Wimbo
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 783
- 524
Mama Mpendwa Shalom
Mwenendo uliopo mpaka sasa, japo tunakupongeza kila kona kwamba unaupiga mwingi mambo ni magumu.
Hawa walioko vijijini ambao ndo hasa wapiga kura wako hawajui habari ya Ukraine na Putin wao, wanachokihitaji wapate maisha ahueni, wakati nchi nyingi zilizoathirika kama sisi zinajipanga kutenga ruzuku ya kugharamia mfumuko wa bei ya mafuta sisi tunaibandika ilivyo na hata wabunge wengine wanalalama ati Waziri ameondoa tozo.
Mama mahali penye njaa na mateso hapawezi kuwa na amani. Ongezeko zaidi ya ya asilimia 50% ya diesel toka umeshika madaraka hata kama linasababishwa na external forces lazima njia mbadala za kulegeza nati litafutwe.
Najua unao washauri wengi Wazuri Wa uchumi na siasa lakini nikuombe Mama yetu iangalie Tanzania, kiangalie Chama chetu CCM wengine wanaweza kukushauri kwa maslahi binafsi watu wengi wakaumia.
Huyo mama unayemtetea kila siku anayeuza mbogamboga alikuwa analipa tsh 500 kupanda bajaji Jana bei imepanda nauli Tsh 1000/- tumemrudisha nyuma sana. Usifurahie akina mama hao na madira yao wapiga iyenaiyena "mama anaupiga mwingi" wengine wanafiki tu na wengi wao hawajui machungu ya mama Wa kijijini ambaye bado anaishi kwa Jembe la mkono.
Punguza gharama za uendeshaji wa serikali yako tenga ruzuku ya mbolea na mafuta na kupigania bei za mazao ya wakulima wetu wanyonge, pambana reli zikamilike haraka ili kupunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazonunua mafuta, kile kitengo cha kukusanya dhahabu zetu ili kuwa na reserve itakayotusaidia kubalance currency yetu kiangalie vizuri.
Lakini usiache kuwa mhubiri kwa hao wanaojikusanyia huku wengine wakilala na njaa, wambie maisha hayazidi miaka 120 na hakuna atakayeondoka na kitu.
Tunapoadhimisha nia tukufu za waasisi Wa Nchi yetu tujiweke kwenye mzani tujipime baada yetu yepi yataubeba uwepo wetu.
Umewahi kusema nafasi hii umeruzukiwa na Mungu. Ni kweli wewe kama wewe usingeshinda uchaguzi ule, ( huu no mtazamo wangu) kama ndivyo Mungu aliandaa kusudi jema kwako na kwa Nchi yetu Msikilize Yeye.
Amekuweka ili uivushe Tza ng'ambo ya mafanikio usisahau usipofanya maagizo yake Mungu ni mkali mno.