Rais Samia awashangaa wanaosema miradi ya Magufuli haitoendelezwa, adai uwezo wao wa kufikiri ni mdogo

Nape hakusema huo mradi usimame!

Alitaka garama zake ziwekwe wazi!

Machadema ndio yakawa yanasema miradi isimame maana haina faida

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kwavile alisemea bungeni ushahidi uko kwenye Hansard hakuna haja ya kubishana!

Aliyosema ichinguzwe ni mikopo aliyokopa Magufuli!!
 
Kwavile alisemea bungeni ushahidi uko kwenye Hansard hakuna haja ya kubishana!

Aliyosema ichinguzwe ni mikopo aliyokopa Magufuli!!
Hakuna mahala popote Nape alisema hiyo miradi isimamishwe,

Kama alisema niambie alisema sababu ya kutaka hiyo miradi iachwe ni nini?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hivi Ina maana HUYU mama alikuwa hajui kuwa mwana ccm ubongo unaporomoka ,na mwaka huu mkutano mkuu wa chama Cha mazezeta mmeamua uwe kwenye sikukuu yenu tarehe 1/4/2022
 
Tanzania imepita marais 5 ila yenyewe ipo na itaendelea kuwepo baada ya mh.Rais Samia na watakaomfuatia.....

Twende na mh.Rais SSH kwa ujenzi wa Tanzania bora!!!!

#Siempre JMT
Yeye si ana mkataba na Mungu! Sawa
 
Kwenye Mazuri utamsikia Rais akisema "Nae alikuwa sehemu ya Awamu ya Tano"

Kwenye Magumu utasikia akisema "Tunafungua nchi" Atuambia kwanza kwa nini aliifunga.
Kwanini alisaidia kuifunga nchi.
Kwanini alisaidia kuua uchumi anaodai kuusimamisha.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli haitaendelezwa, hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo, zilizojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016.

“Kulikuwa na maneno mengi, iliyoachwa haitaendelezwa ukiuliza sababu hakuna. Hakukuwa na sababu ya kwamba miradi hiyo isiendelezwe, kwani ilianzishwa na kuagizwa ndani ya Ilani ya CCM. Sasa kwa kunitazama sura na kusema isingeweza kutekelezeka miradi nadhani hekima haikutumika.

“Wanaposema miradi haitaendelezwa nadhani upeo wao wa kufikiria ni mdogo sana. Hata miradi hii ilivyoanzishwa nilikuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo ni sehemu tangu kuanza kwake na kutekelezwa,” amesema Rais Samia wakati akizindua mradi wa nyumba 644 za Magomeni Kota.

Hata hivyo, Rais Samia akiwahutubia wakazi wa Magomeni na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam amesema “lakini tuwaombe nasi tujiombee kwa Mungu atupe nguvu, uwezo na hekima zaidi ili tuweze kuendeleza miradi kwa maendeleo ya Taifa.
Kwani si ni hiki hiki chama cha wezi ndiyo kimeshika dola toka tumepata uhuru mwaka 1961? Tatizo la CCM ni kutokuwa na viongozi wanao ona mbali, hawako hapa kuliongoza hili taifa zaidi ya wizi na kulindiana maslahi tu na hawanaga haibu kujiumbua. Juzi tu hapa Kikwete katoa sifa lukuki kwa Mama Samia kutatua tatizo la maji Chalinze kwa kipindi cha mwaka mmoja tu toka aingie madarakani. Kumbukeni, yeye Kikwete alikaa madarakani miaka 10 hajafanya chochote. Kuongozwa na CCM kwa kweli ni kurudishwa nyuma kimaendeleo, mtu aliyetufaa hapa nchini alikuwa Magufuli tu.
 
Mama SSH ni vyema akawa haingii sana ktk malumbano na wanasiasa badala yake atende kazi kama raisi.
Mipasho inaweza kumuondoa ktk 'reli' kama ambavyo imeanza kuonekana.
 
Kila siku kuongea yale yale tu, inamaana hana sera, kuna watu anashindana nao au?

2025 ije haraka tu tupate Rais mwingine huyu hapana kwakweli
1648101713301.png
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli haitaendelezwa, hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo, zilizojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016.

“Kulikuwa na maneno mengi, iliyoachwa haitaendelezwa ukiuliza sababu hakuna. Hakukuwa na sababu ya kwamba miradi hiyo isiendelezwe, kwani ilianzishwa na kuagizwa ndani ya Ilani ya CCM. Sasa kwa kunitazama sura na kusema isingeweza kutekelezeka miradi nadhani hekima haikutumika.

“Wanaposema miradi haitaendelezwa nadhani upeo wao wa kufikiria ni mdogo sana. Hata miradi hii ilivyoanzishwa nilikuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo ni sehemu tangu kuanza kwake na kutekelezwa,” amesema Rais Samia wakati akizindua mradi wa nyumba 644 za Magomeni Kota.

Hata hivyo, Rais Samia akiwahutubia wakazi wa Magomeni na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam amesema “lakini tuwaombe nasi tujiombee kwa Mungu atupe nguvu, uwezo na hekima zaidi ili tuweze kuendeleza miradi kwa maendeleo ya Taifa.
1. Huo mradi uwe ni kichocheo cha kujenga makazi bora mengine nchini ili kupunguza tatizo la makazi bora kwa wafanyakazi, watumishi na wananchi wa kawaida.

2. Miradi mikubwa ya kimkakati likiwemo bwawa la Nyerere ikamilike kabla ya uchaguzi wa 2025.

Raisi Samia amefanya kazi na hayati Magufuli hivyo hana nafasi ya kutoa mipacho majukwaani, apige kazi kuonyesha yeye ni mwendelezo wa "Hapa Kazi Tu".

"Hapa Kazi Tu" ni msemo ambao ambao umewekwa hadi kwenye ndege zetu za ATCL kutambulisha Tanzania kuwa ni nchi ya wachapa kazi na ipo katika safari ya kujikomboa kiuchumi.

Raisi Samia atambue kuwa kulipa kodi ni hiari lakini ni lazima, ili kupata fedha za kuijenga nchi khasa katika suala la miundombinu muhimu barabara, maji, na umeme.

Hivyo serikali yake ihimize kulipa KODI ya maendeleo ambayo ndio njia pakee ya kupata mapato na kupunguza utegemezi wa fedha za mikopo.

Nakazia, raisi Samia aachane na mipasho majukwaani, "Talk Less Do More".
 
Nataka kujikita kwenye kazi anayoifanya, ila yeye mwenyewe ana distract watu wasijikite kwenye kazi anayoifanya.

Tatizo ni lake, si langu.

Angefanya kazi na ku stick on the message, ningejikita kwenye kazi.

Huu ndiyo utamaduni wa siasa za Tanzania au siasa period?

Mtu kashapewa urais, sasa anajibizana na nani?

Rais kazi yake ni kuunganisha wananchi. Atuambie wananchi "serikali inapenda watu muwe na makazi bora, tumejenga nyumba".

Hizi habari za "walisema hatuwezi, tumeweza" kwanza zinagawanya watu. Hili jambo baya.

Pili, zinaonesha inferiority complex.

Ni kama vile rais hajiamini.

Anajiona kama mtoto mdogo aliyeweza kusimama, sasa anapiga kelele kila mtu wa karibu yake amuone kasimama.

"Mama, Baba, achimama, achimama"

Halafu watu wamuimbie wimbo.

"Kasimama peeke yake, kaonesha ubingwa wakeee".

This is basically what President Hassan is doing.

Just do the work please. Taifa lishagawanyika sana miaka ya Magufuli, wewe unatakiwa kuliunganisha, si kuligawa zaidi.
Bora taifa liendelee kujigawa. Mimi sitaki kuungana na watu wa Jiwe. Ni watu hatari sana, akili zao ni ndogo kabisa. Nikiungana nao watachukua akili zangu, nitakuwa mjinga, roho mbaya na muuwaji kama wao. Nasema tuendeleze huu mpaka.
 
Back
Top Bottom