BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Rais Samia awezesha ndege mpya ya mizigo kutua Aprili.
Na Bwanku Bwanku.
Ndege mpya ya mizigo iliyoagizwa na Serikali ya Tanzania kutoka nchini Marekani inatarajiwa kupokewa nchini mwezi Aprili mwaka huu ili ianze mara moja kuendelea kufungua uchumi wa Taifa kupitia usafarishaji wa mizigo kutoka Nje ya Nchi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa ATCL, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema huu ni mwendelezo wa Serikali kuweka mazingira mazuri ya usafirishaji wa mizigo na kuwarahishia Wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao hasa kwa kuzingatia kwasasa usafirishaji wa mizigo unafanyika kwa kutumia ndege za abiria.
Mchechu amesema ndege hiyo aina ya Boeing 767-300F ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mpigo wa mara moja na kutatua changamoto kubwa ya usafirishaji mizigo kwa Wafanyabiashara nchini ambao mara nyingine wamekuwa wakipata shida sana kusafirisha mizigo kutoka nje.
"Tuishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa uwekezaji huu mkubwa unaozidi kufanyika kwenye Shirika la ndege la Tanzania kwa kuleta ndege ya mizigo kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Chama kinachoongoza Taifa (CCM) na kwenye Mipango ya Nchi pamoja na ndege nyingine mpya ambazo inajiandaa kuleta. Uwekezaji huu unaifanya ATCL kuwa Shirika kubwa la ndege nchini na Afrika Mashariki na kuendelea kulikuza zaidi ukanda mzima wa Kusini kwa Afrika (SADC)." Alisema Mchechu.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi amesema ndege hii ni kubwa na ya kisasa sana na kwa kuanzia kwa kipindi cha miezi miwili hadi sita wataanza kwenda kwenye nchi ambazo wamejijenga sana kwenye masoko ikiwemo China, India pamoja na kwenye nchi ambazo zimekuwa zikitumia sana bandari ya Dar es Salaam kupakua mizigo yao kama Congo, Zimbabwe, Comoro na kadhalika huku wakijipanga kwenda nchi zingine zilizojijenga kimasoko hivi karibuni kama Dubai.