Rais Samia aweka rekodi ya kuwajali wamachinga tangu nchi ipate Uhuru

Tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961, Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia suluhu Hassan ameweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza kuwafanyia jambo kubwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga kwa kuwapa donge nono la Pesa la Shilingi Bilioni 5 kwa ajili yao tu.

Serikali nyingi zilizopita zilikua zikiwapangia tu maeneo ya kwenda kufanya biashara zao, bila kutoa kiasi chochote cha fedha ili kuwawezesha Wamachinga huko wanapoenda kwenye maeneo yao mapya watatue changmoto watakazokutana nazo.

Akizungumzia hatua hiyo Makamu Mwenyekiti Wamachinga Taifa Steven Lusinde amesema Rais Samia kwao amekuja kama Nabii aliyeletwa na Mungu kuboresha maisha yao na muda si mrefu watakuwa matajiri.

"Kiukweli ndugu waandishi sisi wenyewe mara ya kwanza kuona kwenye Akaunti yetu imeingia Bilioni 5 kwa ajili ya Wamachinga tu hatukuamini, kimsingi tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia na tunamuahidi kumuunga mkono mpaka mwisho wa uongozi wake." Amesema Lusinde

Aidha Kiongozi huyo amesema Wamachinga wote nchini wameitikia vizuri wito wa Serikali wa kuhama kwa hiari, na hivi karibuni watakua wameshahamia kwenye maeneo waliyopangiwa.

#SisiTumekubali
#KaziIendeleee
Kaziiendelee
 
Back
Top Bottom