi Logically tu inakuingia Akilini kwa Mtu ambaye Kiserikali ni Commander In Chief na pia ndani ya Chama ndiyo Mwenyekiti Taifa halafu akatokea Mpumbavu wa Kumtisha na Kumshurutisha?

Acheni Kudanganyana huko Vijiweni Kwenu mnakoshinda na jifunzeni kuwa na Fikra pana zaidi.

Anachokifanya sasa Mama ( Rais ) Samia ni kwenda na rythm ya Hayati Rais Dkt. Magufuli iliyokubalika na Wanyonge ( Masikini ) wengi wa Tanzania ili azidi kuwateka Akili na mwaka 2025 akigombea rasmi Yeye kama Yeye imbebe katika Kura.

Picha halisi ya Kiuongozi ya Rais Samia utaanza kuiona kuanzia mwaka 2025 ( kama atagombea na kukubaliana na Dk. Hussein Mwinyi ambaye anautaka sana Urais wa huku Bara ) kwani kwa sasa Yeye ni 'Rais Deiwaka' tu baada ya aliyekuwepo Kufariki dunia na yupo hapo Kikatiba na siyo Kiuchaguzi.
 
Kwanza kabisa napenda kukupa pole na majukumu ya kitaifa.

Vile vile tunakuombea wewe na Serikali yetu katika utekelezaji mwema wa majukumu ya nchi ili kuinua uchumi,

Mweshmiwa Rais katika muda mchache huu umeonuesha matumaini ya watanzania kupata maisha bora, Ajira na uchumi kuinuka tena hongera sana na Mungu akubariki kwa hilo.

Niende kwenye lengo husika, katika siku za hivi karibuni umekuwa ukifanya ziara na kusimama barabarani kuongea na wananchi, lakini wananchi wanapopewa maiki kusema kero zao hakuna solution yoyote zaidi ya kusema unawaachia maofisa wako.

Mbaya zaidi kuna watu wanashida za muda mrefu mfano yule mama mjane juzi anakueleza shida yake, wewe kama Rais ilibidi uitatue pale pale kwa kuwahita wahusika wajibu, matokeo yake unamwambia awaone sijui wakuu wa mkoa sijui nani, kwani unafikiri ye alikuaga hawaoni?

Hii nchi ina watu wenye viburi kesi zinafichwa hata na ma OCD lakini mtu anapokuona wewe Rais anaona kama amepata mkombozi utatue swala lake.

Kama umeamua kuendeleza style ya mtangulizi wako ya kuongea na wananchi njiani basi endeleza na kutatua kero, JPM alikua kama imetokea kero anawaita wahusika kiwahoji pale pale na anatoa maamuzi pale pale.

Sasa Rais wangu wewe hufanyi hvyo, sisi wananchi tunakutegemea ww huku Uraiani kuna uonevu mwingi sana.

Mimi nafikiri kama utaendelea na style yako hii basi ziara za barabarani achana nazo hazina tija kwetu.
Kweli kabisaaaa...kama hatatui shida hapo kwa hapoo..baas hakuna haja ya kusimama..otherwise anawapotezea muda wafanya biashara na wafanyakaz wa eneo husika
 
Back
Top Bottom