Rais Samia: Askari mnalalamikiwa kushikilia leseni za madereva muda mrefu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado Askari wanalalamikiwa kwa masuala kadhaa ikiwemo kushikilia Leseni za Madereva kwa muda mrefu au kuwalazimisha kulipa faini papo hapo ilihali Sheria inampa muda Dereva wa kuilipa.

Amesema, "Kingine ni kuna ukamataji mwingi wa Vyombo. Ukipita Vituo vya Polisi utakuta Pikipiki nyingi zimepangwa, na nyingine hazionekani kama zimekamatwa jana na leo"

Ameongeza, "Makosa yasikilizwe, kesi imalizike ahukumiwe kosa. Vyombo vinabaki muda mrefu unahisi vimetelekezwa. Iangaliwe kwa undani kero hizi zinasababishwa na nini"
 
Kuna mmoja alikamata leseni ya dereva wangu akamwambia niifuate nyumbani kwake Kurasini. Niliishia kununua resheni ya nyumbani kwake ya wiki nzima😭
 
Suluhisho
  1. Kuwekwe vituo maalumu vya ukaguzi wa vyombo vya moto kwenye kila barabara
  2. Vituo hivyo vifungwe cctv cameras for transparency reasons
  3. Askari wasiruhusiwe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye mifuko yao katika vituo hivyo vya ukaguzi
  4. Kuwepo dawati la malalamiko dhidi ya askari kwenye kila mji na wapokeaji wa malalamiko wasiwe askari ...labda PCCB
  5. Kwenye hilo dawati la malalamiko kuwepo mashine za kurekodi malalamiko husika
VInginevyo Rais utachakaa kero ni nyingi na huwezi kuzifuatilia zote, omba mashine zikusaidie ili haki unayoihubiri ipatikane bila uonevu
 
Suluhisho
  1. Kuwekwe vituo maalumu vya ukaguzi wa vyombo vya moto kwenye kila barabara
  2. Vituo hivyo vifungwe cctv cameras for transparency reasons..
Ikiwa hivi faini n rushwa zitapungua, kwa sasa kila baada ya umbali mfupi kuna geti na kila geti lazima utoe si chini ya 3000 madam tu unafanya biashara ya abilia, hawajali mafuta yamepanda yaani taabu sana
 
Kampeni zikianza magari yote mnawapa CCM na hayo ndiyo malipo yenyewe
Kiongozi katika biashara huwezi kubagua wateja, akija CCM, CHADEMA, ACT, CUF et all amekupa mkwanja unachukua, sidhani kwa mfano dukani utakuwa unabagua wateja huyu ni adui yangu nisimuuzie hiyo siyo biashara
 
Back
Top Bottom