Rais Samia ashiriki mkutano wa COP27 nchini Misri. Awakutanisha marais 11 kujadili umeme

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,712
Leo tarehe 07 Nov. 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania alishiriki mkutano wa 27 wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo umefanyika kwenye mji wa Sharm El Sheikh. Rais Samia ameambatana na Waziri wa mambo ya nne na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Stergomena Tax.

1667858855515.png

---

Rais Samia awakutanisha marais 11 kujadili umeme​

Ni katika mkutano wa COP 27 unaoendelea nchini Misri kuanzia Oktoba 31 mpaka Novemba 18.

Dar es Salaam. Kutokana na upungufu wa megawati zaidi ya 6,000 unaozikabili nchi za kusini mwa Afrika, Rais Samia Suluhu Hassan kesho ataongoza mjadala ya kuongeza uzalishaji wa umeme na usambazaji wake katika mkutano wa 27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Tabianchi (COP 27) kutafuta suluhu ya kudumu.

Rais Samia amewaalika wakuu wenzake wa nchi 11, rais wa Benki ya Dunia na rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ili kufanikisha uzalishaji na usambazaji wa nishati ya kutosha kwa ajili ya viwanda vinavyoendelea kujengwa barani humu.

“Mara zote Tanzania ilikuwa mshiriki tu, hii ni mara ya kwanza tunaandaa mkutano wa pembeni unaowakutanisha wadau muhimu. Kwa sasa, kwa ujumla tuna upungufu wa megawati 6,000 lakini miaka mitano ijayo utafika megawati 10,000. Tunahitaji nguvu ya pamoja kuwekaza,” amesema Januari Makamba, Waziri wa Nishati.

Waziri Makamba amesema Afrika huzalisha umeme kwa ushirikiano wa mataifa kadhaa (power pools) na Tanzania ni mjumbe wa ushirika wa mataifa ya kusini (Southern Africa Power Pool) ulioanzishwa mwaka 1997 ukilenga kuimarisha uzalishaji na usambazaji ili Taifa litakalokuwa na ziada liliuzie lenye upungufu.

“Tangu SAPP ianzishwe hakujawahi kuwa na umeme wa kutosha hata miundombinu ya usambaji haikujengwa. Sasa hivi Tanzania tunakamilisha njia ya usambazaji kwenda Zambia na ile ya Kenya itakayokamilika Desemba. Kwa ukubwa wa soko letu, itakuwa rahisi kupata mkopo nafuu.

Rais (Samia) amewaita wadau ili kujadiliana vyanzo mbadala hasa umemejua na upepo vinavyoweza kuchangamkia na kampuni kubwa za nishati,” amesema Makamba.

Kwa sasa, waziri alisema Tanzania inavyo vyanzo vinavyoweza kuzalisha zaidi ya megawatu 2,000 za umemejua na upepo na tayari Serikali inatekeleza miradi ya kuzalisha megawati 300 akitolea mfano uliopo Kishapu mkoani Shinyanga na Singida.

Takwimu zilizopo zinaonyesha nchi wanachama wa SAPP zina vyanzo vya kuzalisha zaidi ya jigawati 10.3 vinavyoweza kuendelezwa ndani ya miaka 10 ijayo na kukidhi mahitaji iwapo zitajenga giridi ya kilomita 6,085 kuusambaza kwa wananchi wao.

“Tunahitaji uwekezaji wa dola 18 bilioni za Marekani kukidhi mahitaji yatakayoongezeka kwa miaka mitano ijayo katika mataifa yote 12 ya SAPP,” amesema Makamba.
 
Aya kila la kheri chifu kwa kuwakutanisha marais 11.
Nadhani upo uwezekano wa kuja na jibu mbadala dhidi ya umeme unaotegemea maji.

Hali ya tabianchi imeleta mkanganyiko mkubwa kijamii. Utoshelevu wa maji kwa matumizi ya viumbe hai umekuwa mdogo sana. Tunahitajika kama nchi zinazoendelea kujinasua kwa kujiunga pamoja kulinda ba kuboresha mazingira yetu kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ningelipata nafasi ya kumshauri Rais, ningemuomba ashirikiane na wenzake kuunda baraza ama umoja wa nchi za uchumi wa kati na wa chini ili wawe na forum ya kujadili vipaumbele vya nchi hizo na kuweka misimamo inayoweza kuiokoa dunia.

Kama nchi tajiri duniani zina umowa wao na clubs zao. Inabidi sisi wa chini ya hapo tuwe na sauti yetu inayoweza kutuunganisha pamoja bila kujali mabara tunayotoka.

Ikumbukwe kwamba nchi tajiri zinategemea sana umaskini wetu ili ziendelee kutajirika zaidi.

Ni muda wa kuwa chanya kwa ajili ya mataifa yetu. Tupige hatua za kuiondoq dunia kutoka kwenye ukingo wa maangamizi yatokanayo na uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli za maendeleo na kiuchumi wa nchi zenye ukwasi mkubwa. Nchi hizo zimejipa ukinara wa kuamua hatima ya dunia. Nchi hizo zinatoa ahadi za kuwekeza kwenye kulinda na kutunza mazingira lakini hakuna lolote zimefanya hivyo kuuweka ulimwengu hatarini.

Rais naamini anaweza kuchukua mawazo yetu wakaangalia namna ya kuyafanyia kazi
 
Wenzake huwa wanaahurisha safari na mikutano. Lkn ndiyo hivyo tena, amefurahia kuona mbuzi 19 wa kafara wamekwenda peponi
Yaani vifo vya raia 19 ndiyo vizue mkuu wa nchi kuhudumia raia milioni 61+ ?.Dah!Kweli watz mlio wengi uwezo wa KUFIKIRI NI MDOGO.
 
Dar es Salaam. Kutokana na upungufu wa megawati zaidi ya 6,000 unaozikabili nchi za kusini mwa Afrika, Rais Samia Suluhu Hassan kesho ataongoza mjadala ya kuongeza uzalishaji wa umeme na usambazaji wake katika mkutano wa 27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Tabianchi (COP 27) kutafuta suluhu ya kudumu.

Rais Samia amewaalika wakuu wenzake wa nchi 11, rais wa Benki ya Dunia na rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ili kufanikisha uzalishaji na usambazaji wa nishati ya kutosha kwa ajili ya viwanda vinavyoendelea kujengwa barani humu.
Hili tatizo la umeme limekuwa likijirudia kila awamu.

Wakati wa Mwinyi alituletea IPTL tukafikiri tumepata suluhisho la tatizo lakini tatizo halikumalizwa.

Lilipojirudia tena wakati wa Kikwete tukaamini pengine wawekezaji wa Richmond toka Marekani wangemaliza tatizo, lakini tatizo la umeme bado lipo palepale na warithi wa Richmond tunaambiwa wanalipwa mabilioni ya shilingi, sijui kwa kazi gani wanayotufanyia.

Pengine utawala huu utakuja na suluhisho la kudumu.
 
Ni vile tunaiamini sana CCM badala ya kuwaamini Watanzania
 
Back
Top Bottom