BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 327
- 414
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Posta- Ngara Mjini Mkoani Kagera kuanzia Saa 4 asubuhi hii.
Utafuatilia matangazo haya ya moja kwa moja kupitia Televisheni, Redio na Mitandao ya Kijamii.
=======
Askofu Niwemugizi: Nikushukuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, mwaka 1997 nilipewa heshma kubwa sana ya kuwa na hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na hayati Benjamin Mkapa, Rais wa nchi wakati huo nilipopewa uaskofu na kusimikwa pale Rulenge, leo umenipa heshima wewe mheshimiwa Rais ambayo haitatoka moyoni mwangu.
Mimi ni mtu mdogo sana, sasa kwamba wewe unaacha majukumu yako unakuja hapa, ntaachaje kukumbuka. Asante sana, Mungu akubariki.
Nakupa pole kwa safari ndefu ya ughaibuni lakini nakupongeza kwa kuliwakilisha Taifa letu vizuri huko ulikokuwa kwa mikutano ya kimataifa. Kutojihurumia na kusafari tena baada ya safari hiyo ndefu nje ya nchi na kutenga muda ufike Ngara kwenye adhimisho hili ni heshima kwangu na kwa wanajimbo la Rulenga, Ngara.
Kufika kwako nakutafsiri kama ishara ya wewe kutaka kuwa karibu sana na kushirikiana na viongozi wa dini zote kusikilizana nao na kushauriana nao katika masuala muhimu ya kulijenga Taifa letu.
Mimi nakuahidi, niko tayari kukuunga mkono kushirikiana na Serikali yako kwa kuzingatia ukweli, kukuza haki na amani nchini mwetu.
Hospitali za Biharamulo ambazo ni hospitali teule ya wilaya na hospitali ya Rulenge. Hospitali hizi hazifanyi biashara, kile kinacholipwa kidogo ni kuziwezesha tu ziendelee kutoa huduma, kwa hakika zikifungwa hospitali hizi wananchi wataumia.
Tunaomba madeni tuliyonayo ya TRA tusamehewe kwasababu yanatuelemea kwelikweli toka mwaka 2015 mpaka 2020 Biharamulo inadaiwa milioni 113 na hospitali ya Lulenge inadaiwa milioni 213.
Kwakuwa mheshimiwa Rais hospitali hizi zinawahudumia raia wako, basi ikikupendeza utusamehe, pia ikiwezekana utusaidie kupata vibali vya ajira tuboreshe huduma kwa kuwa idadi ya watumishi itayotuwezesha kutoa huduma bora kwa raia wako wa Tanzania.
Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.
Rais Samia: Kumekuwa na matukio mengi ya mauaji na Watu kujiua kwa kipindi hiki, takwimu zinaonesha katika Wilaya hii ya Ngara pekee mwaka 2020 kulikuwa na matukio 22 ya mauaji na matukio matatu ya Watu kujiua,mwaka 2021 kulikuwa na matukio 21 ya mauaji na mawili ya Watu kujiua
Kuna sababu nyingi zinazofanya kuongezeka kwa matukio ya vifo na mauaji, huwa tunaunda Tume ndani ya Polisi kuchunguza sababu, ripoti zinapokuja wanasema, wivu wa mapenzi, imani za kishirikina, msongo wa mawazo, visasi, ugomvi wa kifamilia, ugumu wa maisha n.k
Ukiangalia sababu za mauaji zinakuonesha kwamba Watu hawako karibu na Mungu, hakuna Dini iliyotoa ruhusa kujiua au kuua, na tunafunzwa kuamini kwamba kifo kinapotokea ni kazi ya Mungu sasa sina hakika wanaojiua au kuua wenzao kama ni kazi ya Mungu sina hakika
Baba Askofu Niwemugizi umezungumzia mmomonyoko wa maadili na pia Watu kusahau mila na desturi ambako kumeondosha utu wetu, tuna kazi kubwa Viongozi wa Dini kurudisha tena nyoyo za Watu kuthamini utu, kurudisha tena Watu kumjua Mungu
Kama unamjua Mungu huendi kumuua mwenzio kwa urithi, kisasi au kwamba umeambiwa amekuroga hukuvuna huendi kumuua mwenzio kama kweli unamjua Mungu, nitoe wito kwa Viongozi wa Dini turudi kwenye mafundisho yetu tuisaidie Jamii