Rais Samia atua Tanzania, aongelea mafanikio ya safari yake Marekani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
1651134662343.png

1651134786510.png

1651134703922.png

Akizungumza baada ya kurejea Nchini Tanzania kutoka Marekani, amesema Watanzania wategemee matunda kutoka Filamu ya TheRoyalTour na Nchi ijitayarishe kupokea wageni wengi

Amesema Fedha za kutengeneza Filamu hiyo zimetokana na michango ya Wafanyabiashara mbalimbali Ndani na Nje ya sekta ya Utalii iliyoanguka kidogo kutokana na mlipuko wa COVID19

Aidha, Rais Samia amesema akiwa ziarani amezungumza na Serikali ya Marekani na kunyoosha pale palipokuwa na changamoto, akisema "Sasa tupo vizuri, tunaenda nao vizuri sana"

Mambo zaidi aliyoongea Rais Samia.

Rais Samia Suluhu Hassan:
Uhusiano wa Tanzania na Marekani umetimiza miaka 60 mwaka 2021. Zamani tulikuwa zaidi kunyoosha mikono, tunaomba hiki na kile

Lakini sasa tumekubaliana pamoja na kwamba hayo yatakuwepo, uhusiano mkubwa ni Uwekezaji na Biashara

Rais Samia: Tulifanya mazungumzo na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa (Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani), tumekubaliana vizuri

Fedha kama ile tuliyoleta na kuipeleka kwenye Vituo vya Afya na Madarasa, tunatarajia kuna nyingine itakuja iende kwenye maendeleo

Rais Samia: Kuna kundi lilienda kufanya Mkutano na Meya wa Jiji la Dallas, na matokeo ya Mkutano ule ni kwamba wenzetu wamekubali na wana hamu wafanye undugu na Miji yetu

Tunaangalia uwezekano wa kuwa na ndege zitakazotoka moja kwa moja Dallas mpaka Tanzania kuleta wageni

Rais Samia: Katika mazungumzo yetu na Wafanyabiashara wa Marekani tumesaini mikataba ya makubaliano ya miradi ya kuja kuwekeza Tanzania, thamani tuliyopiga ilifikia Trilioni 11.7

Kazi ni kwetu kuwapokea hawa watu bila usumbufu na kufanya uwekezaji wao uwepo Tanzania
 
Uwanja wa ndege KIA, wanawanchi wakiwa tayari kumpokea Mama
 
Akizungumza baada ya kurejea Nchini Tanzania kutoka Marekani, amesema Watanzania wategemee matunda kutoka Filamu ya TheRoyalTour na Nchi ijitayarishe kupokea wageni wengi

Amesema Fedha za kutengeneza Filamu hiyo zimetokana na michango ya Wafanyabiashara mbalimbali Ndani na Nje ya sekta ya Utalii iliyoanguka kidogo kutokana na mlipuko wa COVID19

Aidha, Rais Samia amesema akiwa ziarani amezungumza na Serikali ya Marekani na kunyoosha pale palipokuwa na changamoto, akisema "Sasa tupo vizuri, tunaenda nao vizuri sana"
Safi Saaana Mh rais Samia Suluhu ....nasema Chapaaa kaziii narudia Chapaaaa kaazzii ...kama hukubaliane naye hamia Bunjumbula
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Akizungumza baada ya kurejea Nchini Tanzania kutoka Marekani, amesema Watanzania wategemee matunda kutoka Filamu ya TheRoyalTour na Nchi ijitayarishe kupokea wageni wengi

Amesema Fedha za kutengeneza Filamu hiyo zimetokana na michango ya Wafanyabiashara mbalimbali Ndani na Nje ya sekta ya Utalii iliyoanguka kidogo kutokana na mlipuko wa COVID19

Aidha, Rais Samia amesema akiwa ziarani amezungumza na Serikali ya Marekani na kunyoosha pale palipokuwa na changamoto, akisema "Sasa tupo vizuri, tunaenda nao vizuri sana"
Hatufungamani na upande wowote..
Sasa akazindue ROYO TUA kule kwa ' Ngumi jiwe' Putin 😊
 
Back
Top Bottom