Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 581
- 574
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo 10 Oktoba 2021.
Fuatilia matangazo hapa
Dondoo ujio wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka IMF.
1. Kujenga madarasa mapya 15,000 ya sekondari.
2. Kujenga madarasa 3,000 shule za msingi shikizi
3. Kutengeneza madawati 462,795
4. Kumalizia vyuo vya VETA 32
5. Magari 25 ya kuchimba visima vya maji.
6. Mitambo 5 ya kujenga mabwawa ya maji.
7. Kujenga ICU 72
8. Magari ya wagongwa (Ambulance) 395 na ya chanjo 214
9. Mifumo ya Oxygen hospitali 82
10. Mitungi ya gesi 4,640
11. Mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni 40.
12. Vitanda vya wagonjwa 2,700
13. Xray za kisasa 85
14. CT- Scan 29
15. MRI hospitali zote za kanda
Rais Samia Suluhu Hassan
Kwenye kipindi cha miezi sita tumeweza kutatua changamoto 11 za Muungano ikiwemo masuala ya usimamizi wa ukokotoaji na ukusanyaji wa kodi za huduma za simu unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar, Sheria ya Uvuvi kwenye ukanda wa uchumi wa bahari kuu pamoja na suala la ucheleweshaji wa mikataba mbalimbali ya miradi ya maendeleo
Hakuna shaka kutatuliwa changamoto hizo kumeimarisha muungano wetu.
Kwenye hotuba yangu tarehe 22 Aprili nilitaja baadhi ya hatua tulizopanga kuzichukua ili kukuza uchumi ikiwemo kuhakukisha viashiria vyote vya uchumi jumla vinabaki kuwa imara. Kutathmini mifumo, taratibu na viwango vya kodi, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Nfarijika kuwa katika miezi 6 iliyopita, tumetekeleza hayo yote.
Uchumi umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.3 ukilinganisha na asilimia 4 kipindi kama hicho mwaka uliopita
Tumedhibiti mfumuko wa bei ambapo umeendelea kuwa na tarakimu moja. Katika kipindi cha mnwezi Aprili hadi Septemba 2021 mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 4. Hadi mwezi Agosti 2021 akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 5.8 iliyotoshelea kuagiza bidhaa kwa kipindi cha miezi 6 ikilinganishwa na akiba ya dola za Marekani bilioni 4.9 iliyokuwa kipindi kilichopita.
Hali ya ukusanyaji wa mapato inakwenda vyema. Kuanzia Aprili mpaka Septemba tumakusanya trilioni 9, bilioni 905, na mapato yasiyokuwa ya kodi yalikuwa Tshs. Trilioni 1 bilioni 436
Tumrefanikiwa kupata mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Tsh. Trilioni 1 bilioni 447.
Katika kipindi hicho tumetuliza kilio cha muda mrefu cha kufanya marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani, yaani VAT Refund. Kiasi cha bilioni 451 na milioni 300.
Tumeendelea kulipa madeni ya ndani na je. Tumeweza kumaliza uhakiki wa madeni ya ndani yanayofikia shilingi bilioni 439 yanayotokana na madai ya watumishi, wazabuni wakubwa na wadogo, wakandarasi wakubwa, madeni ya huduma za umeme maji na simu kwa taasisi za umma
Madeni yote hayo yameanza kulipwa na yanaendelea kulipwa. Kazi ya uhakiki wa madeni yaliyobaki inaendelea.
Kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara, hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo ikiwemo kuondoa urasimu kwenye utoaji wa vibali vya kazi ambapo tumeanzi mfumo wa kielektroniki, yaani e-permit. Mfumo huu umepunguza siku za utoaji vibali kutoka siku 14 hadi siku moja kwa sasa endapo mwombaji atakuwa amekamilisha taratibu zote.
Katika Miezi 6 iliyopita tumeshughulikia maslahi ya Wafanyakazi kwa kuwaajiri wapya, kuwapandisha madaraja na kubadili kada
Pia tumewapa unafuu kwa kupunguza Kodi ya Mapato(PAYE). Tumetenga Tsh. Bilioni 20 zinazoenda kuongeza nguvu kwenye TASAF
Tumeanza mradi wa kushughulikia matatizo ya Machinga, mradi huu utaenda kujenga masoko kwa ajili yao
Pori la akiba la Selou limebaki chini ya mfumo wa Urith wa Dunia ambapo linaendelea kufaidika na misaada ya mfuko huo
Kuanzia Mwezi Desemba 2021 Wasanii wataanza kupokea mirabaha kutokana na kazi zao
Sanaa imeajiri Vijana wengi Nchini na kusaidia kukua kwa uchumi
Sitaki utitiri wa kamati. Ili kuwa na uwajibikaji ziundwe kamati za kimkoa ambazo zitashughulika na mradi huu wa maendeleo kwa Wananchi
Kwa wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi, wajaribu kudokoa pesa hizi au wabadilishe matumizi
Kwenye fedha hii ya miradi ya maendeleo ya Taifa sitakuwa na huruma na Mtu
Kuanzia kwa Mawaziri wangu hadi chini kwa Wananchi. Kwa hiyo mkasimamie miradi kwa uadilifu
Natoa wito kwa Wananchi na Watumishi wa Umma mkiona kuna shida katika mpango huu wa maendeleo, mtoe taarifa ili tuweze kuchunguza na kuchukua hatua