Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,395
- 3,899
Akiwa nchini Kenya, Rais Samia alieleza kuwa nia ya kuizuru Kenya mapema sana ilikuwa kujitambulisha kwa majirani kwa kuwa alikuwa "mpangaji mpya"!
Leo akizungumza na wanaoitwa "wazee wa Dar es Salaam" amekariri tena ya kuwa ataendelea kuzuru nchi mbalimbali akitoa sababu ileile ya "kujitambulisha kwa majirani" akiwa ni "mpangaji mpya"!
Kiongozi mzalendo anawajibika kueleza manufaa ya kila anachonuia kufanya. Inashangaza ni kwa nini Rais anakimbizana kujitambulisha kwa majirani, yaani utii wake upo kwa majirani na siyo kwa mwenye nyumba, watanzania waliompangisha Ikulu yao.
KWA kuwa mwenye nyumba anayo madhara ikiwa ni pamoja na kutompangisha tena, nilitegemea angeweka kipaumbele kuwazuru wananchi kwanza ndipo aanze kupepea iwapo kuna manufaa ya umma katika kupepea.
Nawasalimu kwa jina la Mwenyezi Mungu aliyeumba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kazi Iendelee 🇹🇿🇹🇿