Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA TZS 35BL KUJENGA UWANJA WA "MUSOMA AIRPORT " ILI KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.​

3-25.jpg
Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma karibu na Sehemu alikozaliwa muasisi wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere,

Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma uliotelekezwa na awanu zote tangu Uhuru,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua mkoa wa Mara,,Uwanja huu pia utahudumia na maeneo ya jirani kama Simiyu na Mwanza,

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma|Mara na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo kwani kabla Watalii wengi walishuka uwanja wa KIA,

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakika hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan,
Wanabodi,

Hili ni swali tuu najiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea sasa. Kwenye Mwenge kinachokimbizwa nchi nzima, jee kweli ni ule mwanga tuu
Ingekuwa ni Amri Yake, Magufuli Angefutilia Mbali Mbio za Mwenge!, Jee Ni Amri ya Nani?!.

Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru
Leo siku ya Nyerere day katika kumdurusu Mwalimu Nyerere kuna maswali najiuliza Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?.
Nawatakia maadhimisho mema na mapumziko mema ya Nyerere Day.
P
 
Cheap!

Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.

Mengine yote usanii tu.

Acha roho mbaya,,uwanja wa ndege una umuhimu wake pia mkoa mara licha ya kuwa na hifadhi km serengeti,,,hakuna cha kujivunia,,mama kaweka pesa japo kiduchu kuboresha uwanja,,unatoa nyongo “”mama tunaomba tufungulie bandari ya musoma iliotuunganisha na watu wa Uganda na kenya
 
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA TZS 35BL KUJENGA UWANJA WA "MUSOMA AIRPORT " ILI KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.​

3-25.jpg
Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma karibu na Sehemu alikozaliwa muasisi wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere,

Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma uliotelekezwa na awamu zote tangu Uhuru,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua mkoa wa Mara. Uwanja huu pia utahudumia na maeneo ya jirani kama Simiyu na Mwanza,

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma|Mara na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo kwani kabla Watalii wengi walishuka uwanja wa KIA,

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakika hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan,
Hongera sana Rais Samia Suluhu kwa kazi nzuri unayoifanya
 
Back
Top Bottom