Rais Samia atakuwa hatari wa Demokrasia kuliko Hayati Magufuli

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Wale waliokuwa wanamuona Hayati Magufuli ni dikteta naomba tutafutane miaka miwili ijayo.

Magufuli alijiamini sana hakuwa muoga sana. Ila sasa Mama atakuwa hatari zaidi kwasababu ya hofu za namna alivyopata cheo na pili kimaumbile.

Leo gazeti limeshafungiwa na yale magazeti makali Mwanahalisi na Tanzania Daima hayajafunguliwa mpaka leo. Mbowe yuko ndani badala ya Uamsho

Mkutano wa pili wa Magufuli na Waandishi wa Habari aliwaambia" Watch it your not free to that extent" nasubiri mkutano wa pili wa mama na Waandishi tuone atawaambia maneno yale ya mkutano wa kwanza?

Vyama havifanyi mikutano siasa imehamia kanisani Ufufuo na Uzima nako wanataka kumdhibiti.

Unadhibiti vyama, magazeti, makanisa, misikiti n.k je watu watapumulia wapi?
 
Mama anaupiga mwingi sana ...muoga sana anawaogopa mno Sukuma Gang.....ametabiriwa hagombei 2025
 
Mama alishasema anaendeleza yale yaliyoasisiwa na Mtangulizi wake. Haya yanayoendelea ndiyo yaliyokuwa agenda kuu ya awamu ya pili ya wawili hawa.

Ukiangalia Kwa makini utagundua kuwa Mh Lema na Lissu kukimbia ni kwamba walishajua ni nini kitakachofuata baada ya Rais kuapishwa. Mashitaka yao tayari yalishaandaliwa. Kesi aliyonayo Mbowe ilikuwa ni miongoni mwa mashitaka yale dhidi ya Viongozi wa Upinzani.

Mwanzoni Mama alikuwa na hofu ya Mungu lkn waandaji wa mikakati ile walimuambia Mama bila kuyatekeleza yale yote yaliyopangwa na Mzee huteweza kuongoza. Tupe go ahead tutekeleze mipango yake yote. Mama bado alisita lkn mara baada ya wale jamaa kumpangia ziara ya Mwanza, aliporejea tu Jijini Mama hakuwa Yule tena. Sijui alikwenda kunawishwa na maji ya ziwa pale Busisi au ni nini kilimpata sijui. Kifupi ni kwamba Mama kawa katili kweli kweli lkn mwisho wake utakuwa ni mbaya kwani Mungu ni yule yule jana na leo.
 
Wamnamburuza anaburuzika wamemuonjesha utamu tayari, hawezi kuwa yule, wale jamaa sijui Wana chuo cha kufundisha ukatili?
 
Lakini kadri udikteta unavyozidi kuongezeka ndio utawala wenyewe wa kidikteta unavyozidi kuelekea ukingoni. Kiuzoefu waga inakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom