Rais Samia awaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, yumo Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Mabalozi

Ningekuwa SSH ningeanza na baraza la mawaziri, hao watu wa mwendazake ndio 'magaidi' wake na sio Mbowe!
Muda ni mwalimu mzuri sana, atakuja kujutia hilo
 
Akimaliza hapo akapande ndege.
Yaani huyu Madam ni kupanda ndege na kuagwa na kupokelewa, kupanda ndege, kuagwa na kupokelewa 😂😂😂 inaonekana anapenda sana ndege huyu.

Huyu Madam hii kazi itamshinda very soon.
 
Hongera sana Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Elisante Gabrieli, hakika unalo jukumu la kuuboresha zaidi Muhimili huu wa Mahakama ambao ni muhimu kwa wananchi.
sisi wananchi tunataka kutendewa haki.
hakikisha watumishi wa mahakama wanapendana wao kwa wao, wapunguze majungu maana majungu yanapunguza ufanisi wa kazi. kwanza hakikisha haki inatendeka miongoni mwa watumishi wa Muhimili wa Mahakama kwa kufanya hivyo na sisi wananchi tutakuwa na imani kuwa tutatendewa haki. Haki lazima kwanza itawale kwenye Muhimili wenyewe hiyo itajenga imani kwa wananchi.
ondoa uonevu, haki itawale. usikubali kuhadaiwa na wachache, simamia weledi wako.
watumishi wa Mahakama badilikeni acheni kusemana semana na majungu maofisini, mmeaminwa kutenda haki acheni tabia zisizo faaa zinatukera sisi wananchi.
Mtendaji Mkuu Prof. Elisante atasafisha uozo wote, tabia za kinafiki, tabia za kujipendekeza kwa nia ya kupata upendeleo n.k safisha.
watumishi wa mahakama badilikeni.
 
Message was simple and clear. Kama vipi hamieni Burundi huko!

Mnadhani maendeleo yanashuka tu kutoka mbinguni???

Wewe linalokuuma ni Waislam kuteuliwa au Wazanzibari kupewa nafasi?? Likikuuma sana usisite kusema
Taratibu na uwe na adabu kidogo,usitutolee povu,huna uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kumpeleka Burundi,kila mtu anayo haki,uhuru wa kueleza hisia zake juu ya jambo flani au mtu flani,yeye ni nani asiongelewe? Kama nchi imeshamshinda tuache kusema,kipi anachokifanya sasa hivi cha maana zaida ya kupaa na ndege kila siku,Tuliza makagale na uache mihemuko!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Katiba pendekezwa iliyopunguza Madaraka ya Rais ililetwa wakati wa JK ikakataliwa, Wapinzani walitaka hadi Serikali 3 nayo iwemo

Subira yavuta kheri
Nimesikia kutoka Uganda Jana kuwa rais M7 kateua majaji wa mahakama kuu. Lakini hiyo haitoshi maana inabidi majina yao yapelekwe bungeni ili yaidhinishwe kama kweli wanafaa kulitumika taifa au kumtumikia aliyewateua, na huenda palikuwa na vetting kabla ya huo uteuzi.
Huko ni Uganda ambako tuliaminishwa miaka yote kwamba siasa zao sio nzuri na wana udikteta!
 
Hongera sana Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Elisante Gabrieli, hakika unalo jukumu la kuuboresha zaidi Muhimili huu wa Mahakama ambao ni muhimu kwa wananchi.
sisi wananchi tunataka kutendewa haki.
hakikisha watumishi wa mahakama wanapendana wao kwa wao, wapunguze majungu maana majungu yanapunguza ufanisi wa kazi. kwanza hakikisha haki inatendeka miongoni mwa watumishi wa Muhimili wa Mahakama kwa kufanya hivyo na sisi wananchi tutakuwa na imani kuwa tutatendewa haki. Haki lazima kwanza itawale kwenye Muhimili wenyewe hiyo itajenga imani kwa wananchi.
ondoa uonevu, haki itawale. usikubali kuhadaiwa na wachache, simamia weledi wako.
watumishi wa Mahakama badilikeni acheni kusemana semana na majungu maofisini, mmeaminwa kutenda haki acheni tabia zisizo faaa zinatukera sisi wananchi.
Mtendaji Mkuu Prof. Elisante atasafisha uozo wote, tabia za kinafiki, tabia za kujipendekeza kwa nia ya kupata upendeleo n.k safisha.
watumishi wa mahakama badilikeni.
 
Mama anapiga kazi kimya kimya bila hata Masifa na Nchi imetulia tuli.. Tumpe muda mambo yataenda tu.
 
Back
Top Bottom