Rais Samia awaonya Viongozi wanaotumia ubabe migodini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Wilaya, Wabunge na Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano mzuri kwa Wananchi badala ya kufanya ubabe Migodini.

Amesema, "Wabunge ambao maeneo yenu miradi hii ipo, iwasaidie kujenga Maendeleo na nchi sio iwajenge ninyi binafsi. Kuna ile kwenda na kutisha kwenye migodi. Tutafuatilia, faida irudi kwa Wananchi"

Ameeleza, "Suala la kurejesha fadhila kwa Wananchi nalo sio suala la hiari kwasababu mali ile imeumbwa pale walipo. Ni mali yao, ni mali ya Serikali. Kama tunaenda kuichukua, lazima turudishe faida kwao, sio twende kuchota tuwaache walivyo"
 
Hao wenyeji wangewezeshwa tu na vitendea kazi wangekuwa wawekezaji wenyewe,
Sema ndio hivyo tena madini yakikutwa shambani kwako ni mali ya serikali ila ikikutwa bange inabidi ueleze ilifikaje hapo
 
Back
Top Bottom