Rais Samia Hassan anatekeleza kampeni ya Tundu Lissu ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
2,994
2,000
Wanabodi, ni dhahiri Mpaka sasa Mama Samia Suluhu Hassan anatekeleza maneno aliyohubiri Tundu lissu wakati wa kampeni mwaka 2020,Yalikuwa maneno matatu tu yaani Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.

CCM walipozidiwa hoja na Tundu Lissu wakaamua kuzima intaneti, wakatunga hali ya hewa ni mbaya kwa helikopta kutua.

Uhuru, Ahadi ya Lissu ilikuwa Maendeleo ya vitu bila uhuru ni sawa na bure, Lisu aliahidi kufuta kesi zisizo na ushahidi mfano kesi za Mashehe wa uhamsho, Kesi za uchochezi za kusema na kujadili mamlaka ya Urais. Mama Samia alishafuta kesi za Mashehe wa uhamsho na baadhi za akina Papa Msofe za utakatishaji pesa.

Maendeleo ya watu na sio Maendeleo ya vitu, Lissu alihubiri watu lazima wawe na maisha yenye unafuu kuwalipa penseni na mafao yao, Kuongeza mishahara yao, Jeshi la polisi wakati wa kampeni lissu alisisitiza wana hali ngumu hawajapandishwa vyeo wala mishahara kwa miaka mitano, Mama Samia ameanza kuwapandisha vyeo Polisi na Pension kidogo watu wameanza kulipwa.

Haki, Tundu lissu alihubiri haki wakati wa kampeni 2020. Aliwasema watawala wanaokaa juu ya katiba na kutumia Madaraka kunyanyasa watu, Leo hii Mama Samia kidogo ameanza kutekeleza, Ole Sabaya mtu mwizi na tapeli amemuweka pembeni kupisha Uchunguzi wa Takukuru.

Wakati wa kampeni mwaka 2020 nilisisitiza CCM hatuna hoja za kumjibu Tundu Lissu, Tundu lissu aliizidi ccm kwa kila kitu mwaka jana uwezo wa kujenga hoja, uwezo wa kushawishi na Smartness kichwani, Matokeo yake ikatumika nguvu kupora uchaguzi

Lakini sasa, CCM ile ile inatekeleza ahadi na Sera za Tundu lissu, CCM ilikuwa inahubiri kupora Fedha kujenga miradi lakini Leo wanasubiri ahadi zenye mashiko za Tundu lissu uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.

Ni vyema ccm wakaelewa upinzani ni imani na itikadi, Upendo haulazimishwi. Miaka mitano ilitumika kuwalazimisha watu kuipenda ccm kinguvu kwa biashara ya manunuzi na ni kweli baadhi walinunulika kutajirisha matumbo yao lakini sasa ni dhahiri Chadema inasonga mbele kwenye operesheni zake za Chadema Kidijitali zaidi.

CCM inatumia mbinu za kizamani sana, Mbinu za kisasa mpinzani wako sio adui bali anakusaidia kukujenga, Kwa sasa Chadema wapo Kidijitali na wanahubiria wanachama wao kuhusu teknolojia, CCM kimya.
Crap
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
41,878
2,000
Kwa mantiki hiyo Chadema imeshinda uchaguzi na Lisu ndio Rais.

Kimsingi ww hatuwezi kukulaumu maana ww ni wa kizazi kinachoishia kinachoamini kwa ccm kutawala no matter what. Kwa taarifa yako ccm ni chama cha kizazi kilichopita, ndio maana kinatumia mabavu, hila na ghiliba kuendelea kubaki madarakani, lakini kiukweli kimeshapoteza ubunifu na hasa hasa ushawishi.

Kutokana na mahitaji ya muda, iwapo angetokea masiha huko ccm angewashauri wakubali katiba mpya kukiwa na amani, kisha washiriki kwenye uchaguzi halali, wakishinda washinde kihalali, na wakishindwa wakubali kisha wajijenge upya kama wataweza kweli kuendelea kubaki kwenye siasa za ushindani, japo naona hili ni gumu kwao kwani sehemu kubwa wanategemea mbeleko ya vyombo vya dola kuliko ushawishi. Binadamu yoyote huwa ana tabia ya kuchoka, kwa sasa wananchi wameshaichoka ccm, na ccm hata ifanye nini, haiwezi kuwa na ushawishi wowote, zaidi ya kutumia mabavu na ghiliba kubaki madarakani. Hivyo ccm ielewe iko nje ya muda, hata itumie nguvu, na kuhonga wapinzani vyeo, bado hali yao itakuwa ngumu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom