Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Hivi hawa huyo mwendazake, aliyesalimu amri kwa corona, alikuwa akiwaokota wapi?

Namtazama huyu afande anavyopokea amri, nabaki nashangaa tu na kujiuliza, hizo nguvu hao wahuni wanazitoa wapi?
Halafu kama vile nimezinduka uzingizini, nakumbuka ile kauli ya aliyewateua ya kuwataka vichaa kama yeye.
Alihakikisha kila mkoa unatawaliwa kwa namna ile ile alivyoitawala Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Halafu walinda usalama wetu mikoa yote ilibiwabidi kutii bila shurti maagizo ya hao hao vichaa!

Sote tunajua kwamba Baba wa Taifa, kama angekuwa bado yu hai, hangeweza kukaa kimya kwa hali iliyokuwa ikiendelea nchini kwa miaka mitano, je huyu kijana asiye na adabu angethubutu kumkanya achunge ulimi wake la sivyo atwangwe?
 
Hmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.

Anateua leo, jioni anatengua.

Kesho anateua, keshokutwa anatengua!

Hivi hao wateuliwa huwa hawafanyiwi vetting??

NB: Hizi press releases huwa zinatolewa saa ngapi usiku?
Chalamila sio mzima apelekwe muhimbili kupimwa akili
 
Nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu. Arudi kushika chaki ukizingatia bado kijana.
Mkuu inategemea amefikia "level" ipi katika mambo ya "bwaksi..." ikiwa "..pombe imeshakunywa mtu!!" Chaki haitashikika...
Tunawajua wengi walio kama yeye ndio maana tulionya mapema ili asaidiwe na "wanaompenda" lakini wapi... alisifiwa na mwisho wa siku akatapika kwenye altare...
 
Juzi Chalamila akizungumza na waandishi,aliwaomba wananchi wa Mwanza wampokee Rais kwa mabango,yeyote yale hata ya matusi!...hii huenda Ikawa sababu?....
Hapi kabaki duu.
 
Ally Hapi ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kwenye wilaya za mkoa wa Tabora. Jumatatu na Jumanne alikuwa anajitambulisha wilaya ya Kaliua, Jumatano na Alhamisi alikuwa wilaya ya Urambo, Ijumaa amehamishwa mkoa.

Sijui kama alishamaliza kujitambulisha Tabora. Kazi Iendelee.
, akaanze kujitambulisha tena Mara, aanzie serengeti
 
Hio font ya press release mbona haiko good kabisa, Atumie font kama ya Msigwa
 
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya Rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
Huyo ni mtu asiyejielewa, anafikiri anapewa uongozi kwa kumsifia Rais. Awamu hiyo ilishapita.

Kalikoroga sasa alinywe.
 
Hmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.

Anateua leo, jioni anatengua.

Kesho anateua, keshokutwa anatengua!

Hatimaye 'kichaa' apigwa chini...

Huo ukichaa alishajitamkia yeye mwenyewe huyo RC akiwa Mbeya
 
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya Rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
Hiyo ya matusi inazunguka mitandaoni lakini nimefatilia taarifa yake yote mbona hakuna aliposema mabango ya matusi? Media zili edit? Au video imetengenezwa kujustify kufukuzwa kwake? Alafu taarifa yenyewe ina zaidi ya siku tatu! Anyway wenye mamlaka ndio wanajua.
 
🤔 hmm….
 
Damu ya yule kijana aliye mrestisha ini pisi iringa imeanza kumwandama sasa, pole zake ex mkuu wa mkoa....
 
Back
Top Bottom