Rais Samia hajakosea kusema 2025 mwanamke atakuwa Rais tena

Jul 29, 2021
81
158
Nimesoma nakala moja inasema "Rais Samia amekosea tena..." Amekosea kwasababu ya kusema kuwa mwaka 2025 atachukua mwanamke tena. Na nikasoma pia watu waki comment kuwa yeye ana inferiority complex, yaani, ana ile hali ya kujiona yuko chini kwakuwa yeye ni mwanamke. Mimi sikubaliani na hayo kwasababu zifuatazo;

Kwanza, mama Samia hajakosea kutumia wanawake Kama sera yake ya siasa, na sio kwasababu tu yeye ni mwanamke, ila ni kwasababu siasa ya Tanzania inaruhusu hivyo.

Hebu tuangalie Ni sera ya aina gani ambazo hutumika kwenye siasa zetu hapa Tanzania. Kwenye kipindi cha uchaguzi kilichopita, sera mbalimbali zilitumika mfano sera ya Ubwabwa ambapo mgombea alikuwa akiwapa chakula wakati wa kampeni, kuleta wanamziki kutumbuiza wakiwa wamevaa nguo za chama husika, kuwatumia wamachinga na sera nyinginezo.

Hivyo kama ni ubovu wa sera, chimbuko lake lipo kwenye mfumo wa jinsi wanasiasa wanavyotakiwa kufikisha sera zao kwa wananchi. Badala ya kusimama na kusema ni jinsi gani watakavyo tatua matatizo yetu, wanatumia vionjo ambavyo hutupa raha ya muda tu, na sisi Kama wajinga tunavikubali.

Kwahiyo, Mama Samia hajakosea wala hana 'Inferiority Complex' kama wengi wanavyodhani. Ila tu anatumia nafasi "loopholes" zilizopo kwenye mfumo wetu wa kisiasa hapa Tanzania.

Na sisi kama vijana 'Taifa la kesho' ni wajibu wetu kuhakikisha mfumo mzuri wa kisiasa unaanzishwa nchini mwetu. Mfumo nilionao kichwani, ni mfumo wa majibizano 'Debate', amabapo wapinzani watasimamishwa pamoja, wakijibu maswali ambayo yanakuwa yameandaliwa, kutoka kwa wananchi.

Haya maswali yanakuwa ni mchanganuo wa matatizo ambacho wananchi wanakabiliwa nayo. Na wagombea hao watatakiwa kuonyesha ni jinsi gani watakavyo tatua haya matatizo. Na sio kupoteza pesa kwenye ubwabwa na kuleta wanamziki alafu mwisho wa siku tunachagua Viongozi haba.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK

User mpya kwa kazi maalumu
 
Back
Top Bottom