Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,806
Rais Samia leo ameongelea ushauri ambao anaweza kuwapa wanawake viongozi wa sasa. Rais Samia amesema wasijikite kwenye misingi ya uongozi ya chuoni pekee. Ni muhimu kutambua na kujua lengo na ni muhimu kuwa mnyenyekevu ikiwemo kuwasikiliza watu zaidi na kuzungumza kidogo.
Rais Samia kasema ni muhimu kuwasikiliza hata wale wanaodhaniwa ni wapumbavu kwasababu wanaweza kuwa na kitu cha msingi cha kujifunza kutoka kwao. Pia kuelewa jamii yako unayotaka kuwasiliana nao.
Ushauri wa mwisho Rais Samia amesema ni muhimu kujifunza kutoka kwa watangulizi, wale ambao wanafahamu taasisi unayoifanyia kazi kwani wapo wazoefu, watangulizi ambao wamekuwa kwenye ofisi husika kwa muda mrefu, Rais Samia amewataka viongozi kuwasikiliza lakini wasilazimike kufata matakwa yao bali watafute njia yao na muelekeo wao.
Pia Rais Samia ametaka viongozi hao kutolazimisha watu, wasiwe na udikteta bali washirikishe watu, wasiagize watu wakafanye vitu bali wawe na mbinu shirikishi. Amesema wakiwa na udikteta safari yao itakuwa fupi na wahakikishe nafasi walinayo wanayo kwa muda mrefu sio mfupi kwani kuna wakati watakuwa wanajaribiwa.
Kongamano la wanawake viongozi vijana Afrika
Zanzibar
03/12/2022