Rais Samia: Demokrasia ni kuheshimu Sheria, heshima ya Mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za Nchi, ombi la Zitto kuhusu kesi ya Mbowe lajibiwa

“Nataka nijibu lile ombi la mwanangu, iko hivi demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima.
.
“Heshima ya mtu inakuja unapoheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, Serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine,” - Samia H. Suluhu
Nukuu hii inaonesha kisa cha kukamatwa na uamuzi uliopangwa kuhusu kesi. Unapokuwa na kesi ambayo Rais amehadithiwa na maamuzi ya kesi yaliyokwisha fikiwa! Hili ni tatizo kwenye utawala wa sheria.
 
Mama aliona Mbowe kama anataka kumpanda kichwani kwa kampeni yake ya katiba mpya.

Hapa inadhihirisha tuhuma za Mbowe ni za kubumba.... Na pia kumwonyesha tu kuwa huwezi kushindana na serikali
Wakati Rais anaonesha fika kwamba kikombe cha MBOWE kimeshaishinda serikali,hii ni poor planning
 
Mimi ningependa Mbowe afungwe jela na kifungo chake ndicho kitapelekea Watanzania kwa wingi kukiondoa chama changu cha CCM madarakani kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

Huu ni mtizamo wangun
I think ni good ideas, ingawa wengi watakua against
 
Kuna kitu mbowe wamepishana na Samia.
Kila kiongozi akiingia madarakani Kuna watu lazma atawanyoosha.
Mimi nakumbuka magufuli na manji.
Kikwete na Babu seya.
Kiufupi hyo kesi wametengeneza na wanaweza kumfunga.maana wamedhamiria
Kumfunga ni political suicide kwa Samia,na sasa ameshaanza kuliona hilo vyema- Serikali inatafuta namna ya kuifuta hii kesi pasipo wananchi kuelewa vyema kupitia script za kina Zitto,changamoto ni kwamba script imeshavuja mapema kabla hawajai-execute
 
Kutofuata Sheria na kukosa heshima afanye Mbowe, mateso ya kuchomwa mshikaki yamwendee Adamoo, Ling'wenya na akina Urio??? Hii heshima ina gharama sana.
 
angalau hata hiyo nafasi imepatikana na leo tunaweza kupata habari....sasa ZZK naye asingeenda au wote tungesusia hiyo habari tungeitoa wapi...
Kwa jinisi kesi ilivyofika, maji yashawafika shingoni. Kama asingesema kwenye mkutano wa vyama vya siasa angeweza kusema mahali popote pale! Period!
 
Kumfunga ni political suicide kwa Samia,na sasa ameshaanza kuliona hilo vyema- Serikali inatafuta namna ya kuifuta hii kesi pasipo wananchi kuelewa vyema kupitia script za kina Zitto,changamoto ni kwamba script imeshavuja mapema kabla hawajai-execute
"Tatizo muda"
 
Rais hana cha kufanya zaid ya kumwachilia Mbowe manake ndoano lazima aitapike,pressure imekuwa kubwa mno kwake
Nimesoma comments za watanzania kwenye page ya milladayo aisee wamemjibu ni balaa.Si kwa matusi hapana,bali kwa maovu na unyanyasaji wooote unaofanywa na upande wa Rais/ mwenyekiti wa ccm. Watu wana evidences balaa.Wanachambua uchaguzi wa serikali za mitaa,uchaguzi mkuu,matukio ya risas,kuumizwa na kupotezwa watu si mchezo.

Kuna jambo la kujitafakari wao na si kuainisha upande wa upinzani kuwa una shida kumbe chanzo ni wao.



Nimeogopa maneno ya mama mdogo wa mbowe,ni kama ya mama Kabendera.Naogopa kiongozi kuanguka akiwa madarakani tena kwani maneno yale si mazuri.
 
Yaani univunjie hotel niliyokuwa napata riski yangu
Yaani unifyekee bustani yangu ya mbogamboga iliyokuwa inanipa riski yangu
Yaani unifungie account zangu za benki zote ambazo nilikuwa naweka akiba zangu kwa miaka.
Yaani uniweke ndani miezi minne kwa kosa la kuandamana na kusababisha kifo cha akwilina..
Yaani watu naowaongoza uwaumize, uwape kesi za kubambika kukomoana
Yaani ukanivunja mguu wangu, nikajitibia nikapona..sikukata tamaa
Yaani wagombea wetu 60% uwateke, uwanyike sifa za kugombea bila sababu za msingi..
Yaani mawakala wetu uwazuie nje na wakitaka kuingia unawafungulia kesi ya vurugu kituo cha uchaguzi
Yaani viongozi wenzangu wapotee, waumizwe wengine wabakie vilema huku naona...

Kwa yote haya nikapiga kifua changu nikamwambia MUNGU wangu ayasamehe- nikasamehe.... Baada tu ya Urais wako nikaja kwako kwa unyenyekevu mkubwa nikakuomba tukutane tuyajadili kwa kina ili tufikie muafaka ama maridhiano ya kitaifa - ukawa kimya kwa maana nyingine hukutaka.

Leo umenipa kesi ya UGAIDI, nasota gelezani ni sawa , ila kweli leo unaniambia nini sina HESHIMA, kweli ndugu ?? Hapana, kwa hili hapana Hapana umenikosema sana.
Duuu very painful
 
Back
Top Bottom