Rais Samia anajenga barabara ya Same - Kisiwani - Mkomazi km 97

Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
1,002
524
Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kazi inaendelea kwa kasi katika kila kona ya nchi,Kaskazini baada ya kusahauliwa kwa muda leo mama anawafungua kwa kasi.


Ona hii barabara ya Same – Kisiwani-Mkomazi kujengwa lami,​


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same – Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46).
Screenshot_20211122-114713.png

Akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo Eng. Kasekenya amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha KM 11.9 ambapo ujenzi utaanzia sehemu ya Mroyo – Ndungu hadi Kihurio.
Screenshot_20211122-114742.png

Barabara hiyo ambayo inapita pembezoni mwa hifadhi ya taifa ya Mkomazi itachochea na kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi, kilimo, utalii na biashara kwa wakazi wa tarafa za Gonja, Ndungu, Kihurio, Bendera na Mkomazi wilayani Same na hivyo kukuza uchumi wa wakazi hao.

“Tumejipanga kuijenga barabara hii kwa lami na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Screenshot_20211122-114727.png

Aidha amekagua ujenzi wa madaraja ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu na kuzungumzia umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu hiyo ili itumike wakati wote wa mwaka.
Screenshot_20211122-114511.png


Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando amesema ujenzi wa madaraja na makalvati katika barabara ya Mwembe hadi Ndungu ni zoezi endelevu hivyo kuwataka wananchi kuepuka kulima karibu na hifadhi ya barabara ili kuepuka mmomonyoko wa udongo.

Naye Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela amesema ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi (KM 96.46), na Mwembe-Myamba-Ndungu (KM 90.19), ukikamilika utafungua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Same ambao kwa kiasi kikubwa unategemea shughuli za kilimo cha mazao ya tangawizi na ndizi na kuhuisha utalii katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi.
 
But huwezi kulinganisha na Kongwa wala Iramba
Kweli mkuu....kinachoturudisha nyuma wilaya ya Same ni mtandao wa bara bara....

Bara bara zinachochea Sana shughuli za maendeleo.....ilivyokuwa Rombo kipindi hakuna lami ni tofauti na sasa...unajisikia fahari ukiwa Rombo......

Naamini huu mradi ukikamilika utachochea Sana maendeleo kisiwani.......

CCM ni janga...haya mambo yalitakiwa kufanyika miaka 20 iliyopita
 
Haya mnaosema Rais Samia hafanyi kitu njoo mtazame hii,
Narudia tena,Tanzania tunaye Rais wa kujivuna na kujivunia
Na hawa wasichana wanaorudishwa shule,anajua ukubwa wa tatizo analolileta kwenye jamii kweli huyu?Machokoraa,umalaya,mzigo kwa wazazi na jamii kwa ujumla wa malezi,kuharibika kwa maadili ya jamii nk.Itakuwa vurugu tupu.
 
Kweli mkuu....kinachoturudisha nyuma wilaya ya Same ni mtandao wa bara bara....

Bara bara zinachochea Sana shughuli za maendeleo.....ilivyokuwa Rombo kipindi hakuna lami ni tofauti na sasa...unajisikia fahari ukiwa Rombo......

Naamini huu mradi ukikamilika utachochea Sana maendeleo kisiwani.......

CCM ni janga...haya mambo yalitakiwa kufanyika miaka 20 iliyopita
Sio kisiwan tu naiona ndungu ikifanana na hedaru
 
Back
Top Bottom