Rais Samia atoa pole kufuatia mauaji Daraja la Salender, ataka uchunguzi ufanyike

Ni mawazo yako ya kijinga tu

Ila huwezi kufurahi polisi kuuliwa/

Polisi ni mtanzania mwenzako anaweza kuwa baba ako,binamu,mjomba au hata rafiki yako.

Jaribu kuwa na akili japo ndogo yakufikiria police hawatoki nje ya tanzania ni hawa hawa ndugu Zetu
Kwani wale wanachama wa upinzani waliouwawa bure, kutekwa au wanaobambikiwa na polisi kesi za uongo za uhujumu uchumi, ugaidi wao si watanzania? sio ndugu zetu? hawana mioyo, au hawana damu?? Au ndo mkuki kwa nguruwe....?
 
Naona unafanya utani na risasi ww, kanda ya Ziwa ndio wamezoea risasi? Hivi ukiwa unaandika unajitoa ufahamu n kuonyesha how poor minded you are, tatizo practically hujui hata maana ya risasi.
Unaona sasa

Mwanaume wa Dar ... Nenda nyamongo, Tarime huko , uwapelekee habari za Risasi.


Kumbe wewe na familia yako. Mlijifungia ndani ,nakuingia uvunguni???

Wanaume wa Dar bana
 
Mfumo wa jeshi la police inabid liende kisasa.
Ni gharama kubwa kulifanya jeshi la polisi kuwa la kisasa.

Sidhani kama serikali ipo tayari kugharamia maboresho la jeshi hilo kuanzia mafunzo hadi IGP awe msomi, mwenye ueledi wa hali ya juu na mtaalam.

Mimi nimekuwa nikitoa mapendekezo humu kwa miaka mingi lakini utaambiwa "bwana Richard unazo fedha za kugharamia?

Bahrain wana tatizo kubwa la watu kuwashambulia polisi na kuwaua ni hiyo ni kutokana na polisi kuua hovyo raia khasa pale wanapoandamana.

Walichofanya Bahrain serikali imemwajiri kamishna wa zamani wa polisi mtaalam ambae ni mwingereza atokea Scotland Yard.

Yupo pale Bahrain na jeshi la polisi la sasa limekuwa laendeshwa kisasa baada ya kuanza kulifanyia reforms.

Hivyo ni uamuzi tu kutenga fedha na kuomba msaada wa kitaalam, nchi yetu ni tajiri kuzidi Bahrain.
 
Sasa uchunguzi huu sawa ufanyike......lakin mbona wa SOKO LA KARIAKOO hatukuskia lolote baada ya uchunguzi.
 
IMG-20210826-WA0086.jpg
 
Tukio hili linanirejesha kwa kilichomtokea Tundu Lissu.

Nani aliondoa ulinzi area D? Walinzi wangekuwepo bila shaka wangepambana na magaidi waliomshambulia Lissu.
Hivi hapakuwa na majibizano Toka kwa walinzi area D na vyombo vya usalama tukio la Lissu???!!!
 
..anasema walinzi waliondolewa.

..sasa serikali inatakiwa imkamate aliyeondoa walinzi.

..na kupitia huyo wawatambue wahusika wengine wa ugaidi ule.
Anayetuhumu ndiyo athibitishe...arudi kutoa maelezo upelelezi uendelee
 
Anayetuhumu ndiyo athibitishe...arudi kutoa maelezo upelelezi uendelee

..kwenye tukio lile Polisi / Jamhuri ndio wenye wajibu na mamlaka ya kutuhumu mahakamani.

..Polisi wanatakiwa wamkamate aliyeondoa ulinzi na wengine alioshirikiana nao kuwezesha tukio lile la ugaidi.

..Lissu ataitwa mahakamani kama mhanga wa tukio na shahidi wa serikali / jamhuri ktk shauri husika.
 
Back
Top Bottom