BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 325
- 414
Na Bwanku M Bwanku.
Leo Alhamisi Mei 04, 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ni mgeni rasmi na atafungua mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya 4 ambapo Mawaziri 14 kutoka Nchi za Comoro, Mauritius, Sudan, Somalia, Madagascar, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli, Eritrea, Sudan Kusini, Uganda na mwenyeji Tanzania watashiriki Jijini Arusha kwenye hoteli ya Glan Melia.
Kuelekea mkutano huo mkubwa utakaowakutanisha Mawaziri 14, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za kuwakaribisha Mawaziri hao kwenye mkutano huo mkubwa wa Kanda ambao ni mara ya kwanza unafanyika nchini Tanzania.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya michezo kwenye ukanda huo wa 4 wa michezo wa Umoja wa Afrika na namna ya kuboresha michezo zaidi.