Rais Samia chonde chonde rudi tena Bandari, kuna wajanja wanaanza kuku-beep

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,159
27,194
Mama Samia popote ulipo nakuomba uangalie tena Bandari Kuna Jambo halipo sawa huko.

Kuna C&F companies wameanza kulalamikia delays na hii ni kutokana na mfumo wa kisasa wa kufatilia mizigo na ulipwaji Kodi electronically kuharibika takribani wiki sasa na hivyo kurudi kwenye mfumo wa zamani.

Mfumo wa kisasa ni mzuri na unapaswa kuwe na back-up, kitendo cha kusema umeharibika inabidi utumike wa zamani kunaweza kuandamana na hujuma ili watu wafanye yao.

Tunajua wabongo tulivyo wajanja, hapo inaweza kuwa loop-hole na usishangae ukakaa hata miezi bila kurudishwa.

Mama Samia nakukubali sana, naamini Hilo pia haliwezi kukushinda.

#kazi iendelee#

Screenshot_20210411-214804_1.jpg
 
Hatuhitaji uongozi wa "one man show" tumeshajifunza vya kutosha. Hatuhitaji mtu mmoja atatue kero zetu. Tunahitaji sheria madhubuti ndiyo ziendeshe nchi.

Sheria ziboreshwe lakini pia maslahi ya watumishi yaboreshwe ili kuleta usawa. Mtumishi anaitumikia serikali zaidi ya miaka 30 lakini kajumba ka chumba na sebule anakajenga kwa shida sana, hiyo sio sawa.
 
Hii ni moja ya madhara ya kugeuza vyombo nyeti vya serikali kuwa mawakala wa CCM kushughulikia wapinzani. Wanakosa brain, wanakosa intelligence.

Huwa najiuliza inakuwaje sehemu zote hizi ambazo ni nyeti na watu wa TISS wanakuwa wapo, unakuta mambo yanaanza hadi kuharibika bila detection yoyote?
 
Hatuhitaji uongozi wa "one man show" tumeshajifunza vya kutosha. Hatuhitaji mtu mmoja atatue kero zetu. Tunahitaji sheria madhubuti ndiyo ziendeshe nchi...
Hizo Sheria madhubuti zipo, ila hakuna anayefuata. Sheria zipo wazi kabisa kuhusu kuhujumu au kuiba Mali ya umma Ila hakuna anayejali. Hivyo Sheria ni lazima awepo wa ku-enforce, bila hivyo ni kazi bure tu zitaishia kuandikwa kwenye mavitabu
 
Hii nchi inahitaji ngumu sana ikiwezekana hata mtu akitakatisha fedha za serikali basi hata anyongwe. Hapo unakuta huo mfumo umeharibiwa kimakusudi tu ili wafanye yao
Kuna haki za binadamu, hawatakubali hizo sheria
 
Mataga siku zote mmekuwa mnashauri na kuibua mambo ya msingi kama haya hakika tungefika mbali, ushauri mzuri.

Swali ni je hivi anayeweza kushughulikia bandari ni Rais pekee, Maafisa usalama, maaskari na wale mapolisi kazi zao ninini kule?
 
Hizo Sheria madhubuti zipo, ila hakuna anayefuata. Sheria zipo wazi kabisa kuhusu kuhujumu au kuiba Mali ya umma Ila hakuna anayejali. Hivyo Sheria ni lazima awepo wa ku-enforce, bila hivyo ni kazi bure tu zitaishia kuandikwa kwenye mavitabu
Yaani mtu anaiba bilioni 5 anaenda kufungwa mwaka mmoja akimaliza kifungo anarudi mtaani kuzitumia pesa alizoiba.

Hizo ni sheria au takataka?
 
Back
Top Bottom