Rais Samia hapendi kodi na mali za dhuluma; vipi kuhusu viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na CCM?

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Moja kwa moja kwenye mada. Mheshimiwa Rais wetu mpendwa mama yetu mama Samia Suluhu Hasani amjipambanua na kweli ukimuangali usoni unaona kabisa kuwa mama hapendi mambo ya dhulma ikiwemo kodi.

Hoja yangu ni juu ya mali ilizojimilikisha CCM baada ya uwepo wa mfumo wa vyama vingi. Nitajikita katika viwanja vya michezo ikiwemo Kirumba Mwanza, Kambarage Shinyanga, Al Hasan Tabora, Samora, Karume n.k.

Kusema ukweli viwanja hivi havikujengwa na CCM. Viwanja hivi vimejengwa na wananchi wote wa Tanzania waliokuwepo wakati huo. Kumbuka utaratibu wa ukusanyaji kodi wa wakati huo haukuwa wa kueleweka, hivyo isingekuwa rahisi wizara ya fedha kupitia bajeti za serikali kujenga viwanja hivi.

Njia rahisi iliyoonekana inawezekana kuwa na viwanja hivi ilikuwa ni kuwachangisha wananchi. Jambo la kutafakari ni kwamba hakuwahi kuwepo mkutano wa hadhara wa wanaCCM au mkutano mkuu wa wanaCCM ulioidhinisha kuwachangisha wanachama wa chama cha mapinduzi kuridhia kujenga viwanja hivi.

Jambo lililofanyika ni mamlaka za serikali kuu au serikali za mitaa kuwatoza wananchi michango ya lazima wananchi wote bila kuuliza uanachama wake. Uwe mwanachama, usiwe mwanachama ulichangia utake, usitake labda kama unataka kufa. Utaratibu uliotumika ni ufuatao:

1) Mchango kupitia nauli za mabasi: Bila kujali unaenda hospitali, shuleni, msibani au polisi katika nauli za kusafiri kuliongezwa pesa ya mchango wa ujenzi wa uwanja. MHESHIMIWA RAIS, HAPO TUNAWEZA KUSEMA CCM IMEJENGA VIWANJA?

1) Katika manunuzi ya bidhaa
 
Na siasa za dhulma je? Jana pale Mwanza Nusrat Hanje amepandishwa jukwaani akajitambulisha kama mbunge wa chadema anayewakilisha vijana mkoa wa Singida.

Huku akijua walishavuliwa uanachama. Kwann mama SSH ameruhusu dhihaka hii? Anabariki dhulma ktk siasa?
 
Viwanja vilijengwa kwa njia ya kutoza kodi mfanokirumba bidhaa zote za viwandani zilizokuwa zinakuja kanda ya ziwa ziliwekewa kodi maarumu kwaajili ya ujenzi wa kiwanja,wakulima walikatwa kwenye mauzo ya pamba wakakusanya hizo fedha kwa njia ya kutoza kodi, namna yapili ilikuwa ni michango yalazima kwa wakulima na wafanyakazi haikuwa hiali hiyo nayo ni kodi.

Kwa ujumla hata CCM wanajua kuwa viwanja hivi sio mali yao ni mali ya wananchi wa Tanzani.
 
1) Katika manunuzi ya bidhaa

Bila kujali unamnunulia nani bidhaa kila bidhaa iliongezwa mchango wa viwanja. Mfano sukari kwa uji wa mgonjwa, mchele kwa chakula cha watoto, jembe na fyekeo vya mtoto anayeenda kuanza form one, shoka la mkulima, kitambaa cha sanda ya kuhifadhia maiti vyote vikiongozwa bei ili kujenga viwanja.

Ndugu wananchi mnajua kabisa maduka yaliyokuwa na bidhaa ni ya RTC, ungekwepea wapi kuchanga pesa hiyo? MHESHIMIWA RAIS HAPO TUNAWEZA KUSEMA KUWA VIWANJA NI MALI YA CCM?
Kwingine waliweka kamba barabarani ili uoneshe stakabadhi ya mchango wa viwanja, hawakuuliza kadi za CCM. MHESHIMIWA RAIS HAPO TUNAWEZA KUSEMA KUWA VIWANJA NI MALI YA CCM?

