Rais Samia ataka uchunguzi ufanyike kubaini chanzo cha moto soko la Karume

Kila soko likiungua tutegemee the same speech kutoka kwa viongozi "UCHUNGUZI UFANYIKE" alafu hakuna majibu wala kufidia waliopoteza mali zao (mitaji yao)
Watanzania tumelogwa hakika
 
Kila soko likiungua tutegemee the same speech kutoka kwa viongozi "UCHUNGUZI UFANYIKE" alafu hakuna majibu wala kufidia waliopoteza mali zao (mitaji yao)
Watanzania tumelogwa hakika
Hii nchi ni kisanga
 
"Tutaaunda kamati itakayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchunguza kwa siku 14 kisha tutapokea majibu na kujua cha kufanya na wakati wote wa uchunguzi hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuendelea na biashara katika eneo hili tutaangalia utaratibu mwingine,"
Kazi imeisha. Wamachinga mmekalia dole la wahuni akina Makalla. Poleni sana waathirika wote. Poleni watanzania wote.
 
Ni Jambo Jema Na Itapendeza Iwapo Ripoti Ya Uchunguzi Itawekwa Wazi Na Wahusika Kuwajibishwa Ipasavyo. Hii Ni Bila Kusahau Ishu Ya Soko La Kariakoo Ambalo Nalo Liliungua.
 
Kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake!
Sina uwezo wa kuhesabu bati na tofali!
Wakuu wa mikoa ndio jicho langu!
Watu wazima sio vizuri kusimamiwa!
 
Rais Samia Suluhu ametuma salamu za pole kwa wafanyabiashara wote wa soko la mitumba la Karume jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania ambalo limeungua usiku wa kuamkia leo na kusababisha asilimia 98 cha mali zote za eneo hilo kuteketea.

Taarifa zinasema hakuna madhara kwa wananchi yaliyotokea ukiachana na hasara ya mali zilizopotea.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amewataka wafanyabiasha wa soko la Karume lililoungua kuwa watulivu huku akiahidi kuundwa kamati itakayochunguza kujua chanzo cha moto huo.

"Chanzo cha moto huo katika soko la Karume au mchikichini bado hakijulikani huku kukiwa na makisio ya hitilafu ya umeme, soko hilo limeungua kwa takribani asilimia 98 licha ya jitihada za kuudhibiti," Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameeleza.
Imeelezwa kuwa moto huo ulioteketeza sehemu kubwa ya soko hilo lenye wafanyabiashara zaidi ya 3,500 ulianza usiku wa kuamkia leo huku Jeshi la zimamoto na uokoaji likijitahidi kuuzima lakini uliteketeza soko hilo sehemu kubwa.

"Tutaaunda kamati itakayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchunguza kwa siku 14 kisha tutapokea majibu na kujua cha kufanya na wakati wote wa uchunguzi hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuendelea na biashara katika eneo hili tutaangalia utaratibu mwingine,"amesema bwana Makalla.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi limeandika kuwa kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya Ilala, Elisa Mugisha amesema;

"Na kwa bahati nzuri wakati huo tulikuwa tunatoka Mabibo ambako nako kuna nyumba ilikuwa inaungua moto na tulifika hapa ndani ya muda mfupi tulifika eneo la tukio lakini moto ulikuwa mkali kutokana na asili ya bidhaa wanazouza hapa mbao, maturubahi na nguo na vinasambaza moto kwa haraka tulijitahidi kuzunguka soko na kuanza kuzima."

"Tunachoshukuru Mungu hakuna madhara kwa binadamu na wala moto haukuvuka kwenda kwenye nyumba za wananchi kwa sababu tulikuwa na gari nne ," aliongeza mkuu wa zima moto.Mnamo mwezi Julai, Soko la Kariakoo liliungua huku chanzo cha Moto kikiwa hakijafahamika.

Tathmini zilionesha kuwa maduka zaidi ya 220 yalitekeketea kwa moto katika soko la Kariakoo lililopo jijini Dar es salaam.

Na serikali iliagiza masoko yote na vituo vya mabasi kuwa na huduma za zima Moto ili kupunguza changamoto zinazotokea majanga kama hayo.
Tungeambiwa Kwanza RIPOTI ya TUME ya kuchunguza MOTO wa SOKO la KARIAKOO
 
Back
Top Bottom