Rais Samia atoa rai kwa Umoja wa Mataifa kusaidia Serikali ya Tanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania ingependa Umoja wa Mataifa uwasaidie ili waweze kujenga yanayotakiwa na wananchi ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Umeme na Pembejeo za Kilimo

Ameeleza hayo Septemba 24, 2021 katika Mahojiano Maalum na Habari za UN huko New York Nchini Marekani alipohojiwa Anold Kayanda na kuulizwa kuhusu wito anaoweza kutoa kwa Umoja wa Mataifa

Rais Samia amesema, "Tukiweza kuyapatia yote hayo Uchumi utakua na Tanzania tutaweza kujenga jina letu"
 
Kwani tanzania tunahitaji msaada kutoka kwa mabeberu?

Sisi ni doona kantriiii bwanaaaa
Maaana wapinzani walikuwa wanatuchelewesha sana kupata maendereeoool
 
Shame! Nchi yenye madini kuanzia Uranium hadi tanzanite, gas, helium, almas, mbuga za wanyama! Tanzania yetu ni tajiri sana ila inaongozwa na wajinga kuliko hata hayati Chifu Mangungo!

Tangu umezaliwa hadi unakua majina ya viongozi ni haya Anne Makinda, Makamba, Kachwamba, Chenge, Sitta, nk na bado unategemea mabadiriko? UN wameshindwa kuiokoa Lybia, Congo, Lebanon, Iraq, waje waisaidie Tanzania....kama unaamini hivyo wewe ni marehemu ila bado mwili unatembea kupambana na covid tu!
 
Shame! Nchi yenye madini kuanzia Uranium hadi tanzanite, gas, helium, almas, mbuga za wanyama! Tanzania yetu ni tajir sana ila inaongozwa na wajinga kuliko hata hayati Chifu Mangungo!
Hayo maneno yamesemwa toka awamu ya pili, nini kimefanyika, ?kuwa na rasilimali na kuzitumia ni vitu viwili tofauti, bora hata huyu anayekubali waziwazi kuwa misaada inahitajika baada ya kujua ukweli kuwa uwezo wa kutumia hizi zetu pekee hana, Awamu ya tano licha ya kuwaaminisha watu kuwa hataki misaada na kila kitu anachofanya ni pesa za ndani nini kilitokea?si ndio taifa lilifikia hali hii, kila sehemu ni zaidi ya tabu tu, si afadhari hata huyu amekubaliana na WHO, angalau sasa anapata hata hizo pesa za COVID 19, zinasaidia kwenye mambo mengine.
 
Madini
Gesi
Vivutio vya utalii
Tozo
Yule tajiri ombaomba ndio TZ yangu.

Nalia na taifa langu
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania ingependa Umoja wa Mataifa uwasaidie ili waweze kujenga yanayotakiwa na wananchi ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Umeme na Pembejeo za Kilimo

Ameeleza hayo Septemba 24, 2021 katika Mahojiano Maalum na Habari za UN huko New York Nchini Marekani alipohojiwa Anold Kayanda na kuulizwa kuhusu wito anaoweza kutoa kwa Umoja wa Mataifa

Rais Samia amesema, "Tukiweza kuyapatia yote hayo Uchumi utakua na Tanzania tutaweza kujenga jina letu"
Tanzania sio kisiwa lazima tuangalie namna bora ya kuishi na mataifa mengine hapa ulimwenguni, kongole kwake Mama Samia
 
Back
Top Bottom