Lakini hebu tujiulize kidogo. Kwanini uwanja wa Mkapa sio wa CCM? Si umejengwa chini ya utawala wa CCM? Au Kama umejengwa chini ya vyama vingi kwanini CCM, CHADEMA, CUF, TLP, TADEA e.t.c wasiwe na share? Utasema umejengwa kwa kodi sio wanachama? Kama hivyo ndivyo, ni viwanja gani vimejengwa na wanachama?

Mama ameagiza anayeshutumu, au kulalamika aje na njia mbadala.

Mimi nakuja na njia kwamba viwanja vyote viwekwe chini ya halmashauri za miji na majiji, huyo ndiye mmiliki halali wa viwanja hivyo. Na kwakuwa alikuwa na uwezo wa kuijenga vilevile anao uwezo wa kuvikarabati na kuviboresha.

Mama Samia, Kama ilivyofanya Madudu ya Sabaya, ambaye kwa utawala fulani alikuwa bora ndivyo ufumue Madudu ya CCM ambayo kwa tawala ladhaa yalionekana sahihi wakati si kweli!!!

Kwa kweli ujenzi wa viwanja vilisimamiwa na ofisi za mikoa za serikali. Ilifika wakati inakutana na kizuizi cha kamba barabarani inauliza stakabadhi ya mchango wa ujenzi wa viwanja, hawakuuliza kadi ya CCM. Rais wetu mpendwa, hebu tuweke sawa tuanze upya.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Moja kwa moja kwenye mada. Mheshimiwa Rais wetu mpendwa mama yetu mama Samia Suluhu Hasani amjipambanua na kweli ukimuangali usoni unaona kabisa kuwa mama hapendi mambo ya dhulma ikiwemo kodi.

Hoja yangu ni juu ya mali ilizojimilikisha CCM baada ya uwepo wa mfumo wa vyama vingi. Nitajikita katika viwanja vya michezo ikiwemo Kirumba Mwanza, Kambarage Shinyanga, Al Hasan Tabora, Samora, Karume n.k.

Kusema ukweli viwanja hivi havikujengwa na CCM. Viwanja hivi vimejengwa na wananchi wote wa Tanzania waliokuwepo wakati huo. Kumbuka utaratibu wa ukusanyaji kodi wa wakati huo haukuwa wa kueleweka, hivyo isingekuwa rahisi wizara ya fedha kupitia bajeti za serikali kujenga viwanja hivi.

Njia rahisi iliyoonekana inawezekana kuwa na viwanja hivi ilikuwa ni kuwachangisha wananchi. Jambo la kutafakari ni kwamba hakuwahi kuwepo mkutano wa hadhara wa wanaCCM au mkutano mkuu wa wanaCCM ulioidhinisha kuwachangisha wanachama wa chama cha mapinduzi kuridhia kujenga viwanja hivi.

Jambo lililofanyika ni mamlaka za serikali kuu au serikali za mitaa kuwatoza wananchi michango ya lazima wananchi wote bila kuuliza uanachama wake. Uwe mwanachama, usiwe mwanachama ulichangia utake, usitake labda kama unataka kufa. Utaratibu uliotumika ni ufuatao:

1) Mchango kupitia nauli za mabasi: Bila kujali unaenda hospitali, shuleni, msibani au polisi katika nauli za kusafiri kuliongezwa pesa ya mchango wa ujenzi wa uwanja. MHESHIMIWA RAIS, HAPO TUNAWEZA KUSEMA CCM IMEJENGA VIWANJA?

1) Katika manunuzi ya bidhaa
Hivyo viwanja ni mali ya CCM maana ilikuwa ni lazima kwa Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuwa mwanachama wa CCM, kwa hiyo viwanja hivyo vilijengwa na wana CCM. Over
 
Inasemekana habari za chinichini kuwa kwa sasa yeye ni mtu au yupo serikalini hayupo kwenye chama ,na mambo hayo hushughulikiwa na upinzani siku kimoja ya chama pinzani kitapofanikiwa kushinda kwa kura za halali, hivyo vitu vitamilikishwa serikali ya mkoa ili kuimarisha mipango ya serikali ,ni suala la muda tu na ccm wanalijua hilo kuwa hivyo vitu ni walidhulumua kwa hiyo wanakula na kubugia hela ya dhuluma,vyote hivyo vitaingia kwenye serikali za mkoa na wilaya.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom