Rais Samia ashuhudia utiaji saini Ujenzi wa SGR kipande cha Nne (Tabora - Isaka 165km), aeleza kutoridhishwa na utendaji wa TPA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959


AMOS MAKALLA – RC DAR ES SALAAM

Mh. Rais SGR itategemea sana bandari. Nikushukuru sana kwa kutoa fedha bilioni 210 za kuboresha Bandari.

- Bandari zimeboreka, mizigo kibao
Fedha zile ulizozitoa zimeleta manufaa makubwa. Hapa Dar es Salaam wanasema Bandari sasa ni mgodi – yaani ni mgodi kama ilivyo migodi ya madini. Kwa maana Bandari yetu sasa mizigo imeongezeka. Meli zimeongezeka.

Mh. Rais, nilikuwa napitiapitia; Congo mizigo yao ilikuwa tani milioni 1.9, sasa ni milioni 2.6. Burundi wanategemea Bandari ya Dar kwa asilimia 99.

Uganda walikuwa hawatumii Bandari yetu lakini kwa ziara zako nchini Uganda umemshawishi Rais Museveni. Wametoka tani laki 1 na 40 sasa wapo tani laki 3.

MASANJA KADOGOSA – MKURUGENZI MKUU TRC

Mh. Rais, leo tunakutana katika hafla fupi ya kutiliana saini mikataba miwili – Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha 4 (Tabora – Isaka) na Mkataba wa Mafunzo kwa Vitendo kati ya TRC na Shirika la Reli la Korea (Korea Railway).

- Rais Samia ametekeleza ahadi
Tukio la leo Mh. Rais, linafanya vipande vyote sasa vitano kwa maana ya kutokea Dar mpaka Mwanza, vina wakandarasi. Kwa maana phase ya kwanza.

Wakati ukilihutubia Bunge mwaka 2021 uliahidi kuendelea na kukamilisha ujenzi wa reli ya Dar – Makutupora na kuanza ujenzi wa vipande vingine kikiwemo kipande cha Mwanza – Isaka, Makutupora – Tabora, Tabora – Isaka, na leo tunashuhudia ahadi yako ikikamilika.

Mh. Rais uliahidi pia kuanza ujenzi wa reli awamu ya pili yenye kilomita 1010. Kwa maana ya kipande cha Tabora- Kigoma (km 411); Uvinza-Kitega, Burundi (km282) na baadaye kuendelea na vipande vingine.

Mh. Rais, naomba kutoa taarifa kuwa kazi ya manunuzi inaendelea.

- Thamani ya reli
Thamani ya reli hii, kwa maana ya utiaji saini wa leo, utafikia takribani trilioni 16.7 kwa awamu ya kwanza (Dar – Mwanza) na serikali hadi sasa imelipa malipo ya jumla ya Sh. Trilioni 6.4. Malipo ya kazi yote inayotekelezwa na kuhakikiwa. Kama nilivyotaja hapo, Mkandarasi hatudai kitu chochote.

Maendeleo ya hatua ya ujenzi kwa vipande vitano (km 1219), kipande cha kwanza tunaendelea na majaribio ya mifumo mbalimbali na – tunaendelea vizuri sana. Kwa sasa hivi sehemukubwa ya ujenzi iliyobakia ni kutoka Ilala kuingia Bandarini.

Serikali inajenga mifumo ya umeme ya kupitisha umeme wa kilowatts 220 kwa maana ya kwamba kipande cha Dr – Morogoro kimekamilika asilimia 100, na kipande cha Makutupora- Dodoma kimekamilika asilimia 90. Na chenyewe tunaendelea vizuri sana.

Thamani ya mkataba tunaosaini leo ilakuwa dola milioni 900.1 (Tsh. Trilioni 2.094) na hii inajumuisha kodi.

- Capacity building kwa watendaji
Kwenye uendeshaji tutapata capacity-building kutoka kwa Korea Railway. Tutakaokuwa tukiendesha huu ni sisi Watanzania (Kwa maana ya TRC) kuhakikisha hakuna kitu kinakwenda kinyume na matarajio yako Mh. Rais lakini pia na matarajio ya Wananchi.

Tuliamua kutafuta Shirika la Reli ambalo ni bora zaidi ili wakati tutakapoanza uendeshaji kutakuwa na watendaji wenye uzoefu. Baada ya kushindanisha, wenzetu wa Korea walipata hiyo kazi. Kwahiyo kule kwenye maintenance kutakuwa na mainjia behind, kwenye signory tutakuwa na mainjinia behind, kwenye operations tutakuwa na mainjinia behind, kwenye control kutakuwa na mainjinia behind. Kila sehemu ya uendeshaji kwa miaka mitatu.

Treni yetu itakuwa ni hi-tech, yaani itaendeshwa kwa teknolojia ya juu. Ni lazima tuwe na tahadhari ya kuhakikisha kuwa uwekezaji huu mkubwa unakuwa na tija.

Wengine watajengewa uwezo hapahapa ndani na wengine nje ya nchi.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

- Sheria za 'PPP' na Manunuzi ziangaliwe

Hizo Sheria kazitazameni, badala ya kutupeleka mbele zinaturudisha nyumq. Dunia ya sasa amekuja mtu, mnaelewana, ana uwezo, mnamuamini, mnasaini na kwenda mbele. Kuanza kuzunguka Sheria ya PPP haikufuatwa, mtu na Fedha anatafuta kwingine pa kwenda

- Siridhishwi kabisa na utendaji wa bandari zetu
Wale tuliowakabidhi uendeshaji wa bandari zetu wafanye kazi kwa kasi mno, siridhishwi kabisa na kazi za bandari, siasa na longolongo zilizopo. Huko nje wanaendesha kwa kasi mno sisi bado tunasuasua, wawekezaji wanakuja tunawazungusha

Nasema bandari watu wafanye kazi, tutatupia jicho, waliokabidhiwa bandari nataka tuelewane vizuri. Bandari ya Dar ikifanya kazi vizuri nusu ya bajeti itatokana na bandari hiyo. Wale mliokabidhiwa bandari nataka tuelewane

- Mwanza, Tabora kuwa Vitovu vya Biashara nchini
Lengo ni kuifanya Dar es Salaam kuwa kitovu kikuu cha biashara Afrika, baada ya hapo Mwanza itafuata katika Kanda ya Ziwa Victoria, pia Tabora kuna reli, bomba la mafuta na barabara

- Wenye akili za kawaida wanalaumu Rais anasafiri tu
Wale wenye akili za kawaida ni rahisi kulaumu, wanasema ‘Rais anasafiri tu, hakai, hatembelei mikoa’, nikienda mkoani tajenga siasa ya ndani hakuna maendeleo, nikienda nje nakwenda kutafuta fedha za maendeleo.
 
Hongera zake. Kila siku anatia tu saini! Kipande cha kutoka Dar Moro, mwaka wa 2 huu, ni sound tu.

Mara treni itaanza rasmi safari zake mwezi fulani! Ukifika huo mwezi wanasogeza tena!
Wewe jua tuu lazima reli ifike Mwanza,Kigoma,gitega na Karema
 
Nitafurahi siku itakapokuwa mpakani na DRC, BURUNDI.

Kwa njia ya kupakia abiria haitalipa na itakuwa aghali
 
Mwisho wa siku awamu ya sita itakuwa kinara wa ujumla kwenye kazi kubwa ya ujenzi wa reli tokea kipindi Cha kuanzisha wazo,kuandaa mpango na fedha pamoja na usanifu wakati wa Jakaya Kikwete, mpaka kuanzisha ujenzi na maboresho ya Mwamba Magufuli na hatua ya kukamilisha ujenzi wa MAMA Samia.

Hongera Sana Mama Samia. Uneonyesha ukakamavu na kutoyumba.
 
Back
Top Bottom