kookolikoo
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 2,751
- 595
Afungwe kwanza ndipo mama amsamehe.
Afungwe kwanza ndipo mama amsamehe.
Mnashindwa vipi kuheshimu wengine ili muheshime.. hivi akili zenu zina akili kweli.Heshima haina gharama. lakini nyie mnaona matusi ni mtaji.
Nani kaomba msamaha au kasema aombe msamaha.?Ikiwa Mbowe hana hiyo jinai na wahusika wanajua hilo lakini hawakiri ukweli ni bora aachwe muda utaongea kwani njia ya mwongo ni fupi. Unaombaje msamaha kwa kosa usilotenda?
Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Sawa mkuu......Rais kasema '' Kama asingevunja sheria tungekuwa naye hapa''
Kauli hii inafanana na ile ya BBC kwa mantiki
Kwamba Rais anaongelea suala lililopo mahakamani. Pili Rais anamtuhumu Mbowe .
Akiwa mkuu wa nchi tayari ana influence maamuzi ya mahakama kwamba,Mbowe ana makosa . Ni Jaji gani Tanzania atakayekwenda kinyume na Rais?
Waliambiwa '' hukumu zenu zizingatie hali ya nchi''
Rais anasema ' kuna kusameheana''.
Kusamehe kunatokea penye kosa, tayari keshamtia Mbowe hatiani na anataka kumsamehe.
Nadhani anapoongea kwa hasira anasahau ni Rais na hivyo kueleza hisia zake na kusahau nafasi yake. Kauli zake za leo hazikumtendea haki Mbowe , zimeingilia mahakama.
Hivi kwanini Wasadizi wa Rais hawamshauri kuhusu masuala ya mahakamani?
Hivi CJ ana maoni gani kuhusu hili na kwamba ameshindwa hata kumnong'oneza
Alinda JokaKuu
Lakini kiongozi kwenye utawala wa sheria chombo pekee kinachopaswa kutoa haki ni mahakama.......kushinikiza kuwa aachiwe huru Hali ya kuwa kesi ipo mahakamani huoni kwamba ni kuvuruga utawala wa sheria....??
Kwa kweli Rais leo kanifungua macho. Nilikuwa najiuliza sana juu ya ugaidi wa Mbowe. Inakuwaje Mbowe awe gaidi? Leo nimepata jibu toka kwa mama. Akina Mama wana majibu. Kasema kosa la Mbowe ni kutofuata sheria na kumkosea heshima mtu fulani. Kazi tuliyonayo na mawakili wa mbowe watusaidie kumtafuta huyo ambaye alimshitaki Mbowe kwa kumkosea heshima.Kuna maswali muhimu ya kujiuliza
Afuate sheria gani? Kavunja sheria gani?
Amheshimu nani? Ni nani kamkosea heshima?
Kwahiyo kesi yake sio ugaidi tena? Bali ni maswala ya sheria na heshima?
Kwani imeshathibitika kwamba Mbowe aliratibu vitendo vya ugaidi? Mbona kesi inaendelea sasa.Sawa mkuu......
Tujikite kwenye mzizi wa mada hii.....
Kuratibu au kuendesha vitendo vya kigaidi ni kosa kisheria na anayefanya anakuwa amevunja sheria.......kauli ya raisi kuwa kama hangevunja sheria angekuwa hapa nadhani ameakisi na kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya tuhuma za Mbowe.......
Kuheshimu sheria ni pamoja na kujipusha na vitendo au matukio yanayopelekea uvunjifu wa sheria......
Kwa mujibu wa utaratibu wa nchi yetu mahakama pekee ndio chombo Cha kutoa haki.....
Kuhusu kusameheana bila shaka amelenga mamlaka aliyokuwa nayo kama mkuu wa nchi kuhusu misamaha dhidi ya wafungwa na sio kesi zinazoendelea mahakamani.......
Hapana mkuu sijasema kuwa Mbowe amethibitika kuwa ni gaidi bali nimeichukulia kama mfano kutokana kauli ya mama....Kwani imeshathibitika kwamba Mbowe aliratibu vitendo vya ugaidi? Mbona kesi inaendelea sasa.
Sasa kwanini watu wanamwombea msamaha mbowe kwa Mama? Mbowe kamfanyia kosa gani mama?Hapana mkuu sijasema kuwa Mbowe amethibitika kuwa ni gaidi bali nimeichukulia kama mfano kutokana kauli ya mama....
Nadhani ni hulka tu na mitazamo ya watu juu ya jambo hilo.....lakini kimantiki kesi ya Mbowe ipo mahakamani na itaamuliwa kwa mujibu wa sheria.,....Sasa kwanini watu wanamwombea msamaha mbowe kwa Mama? Mbowe kamfanyia kosa gani mama?
Lakini mbona Mama anaonyesha kama vile hatima ya Mbowe ipo mikononi mwake vile? kwa mba amevunja sheria na hayamheshimu, katika lipi?Nadhani ni hulka tu na mitazamo ya watu juu ya jambo hilo.....lakini kimantiki kesi ya Mbowe ipo mahakamani na itaamuliwa kwa mujibu wa sheria.,....
Hapana nina hakika hana maana hiyo kwa kuzingatia kuwa yeye ni muumini wa utawala wa sheria......nadhani watu ndio wamechagua kumuelewa hivyo......Lakini mbona Mama anaonyesha kama vile hatima ya Mbowe ipo mikononi mwake vile? kwa mba amevunja sheria na hayamheshimu, katika lipi?
Misingi ya uzalendo ndo ipi hiyo?Mh. Zitto nadhani leo ndiyo kaelewa urais ni taasisi na siyo mtu. Ajifunze na yeye kuwa na adabu. Maana alidhani atasema kiurahisi tu Mbowe atolewe. Mbowe yeye asubiri kama ilivyokuwa kwa Sabaya. Maana mlifurahi sana kwa Sabaya. Inabidi tufike pahala hii nchi iendeshwe kwa misingi ya uzalendo
Sina uhakika kama umemsikiliza vizuri. Majibu yake yana ujumbe ambao unaonyesha wazi kabisa kwamba Mbowe ana hatia kwa sababu kavunja sheria na amekosa heshima. Mimi naona angejibu tu kwamba hilo la Mbowe tuiachie mahakama, basi.Hapana nina hakika hana maana hiyo kwa kuzingatia kuwa yeye ni muumini wa utawala wa sheria......nadhani watu ndio wamechagua kumuelewa hivyo......