Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter ametuma salamu za pongezi kwa Wakenya katika uchaguzi Mkuuu uliomalizika kwa William Ruto kushinda nafasi ya Urais.

Katika ujumbe wake Rais Samia amewapongeza Wakenya kwa kufanya uchaguzi kwa amani na ameeleza matazamio yake ya nchi za Kenya na Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu
Screenshot 2022-08-16 at 08.05.10.png
 
Mbona hataki kumpongeza Ruto direct anafikiri ngoma itapinduka au kisa yeye na uhuru wanaoneana so. Ajitahidi kujifunza Kuna kukosa ktk maisha
 
RAIS SAMIA AWAPONGEZA WAKENYA

Rais Samia Hassan Suluhu amewapongeza Wakenya kwa uchaguzi wa amani na utulivu

"Ninapenda kuwapongeza kwa dhati wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi wao mkuu kwa amani na utulivu, ambapo matokeo yake ni Dkt William Ruto kutangazwa kuwa Rais mteule wa Kenya.

“Tanzania itaendeleza undugu na ushirikiano wa Kihistoria na Kenya uliodumu miaka na mikaka," – Rais Samia.

1660634023737.png
 
Chadema wangesema hajui kiingereza.
Kwani anajua kiingereza Sasa? Mbona hajui.

Hata kwenye Royal Tour ambako alilazimika kurudia scene moja mara 10 lkn bado akawa anaitikia "Yaah" hata kwa mambo yasiyostahili.

Piraa: Your predecessor was stupid ?
Mama: Yaah!

Piraa: I think me and you will make a good couple!

Mama; Yaah.

Piraa: You were not in good terms with your predecessor?

Mama: Yaah.
 
Nilimsikia Chebukati anasema huu ndo uchaguzi wake wa mwisho, ingekuwa poa tungemwomba aje hapa bongolala apambane na wazee wa mabegi meusi.
 
Kwani anajua kiingereza Sasa? Mbona hajui.

Hata kwenye Royal Tour ambako alilazimika kurudia scene moja mara 10 lkn bado akawa anaitikia "Yaah" hata kwa mambo yasiyostahili.

Piraa: Your predecessor was stupid ?
Mama: Yaah!
Piraa: I think me and you will make a good couple!
Mama; Yaah.
Piraa: You were not in good terms with your predecessor?
Mama: Yaah.
Wewe unge penda ajibu je? Mbona nyie mnapenda kumdhoifisha Raisi, leteni hoja za mashiko kuliko mambo ya kike kike
 
Nilimsikia Chebukati anasema huu ndo uchaguzi wake wa mwisho, ingekuwa poa tungemwomba aje hapa bongolala apambane na wazee wa mabegi meusi.
Huku atatekwa na kupotezwa kama Ben Sa8 kabla hajaanza kazi
 
Kwahiyo umewahi Kumpongeza ili usionekane kuwa hukumtaka au Tanzania tulikuwa hatuna upande wowote kati yake na Odinga?

Nilidhani baada ya kusikia kuwa upande wa Odinga umeyakataa Matokeo na wamekata Rufaa basi Washauri wako hasa Rais Mstaafu Kikwete wangekushauri uwe Mvumilivu Kwanza mpaka Supreme Court ya Kenya itakapoamua.

Kwa nilivyofuatilia huu Uchaguzi Mkuu wa Kenya sina shaka kuwa Kidhati William Ruto ameshinda kwani alijipanga vyema na anakubalika na Kundi Kubwa la Vijana ila kwa Kuheshimu Sheria na Utaratibu wake Rais Samia angesubiri hadi Maamuzi ya Kisheria yatoke ndipo ampongeze kwa Uhuru zaidi kuliko sasa na nawaza je, ikitokea Mahakama ikaamua vinginevyo itakuwaje?
 
20220816_100601.jpg


Kwani aliwaambia hataki kumpongeza? Mbona mnawashwa washwa?

Tanzania haikuchukua upande waziwazi japo ingetamani Rau ashinde lakini waamuzi ni Kenyaland wenyewe.👇
 
Back
Top Bottom