Kwanza kabisa nampa Hongera sana kwa Mungu kumpa Umri mrefu, hakika kwa umri wake wa miaka 96 ni upendeleo wa hali ya juu, lkn pia nampa hongera sana kwa kuzindua kitabu chake ambacho kimejaa Mikasa, Fitina, Majungu lkn pia na Uvumilivu.

Sisi wajukuu zako hatukufahamu kabisa juu ya Uongozi wako ulikuwaje/ulitawalaje, ulikumbana na changamoto gani,
lkn kupitia kitabu chako, nimesikiliza tu muhtasari ulio somwa na Prof. Makandala hakika umenifanya nitafakari mambo mengi sana.

Kumbe tabasamu la mzee wetu Mwinyi lilificha maumivu mengi moyoni mwake, kumbe alipitia misuko suko migumu kiasi hicho dah! na bado akawa anatabasamu na kuendelea kuchapa kazi!!

Hakika mzee Mwinyi anastahili Tuzo ya Heshima kuliko gari.

Swali moja nililo jiuliza, ambalo pia na watanzania wenzangu naomba mjiulize au mtafakari;

Ni je, sisi kama watanzania tunajifunza nini?
viongozi mliopo madarakani ktk idara mbali mbali za serikali mnajifunza nini?

Je, nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kama ilivyo kuwa ktk kipindi cha mzee Ruksa?

Mzee Ruksa nakupa Hongera na Pole, hakika ktk safari yako ya uongozi ulipitia matamu na machungu mengi.

Nitanunua kitabu ili nisome zaidi.
 
Kutokana na yaliyo andikwa kwenye Kitabu chake Mzee Mwinhi, inaomekana katika Marais walio pata taabu sana ktk uongozi kuanzia alipo teuliwa kuwa waziri basi ni Huyu Mzee wetu Mwinyi.

Pamoja na kuwa mwadilifu na mtiifu lkn bado alichukiwa sana na alifanyiwa fitina za hali ya juu mpaka akajiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani lkn badae alirudishwa tena ulingoni lkn bado alipigwa fitina na kubabaishwa kuwa eti ni mdini anapendelea waislamu n.k, ama hakika walimyumbisha sana lkn kutokana na uadilifu wake na ucha Mungu alibakia kuwa Imara na Hatimaye Mungu alimsaidia.

Hakika kuna mafunzo mengi sana ya kujifunza ktk kipindi cha utawala wake.

tujirekebishe kwa wale wote wenye chuki binafsi na uchu wa vyeo, tuache tabia za kuiguruga nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli.

tuache kutafuta vyeo kwa uchawi au kwa kuhadaa/unafiki kwani cheo/uongozi hutoka kwa Mungu.

Tusibaguane wala kuchukiana au kufanyiana fitina kisa ni mkristo au mwislamu, sisi sote walio na dini na wasio na dini tunaunganishwa na MAMA Tanzania.

tusibaguane kwa makabila au ukanda kwani sisi sote ni watanzania, hivyo yatupasa kudumisha Amani, Upendo na Utulivu kwa masilahi ya nchi yetu.
 
Kwanza kabisa nampa Hongera sana kwa Mungu kumpa Umri mrefu, hakika kwa umri wake wa miaka 96 ni upendeleo wa hali ya juu, lkn pia nampa hongera sana kwa kuzindua kitabu chake ambacho kimejaa Mikasa, Fitina, Majungu lkn pia na Uvumilivu.

Sisi wajukuu zako hatukufahamu kabisa juu ya Uongozi wako ulikuwaje/ulitawalaje, ulikumbana na changamoto gani,
lkn kupitia kitabu chako, nimesikiliza tu muhtasari ulio somwa na prof. Makandala hakika umenifanya nitafakari mambo mengi sana.

Kumbe tabasamu la mzee wetu Mwinyi lilificha maumivu mengi moyoni mwake, kumbe alipitia misuko suko migumu kiasi hicho dah! na bado akawa anatabasamu na kuendelea kuchapa kazi!!

Hakika mzee Mwinyi anastahili Tuzo ya Heshima kuliko gari.

swali moja nililo jiuliza, ambalo pia na watanzania wenzangu naomba mjiulize au mtafakari;

ni je, sisi kama watanzania tunajifunza nini?
viongozi mliopo madarakani ktk idara mbali mbali za serikali mnajifunza nini?

Je, nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kama ilivyo kuwa ktk kipindi cha mzee Ruksa?
Mzee Ruksa nakupa Hongera na Pole, hakika ktk safari yako ya uongozi ulipitia matamu na machungu mengi.

Nitanunua kitabu ili nisome zaidi.
Kwa kweli zawadi ya gari haikufaa. Sijui waliwaza nini ?!. Mtu kama Mwinyi na uzee wote huo gari la nini ?! Kwanza kila wakati anabadilishiwa magari na serikali
 
Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania...

Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako...

Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake...Rais Samia
Hapa ndio naanza kuamini ule msemo mwenye nacho huongezewa ili awe na kingi zaidi
 
Yajayo yanafurahisha ...wastaafu wote wanapewa magari haya ngoja tusubr Bday ya JK sijui na yeye anapewa nini
Jk atapewa Ferrari, kwakuwa bado ni
HB na alivyo bishoo,itamfaa Sana

But ukiwa mzee tabu tupu ,yaani sura ya mzee Mwinyi inachekesha sana
 
Bora angetumia diplomasia ili kutosababisha taharuki kwa jamii, angempa tu kimyakimya
 
Msisah
Magu aliwapa nyumba zenye thamani zaidi ya hyo benzi
Kweli ukiwa nacho unaongezewa

Ova
Msisahau huyo ni raisi mstaafu aliyeitumikia nchi hii, kupewa gari kama zawadi na raisi aliyekuwepo madarakani kama zawadi yake ya birthday it's not a big deal.
 
Kama kweli mmeahirisha Mechi ya Simba na Yanga kwa sababu ya bethidei ya Mwinyi mmekosea sana.

Aliyetoa wazi la kuahirisha Mechi asakwe halafu alazimishwe kuwajibika.

Kwa hiyo ikifika tarehe kama ya Jana mwaka kesho mtampa zawadi nyingine tena yenye thamani kama hii?

Haya basi pamoja na uzembe huu, kwanini msingesubiri hadi akatimiza miaka 100 angalau ingeleta mantiki kidogo na kigezo cha kulifanya jambo Hilo kuwa la kitaifa.

Kwanza ifahamike kuwa bethidei ni suala la mtu binafsi na familia yake,kutushirikisha sisi na kutuondolea Mechi muhimu kabisa Ni kosa kisheria.

Soka na mambo ya kisiasa ni mwiko kwa mujibu wa FIFA.

Ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Magufuli aliwajengea nyumbazenye thamani ya sh 500M kwa kula mmoja wakati wana nyumba zaidi ya tatu kula mmoja na hawajakosa pa kulala.

Nyie mmemnunulia gari la sh 450 M.

Kuna shule ngapi hazina madarasa na madawati?

Wafanyakazi wa chini kabisa Wastaafu wengine mpaka Leo hawajalipwa mafao yao.

Kuna hospitali hazina vifaa tiba.

Kuna barabara za Mitaani hazipitiki kipindi Cha mvua, mmeshindwa kuweka lami.

Nyinyi watu mtatuvusha kweli?

Mbona vipaumbele vyenu sio vya maana?

Mnazungua bana.
 
Alafu Bethidei ni Mambo ya juwaiga mabeberu,alisikija Ndugu Kabudi akiongea.

Pia ni matumizi mabaya ya chombo Cha Taifa Kama TBC.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom