Rais Samia awekeze kwenye utawala wa sheria, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
940
1,000
La muhimu ni kwa Rais Samia kwa hii miaka minne, au mitatu, aipatie Tanzania katiba mpya. Asijikweze sana kutaka kugombea hapo 2025, hilo si lake. Awaachie wenyewe.

Zaidi ajikite kwenye kuwekeza utawala wa sheria, Katiba mpya na tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, mambo matatu hayo yatamuweka kwenye chati milele na kuandikwa kwenye Historia kama itakavyoandikwa kuwa ni Rais wa kwanza Mwanamke kwa East Afrika Afrika ya kati mpaka kusini huko na pia Mwenyekiti wa CCM.

Nchi inahitaji Katiba mpya, Utawala wa sheria na Tume huru ya Uchaguzi.

Namsihi awachane kabisa na mambo ya kutaka kuendelea kugombea 2025. Asikubali kutomezwa!
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,470
2,000
Wenyewe akina nani?. Jana akikabidhiwa kofia ya uraisi wa chama alisema hilo tukio hakika lina dhihirisha kuwa ccm ina wenyewe.
 

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,028
2,000
Huyu mama alikua kiti cha mbele kwenye mchakato wa katiba mpya. Hivi kwa akili yako ataacha kweli ku revisit ule mchakato??!! Big no hawezi Acha nguvu zake zipotee Kwanza huyu ni Muislam wa wastani flani hua hajikwezi. I don't mean waislam hawajikwezi lkn wale wenye chembe chembe za kuijua dini hua sio wababe sana kama sijui kina Nani if you know what I mean.

so suala la katiba usitie Shaka litakuja tu. At the moment she is putting her efforts in house cleaning, you know how good ladies are at it.
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,470
2,000
Afu tunampa mitano tena, stake asitake.

Nchi hatuwapi tena mazwazwa. Tumejifunza kutokana na makosa tuliyofanya 2015 mpaka Mungu alipoamua kuturekebishia makosa yetu
Kwamba mazwazwa
Washamba
Waliotaka kuendesha nchi kama wanaswaga ng'ombe
Wasioshaurika
Wenye viburi na maneno ya kujivuna
😎

Mungu akabonyeza kibatani cha execute na habari ikaishia ile tarehe 17.
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
62,971
2,000
Kwamba mazwazwa
Washamba
Waliotaka kuendesha nchi kama wanaswaga ng'ombe
Wasioshaurika
Wenye viburi na maneno ya kujivuna
😎

Mungu akabonyeza kibatani cha execute na habari ikaishia ile tarehe 17.
Hiyo tarehe 17 wameamua tu kusema wao. Mungu alishatenda miujiza wiki moja kabla. Mazwazwa wakamficha wakidhani angefufuka... si unajua mtu yule alishawapiga fix yeye ni kiongozi wa malaika?
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,407
2,000
Afu tunampa mitano tena, atake asitake.

Nchi hatuwapi tena mazwazwa. Tumejifunza kutokana na makosa tuliyofanya 2015 mpaka Mungu alipoamua kuturekebishia makosa yetu
Kwa hiyo Mungu sneamua kutukomboa bila vita?
 

Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
792
1,000
Afanye hayo yote na aendelee kuaysimamia 2025-2030 Mungu akipenda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom