beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na ujenzi miundombinu ya utoaji Haki, mafanikio yanayotarajiwa hayawezi kupatikana endapo wadau wa mfumo huo hawatofanya kazi kwa kuzingatia Sheria.
Ameeleza, "Tunaweza kuwa na majengo mazuri na mfumo bora wa TEHAMA, lakini kama Mahakimu, Majaji na wengine hawakuongozwa na nafsi njema katika Utoaji Haki, inaweza isipatikane"
Amesema hayo leo Oktoba 06, 2021 katika Uzinduzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki Jijini Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Mahakama kushughulikia uchelewaji wa kesi, akitaka suala la kusikiliza kesi haraka kupewa kipaumbele
Amesema, "Msikubali kirahisi kubadilisha Mahakimu au tarehe za kusikiliza kwasababu hilo ni moja ambalo linafanya kesi zichelewe"
Pia amewataka Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kuangalia usimamizi wa ubora wa maamuzi katika Mahakama za Mwanzo, akisema malalamiko mengi yanahusu Mahakama hizo