Rais Samia avunja rekodi ununuzi wa ambulance na magari ya Chanjo

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,984
4,083

Maajabu ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Tanzania imeagiza Jumla ya ambulance mpya 395 na magari mapya 214 kwa ajili ya chanjo kwa mpigo kitu ambacho hakijawahi kufanyika tangu tuwe huru kama Taifa,​

===

Mtakumbuka awamu ya tano kwa miaka yote mitano tulifanikiwa kununua jumla ya ambulance 117,

Maajabu ni haya ya awamu hii ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwani tayari tumeagiza ambulance zingine brand new 395 na magari ya Chanjo 214 mapya,

Mambo haya yanafanywa na Rais anayethamini na kulinda Utu na Uhai wa Watanzania wote bila kujali dini, kabila, rangi wala kanda,

Rais Samia Suluhu kwa kutumia fedha ya kusisimua uchumi Economic Stimulus relief fund toka IMF,

Tayari ameagiza zinunuliwe Jumla ya Toyota Land cruiser ambulance mpya 395 pamoja na magari mapya 214 kwaajili ya Chanjo aina zote 15 ikiwemo chanjo ya Covid-19,

Nahapa lazima niwe mkweli kama mambo ni haya basi kumbeza Rais Samia Suluhu Hassan nikujitafutia laana za bure kwa Mungu kwani kazi hii ni ya Mungu mwenyewe,

Mtakumbuka awamu yetu ya tano katika kutekeleza Ilani ya CCM tulifanikiwa kununua Toyota Land cruiser ambulance mpya 117 kwa miaka mitano,

Hayati Dkt John Joseph Magufuli kwa kutununulia hizo ambulance lazima tuendelee kumuenzi na kumwombea pumziko jema,

Kwakuwa Tanzania tuna jumla ya Wilaya 139 na zote zina hospitali za Wilaya,

Wilaya zote baada ya hizi ambulance kufika kila Hospitali ya wilaya itapata ambulance mpya ( brand new) kwaajili ya kunusuru roho za Watanzania hawa masikini kwa kuwakimbiza kwenye hospitali za juu (referral hospitals).

Kwakuwa Tanzania pia tuna jumla ya Halmashauri zipatazo 184 ,

Nakwakuwa hesabu ya ambulance zilizoagizwa ni 395 basi kila halmashauri itapata ambulance mpya,

Ambulance hii mpya itakuwa ni kwaajili ya kuhudumia ama Kituoa cha afya ama Zahanati kwaajili ya rufaa za wagonjwa wao kwenda hospitali za Wilaya na Mikoa,

Watu wa Idara ya afya tunzeni sana mali hizi za Watanzania hawa masikini.

Ambulance hizi 395 ni mara tatu zaidi ya ambulance zote 117 zilizonunuliwa kwa miaka mitano yote ya awamu ya tano,

Jambo hili kwa Wale wenye kumbukumbu nzuri mtakubaliana na mimi kuwa hii halijawahi kutokea katika historia ya nchi hii,

" kama kuna mtu wa kumwombea kwa nguvu zote kwa sasa basi ni Rais Samia Suluhu Hassan "

photo_2021-10-12_12-01-52.jpg
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA
 
Mwingine alikuta Msogagang imekomba kila kitu BOT.
Mwingine kakuta BOT iko full sukumagang amekusanya.
Halafu unalinganishaje hawa watu.

Mwingine yupo tayari watu wachanjwe hata Kama watapata madhara ili pesa ipatikane.
Mwingine alipambania maisha ya watu wake.

Na kipimo kizuri ni baada ya miaka 5,hata JK alianza vizuri,ila mwisho sasa😂😂
 
why records, mbona miaka ya mwalimu, mwinyi, mkapa na jk hatuendaga kwa style hii, why now?
Mkuu wewe umesoma chuo gani kama hujui faida ya "Comparative advantage,"

photo_2021-10-12_11-23-19.jpg



Anaposema pesa ya dawa imeongezeka toka Tshs 31BL 2015 hadi 270BL 2020 hii sio rekodi,

Chadema acheni uchonganishi
 
jibu hoja nimekuuliza why now??
Mbona umejibiwa tayari,

Hii haijaanza leo,

Ndio maana umeoneshwa reference za Nyuma,

Kutoka 31b mwaka 2015 hadi 270b mwaka 2020 ,

Inatofauti gani na hii,

Ambulance 117 awamu ya tano na ambulance 395 awamu ya sita?




 
Unapiga tarumbeta za kipuuzi yaani unalazimisha michanjo ili upate ambulance ina maana watanzania ni viwete wote? Tafuteni namna ya vijana kuwa productive na kusaidia serikali kupata mapato sio kulialia mabeberu kila siku. Kenge wewe na bibio
 
Back
Top Bottom