Rais Samia: Dar kuna Watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi ujambazi na uporaji vimeanza kuja juu

Nigrastratatract

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
865
1,000
“Leo nimesoma mtandaoni, Dar es salaam kuna Watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi ujambazi na uporaji vimeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP upo hapa, mitandaoni wanamtaja Afande mmoja alikomesha ujambazi, wanasema ‘Mama turudishie’, IGP kaliangalie hilo vizuri” - Rais Samia Suluhu wakati akizungumza na Wazee Dar es salaam leo
 

mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
567
1,000
Swala la usalama wa raia na mali zao ni swala la National security ambalo kiongozi yeyote makini angekuwa ana taarifa sahihi na ameshalifanyia kazi sasa kama taarifa tu anazipata mtandaoni... haya anazungumzia askari ambae hata yeye hamjui ? duh tuendelee kula Mtori nyama zipo chini ila waimba mapambio hamuwezi kuona udhaifu mkubwa uliopo kwa sasa kwa vile nyimbo zinazopigwa na DJ mnazielewa .. badala ya kumwambia Dereva aangalie mbele aache kuwaangalia nyinyi mnamsifia kwa kuweza kuendesha gari huku hatazami barabara soon mtajikuta mpo mtaroni mmevunjika na wengine kuumia vibaya .
 

Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,581
2,000
“Leo nimesoma mtandaoni, Dar es salaam kuna Watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi ujambazi na uporaji vimeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP upo hapa, mitandaoni wanamtaja Afande mmoja alikomesha ujambazi, wanasema ‘Mama turudishie’, IGP kaliangalie hilo vizuri”———Rais Samia Suluhu wakati akizungumza na Wazee Dar es salaam leo
Wambea wa mitandaoni kama wewe bwana Musiba ndo majizi makuu, mkigombana huko lumumba ulivyo huna koromeo jitu zima hovyo unakuja kumwaga mitandaoni, hopeless kabisa ww
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,608
2,000
Mitandaoni ndio bunge halali la wananchi, wale majizi wa kura kule bungeni mama anajua wanajadili tu kuifurahisha serikali ila hawana jipya, wala mvuto. Sasa kama wale majizi wa kura hawana hata maswali kwa waziri Mkuu, hapo unategemea huyo mama aache kuja mitandaoni kwenye Nondo za ukweli?
 

Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,096
2,000
Anafanya kazi nzuri kusoma mitandao anapata first hand information...Mh. Rais yupo exposed she is a good blend of old age and modern generation kwakua all throughout she has been working at different levels with people from almost all walks of life...Kongole kwake kwakua msomaji mzuri wa mitandao ndiyo njia pekee yaku triangulate informationa anazopelekwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom