Rais Samia ashtukia upigaji Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA)

Toka maktaba:

16 Juni 2021

Bagambilana : miradi yote 5 ya meli itagharimu Sh bilioni 438.8.

Tunamuenzi JPM miradi ya meli​

News Images

Picha toka maktaba hafla ya kuzindua chelezo Mwanza Kusini South Mwanza

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema mikataba mitano iliyosainiwa jana Mwanza ya ujenzi na ukarabati wa meli ni kazi nzuri ya kumuenzi Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli ambaye ni mwanzilishi wa miradi hiyo.

Aliyasema hayo jijini Mwanza baada ya kuzindua chelezo, meli ya New Victoria ‘Hapa Kazi Tu’ na meli ya New Butiama ‘Hapa Kazi Tu’ pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya ujenzi wa meli mpya nne na ukarabati wa meli ya zamani.

Rais Samia alisema anajisikia faraja kushuhudia kukamilika kwa ukarabati huo wa meli, kusainiwa kwa mikataba na kukamilika kwa ujenzi wa chelezo.

“Kama ingekuwa haijakamilika roho zetu zisingejisikia vizuri kwa sababu mwanzilishi wa miradi hii ameitwa na Mungu na ameitika, kama anatusikia bila shaka anafarijika,” alisema Rais Samia.

Alisema ni dhamira ya serikali kuifanya Mwanza kuwa kituo kikubwa cha biashara kwa kuwa Mwanza iko kwenye ukanda wa mikoa wazalishaji wakubwa wa mazao wa chakula na biashara na mazao ya uvuvi, hivyo serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na miundombinu laini ya kuboresha mawasiliano ya kimtandao.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Philemon Bagambilana alisema ukarabati wa meli hizo ulianza Januari 2019 kwa gharama ya Sh bilioni 27.6 na zilianza kufanya kazi tangu Agosti mwaka jana.

Alisema meli ya New Victoria ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo wakati New Butiama ina uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo.

“Meli ya New Victoria inafanya safari zake mara tatu kwa wiki kati ya Mwanza na Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo, na meli ya New Butiama inafanya safari zake kila siku kati ya Mwanza na Nansio Ukerewe,” alisema Bagambilana.

Aliongeza, “Ujenzi wa chelezo nao ulianza Januari 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 36.4, ni chelezo kikubwa kupita vyote katika Ziwa Victoria.”

Alisema meli ya New Victoria ilitengenezwa mwaka 1960 na meli ya New Butiama ni ya mwaka 1980.

Kuhusu mikataba mitano iliyosainiwa, alisema mkataba wa kwanza ulihusu ujenzi wa meli mpya katika Bahari ya Hindi kwa kulenga soko la Comoro na mkataba wa pili unahusu ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba tani 3,000 za mizigo kwa kulenga ujio wa Reli ya Kisasa (SGR).

Mingine ni ya ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Ziwa Tanganyika; wa nne ni ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo, na mkataba wa tano ulihusu ukarabati wa meli ya Mv Umoja yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na pia ina reli ndani yake.

Bagambilana alisema miradi yote hiyo itagharimu Sh bilioni 438.8.

Source : MSCL
 
Kutoka ziara ya Rais Samia,
Bandari Kuu Dar es Salaam.

Ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta, kwanini TPA ilianza ujenzi wa matenki mapya wakati PUMA ina matenki yako tupu na hayatumiki kwanini yasitumike hayo kulikuwa na sababu gani ya kujenga mapya kama sio uchochoro wa kupiga fedha???

2. Mkataba wa ujenzi wa meli tano, kampuni ya YUTEK iliyoshinda zabuni ambayo inatoka Uturuki baada ya kuchunguzwa ikabainika haina sifa wala haijawahi kujenga meli ila ni kampuni ya kidalali....

3. Amevunja bodi zote 2; kampuni ya huduma za meli na TPA

4. Ameapa kulinda maslahi ya Nchi na haki za wananchi kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa weledi na thamani ya fedha huku akihakikisha hakuna hata senti itakayopotea.

SITOKUBALI JUMBA BOVU LIANGUSHIWE AWAMU YA SITA WAKATI UFISADI ULITOKEA HUKO NYUMA

#SamiaKazini
#KaziIendelee
View attachment 2032524
Rais fukuza hao mbwa wote na wafikishe mahakamani
 
Mh rais tunajua una mapenz mema na wananchi hutak hata sh 1 ipoteee ila wanaccm wanakuhujumu ili wawez kukuheshimu ukimaliza mihura yako kamilisha mchakato wa katiba mpya ndo utakuwa mwisho wa jeuri ya hao CCm
 
Actually, hii ni awamu ya 5 ambayo Rais wake alibadilika baada ya kifo cha aliyekuwepo. Kuiita awamu ya 6 ni utapeli mwingine tu.
Hiki ndio moja ya kituko ninacho shangaa hata mimi sijaelewa maana kwanini inaitwa awamu ya 6.
 
Alishauriwa mapema awateme wateule wa Magu yeye kaamua kuwa kumbatia. Acha wamhujumu. Huku wezi, kule kumchafua kwa kesi za kubumba. Hadi akome. Siro hakustahili kuwepo ofisi ya umma leo... Alistahili kuwepo magereza.
Huyu Hangaya alianza vizuri lkn alikujajichanganya hasa pale alipoambiwa na Sukumagang atulie wamuonyeshe namna Jiwe alivyokuwa akiendesha nchi na pia namna alivyokuwa akuwashughulikia baadhi ya watu hususani wapinzani. Haya uliyoyasema ndiyo madhara yake.

Juzi nikiwa mpakani Namanga nilishuhudia malori yakiwa yamesheheni vitunguu, mahindi pamoja na mazao mengine. Kilichonisikitisha ni pale nilipoyaona malori mengine yakiwa yamesheheni ng'ombe. Nikakumbuka tulivyokataa kusafirisha ngozi mbichi nje ya nchi. Sasa Jamaa wameamua kupelekwa ngozi na nyama Kwa pamoja.
 
Acha kuongea nonsense mkuu, kama walikuwa hawasikilizwi siwangejiuzulu kwa maslahi mapana ya nchi. Hakuna namna ya kukwepa lawama hapa.
Wewe unafikiri usalama wa taifa utakubali kiongozi wa juu wa serikali kama huyo ajiuzulu kwaajili ya kupishana na boss wake? Kuna kipindi 2016 alitaka kujiuzulu huyu mama, usitake kuniambia hukusikia. Na kama hukusikia maana yake sio mfuatiliaji wa siasa za Tanzania
 
Rais Samia ashtukia upigaji wa mabilioni ya fedha

Ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta, kwanini TPA ilianza ujenzi wa matenki mapya wakati PUMA ina matenki yako tupu na hayatumiki kwanini yasitumike hayo kulikuwa na sababu gani ya kujenga mapya kama sio uchochoro wa kupiga fedha???

2. Mkataba wa ujenzi wa meli tano, kampuni ya YUTEK iliyoshinda zabuni ambayo inatoka Uturuki baada ya kuchunguzwa ikabainika haina sifa wala haijawahi kujenga meli ila ni kampuni ya kidalali....

3. Amevunja bodi zote 2; kampuni ya huduma za meli na TPA

4. Ameapa kulinda maslahi ya Nchi na haki za wananchi kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa weledi na thamani ya fedha huku akihakikisha hakuna hata senti itakayopotea.

SITOKUBALI JUMBA BOVU LIANGUSHIWE AWAMU YA SITA WAKATI UFISADI ULITOKEA HUKO NYUMA

#mamayukokazini
#SamiaKazini
#KaziIendelee

IMG_20211204_130918_089.jpg
 
Rais Samia ameelezea tatizo na hatua alizochukua.
Kuhusu katiba mpya ,Kenya kuna katiba mpya lakini Rais Kenyatta na Makamu wake wanaparurana wazi wazi.Kudhani kwamba katiba mpya ndio magic bullet ya matatizo ni kuwa naive.
Inawezekana alishauri ushauri ukakataliwa.Who knows?
Kumpa Rais ultimatum ni kupoteza muda tu.
Kulaumu ni rahisi sana kuliko kuleta solutions.
Kuparurana waziwazi ndiyo matokeo chanya ya katiba mpya. Wewe ndiyo naive.

Katiba haiwezi kuwa magic bullet ya matatizo. Lakini lazima katiba iruhusu accountability. Lasivyo matatizo yataendelea kuwepo huku kila kiongozi akijivua uwajibikaji.

Kama kuwa kiongozi ni free ticket ya kufanya ufisadi with impunity, then katiba itakayoondoa huo udhaifu, inaweza kuwa “a magic bullet” kwenye kumaliza ufisadi na uongozi wa hovyo hovyo usiokuwa na uwajibikaji.
 
04 December 2021
Dar es Salaam, Tanzania

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIZINDUA MABORESHO YA GATI (0-7) BANDARI YA DAR ES SALAAM

Source : Ikulu Tanzania
 
As if awamu ya tano hakuwepo kama makamu wa Rais. Nafasi ambayo ilitakiwa awe mshauri wa rais. Katiba mpya ina umuhimu sana.

Wale wale waliokuwa viongozi wakubwa kabisa wa awamu ya tano wakati wa madhambi hayo, eti wanasema madhambi siyo ya awamu ya sita!🤦🏾‍♂️

Hapo ina maana rais peke yake ndo mtendaji wa serikali.

“There must be somewhere where the line is drawn”
Aliyekuwa top alishirikisha mtu?
 
Kuparurana waziwazi ndiyo matokeo chanya ya katiba mpya. Wewe ndiyo naive.

Katiba haiwezi kuwa magic bullet ya matatizo. Lakini lazima katiba iruhusu accountability. Lasivyo matatizo yataendelea kuwepo huku kila kiongozi akijivua uwajibikaji.

Kama kuwa kiongozi ni free ticket ya kufanya ufisadi with impunity, then katiba itakayoondoa huo udhaifu, inaweza kuwa “a magic bullet” kwenye kumaliza ufisadi na uongozi wa hovyo hovyo usiokuwa na uwajibikaji.
Hujui hata una argue nini.Aya yako ya pili inakinzana na aya ya 3.
Kiongozi yupi ana free ticket ya kufanya ufisadi with impunity?
Katiba ipi inaruhusu hicho?
Una frustration ya jambo lingine(na wewe unalijua) unaliingiza kwenye uwajibikaji.Nani amejivua uwajibikaji wakati hatua zinachukuliwa.Hakuna Nchi ambayo ni Utopia my friend .
 
Magufuli hakutaka kusikiliza la mtu. Msijitoe ufahamu nyinyi
Kwanini asingejiudhuru kuonesha msimamo wake!????

Mama asijitetee nae ni wale wale.. kwa wenzetu, bosi akifanya mafyongo na anagoma kupokea ushauri, mtu anajiudhuru, watu wanajiudhuru kisa tu umeme kukatika tena yeye ni waziri wa nishati na sio engineer wa huko, itakuwa yeye mama!?
 
Back
Top Bottom