Rais Samia: Demokrasia ni kuheshimu Sheria, heshima ya Mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za Nchi, ombi la Zitto kuhusu kesi ya Mbowe lajibiwa

Hapana nina hakika hana maana hiyo kwa kuzingatia kuwa yeye ni muumini wa utawala wa sheria......nadhani watu ndio wamechagua kumuelewa hivyo......
Sina uhakika kama umemsikiliza vizuri. Majibu yake yana ujumbe ambao unaonyesha wazi kabisa kwamba Mbowe ana hatia kwa sababu kavunja sheria na amekosa heshima. Mimi naona angejibu tu kwamba hilo la Mbowe tuiachie mahakama, basi.
 
All animals are equal, but some are more equal than others.

Wale jamaa wa uhamsho aliotoa pressure waachiwe walikuwa watii wazuri wa washeria sana na sio wavunja amani kule Zanzibar.

Ebu huyu mama awe consistent walau kwenye matamko na matendo yake.
 
Rais kasema '' Kama asingevunja sheria tungekuwa naye hapa''

Kauli hii inafanana na ile ya BBC kwa mantiki

Kwamba Rais anaongelea suala lililopo mahakamani. Pili Rais anamtuhumu Mbowe .
Akiwa mkuu wa nchi tayari ana influence maamuzi ya mahakama kwamba,Mbowe ana makosa . Ni Jaji gani Tanzania atakayekwenda kinyume na Rais?
Waliambiwa '' hukumu zenu zizingatie hali ya nchi''

Rais anasema ' kuna kusameheana''.
Kusamehe kunatokea penye kosa, tayari keshamtia Mbowe hatiani na anataka kumsamehe.

Nadhani anapoongea kwa hasira anasahau ni Rais na hivyo kueleza hisia zake na kusahau nafasi yake. Kauli zake za leo hazikumtendea haki Mbowe , zimeingilia mahakama.

Hivi kwanini Wasadizi wa Rais hawamshauri kuhusu masuala ya mahakamani?
Hivi CJ ana maoni gani kuhusu hili na kwamba ameshindwa hata kumnong'oneza

Alinda JokaKuu
Nafikiri kama taifa tumefika sehemu ambayo Mahakama haziheshimiwi Tena na viongozi wetu...

Kipindi cha nyuma tulizoea kusikia kesi iko Mahakamani hivyo siwezi iongelea... Tofauti na Sasa Viongozi wetu ndo wamekuwa wapanda majukwaa na kutoka maelezo ni nini kifanyike na nini kisifanyike Mahakamani, na hapo hapo wanatuhimizi Sisi wananchi tusio na vyeo Tena kwa msisitizo kuheshimu sheria...

Bado nawaza Tanzania miaka 60 ya uhuru....
 
Sawa mkuu......

Tujikite kwenye mzizi wa mada hii.....

Kuratibu au kuendesha vitendo vya kigaidi ni kosa kisheria na anayefanya anakuwa amevunja sheria.......kauli ya raisi kuwa kama hangevunja sheria angekuwa hapa nadhani ameakisi na kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya tuhuma za Mbowe.......
Sheria inasema . mtu anabaki bila hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha.
Je, Mbowe ameshathibitishwa ana hatia? Ni mahakama ipi iliyotoa hukumu
Nani amebaini makosa ya Mbowe nje ya mahakama?
Huoni Rais ana influence hukumu ya Mbowe nje ya Mahakama

Kuheshimu sheria ni pamoja na kujipusha na vitendo au matukio yanayopelekea uvunjifu wa sheria......
Mahakama gani imethibitisha uvunjaji wa sheria na nani alihusika
Kwa mujibu wa utaratibu wa nchi yetu mahakama pekee ndio chombo Cha kutoa haki.....
Well, Rais alsema wenzake wa,eshafungwa, alimhukumu nje ya mahakama. Jana kasema asingevunja sheria, kamuhukumu nje ya mahakama!
Kuhusu kusameheana bila shaka amelenga mamlaka aliyokuwa nayo kama mkuu wa nchi kuhusu misamaha dhidi ya wafungwa na sio kesi zinazoendelea mahakamani.......
Rais anamsamehe vipi mtu ambaye hajathibitika ana makosa? Hivi wewe kuna mtu anaweza kukusamehe hapo ulipo! Mbowe hajapatikana na hatia hivi anasamehewa kwa kosa gani na kutoka mahakama gani?
 
Nafikiri kama taifa tumefika sehemu ambayo Mahakama haziheshimiwi Tena na viongozi wetu...
Kesi ya Mbowe imefunua Mahakama na jinsi inavyotumika na vyombo vya Umma
Unakumbuka kauli ''Mahakama izingatie hali ya nchi' na si kuzingatia sheria !
Kipindi cha nyuma tulizoea kusikia kesi iko Mahakamani hivyo siwezi iongelea... Tofauti na Sasa Viongozi wetu ndo wamekuwa wapanda majukwaa na kutoka maelezo ni nini kifanyike na nini kisifanyike Mahakamani, na hapo hapo wanatuhimizi Sisi wananchi tusio na vyeo Tena kwa msisitizo kuheshimu sheria...
Kesi hii Rais ameiingilia sana, hukumu yoyote itahusishwa na kauli za Rais
Kule BBC tulidhani ni 'tongue slip'' jana imeondoa shaka kuwa Rais ana influence mahakama
Huwezi kuzungumzia kesi ya mtuhumiwa iliyopo mahakamani katika jukwaa la siasa
Mbowe hakupewa nafasi ya kujitetea katika jukwaa hilo alilotumia Rais kusema 'amevunja sheria'

CJ kakaa kimya bila kujua mahakama chini ya uongozi wake inavyopoteza credibility and integrity

Hii si mahakama ya akina Nyalali, Kisanga, Lugakingira!
Bado nawaza Tanzania miaka 60 ya uhuru....
Tunasababu za kumlaani mkoloni
 
Kitimoto leo "umecheua"?Nimemiss "dislikes" zako mwanzo mwisho.Unaonekanaga juha sana.😝😝😝😝😝
Mimi ningependa Mbowe afungwe jela na kifungo chake ndicho kitapelekea Watanzania kwa wingi kukiondoa chama changu cha CCM madarakani kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

Huu ni mtizamo wangun
 
Back
Top Bottom