Rais Samia arejea kutoka Dubai na makubaliano 36 yaliyobeba trilioni 17.1 zenye ajira 204,575

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Na Bwanku M Bwanku

Leo Jumanne kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan kule Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Jana Jumatatu Februari 28, 2022 alirejea nchini kutoka kwenye ziara hiyo ambayo pamoja na mambo mengine alishiriki matukio mawili makubwa ya Kimataifa akianza kwa kuwa Mgeni rasmi na kuhutubia kwenye Siku Maalum ya Tanzania kwenye maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji Dubai Siku ya Februari 26 pamoja na Kuhutubia kwenye Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji Februari 27.

Kwenye ziara hiyo ya Falme za Kiarabu, tayali Rais Samia amerejea nchini akiwa na makubaliano takribani 36 ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali za maendeleo kati ya Tanzania na Falme hizo yenye thamani ya Trilioni 17.1 itakayotoa jumla ya ajira 204,575 kwa Vijana na Watanzania wote. Pata NAKALA sasa ya Gazeti letu uone namna siku 3 za ziara ya Rais Samia Dubai inavyokwenda kubadirisha Uchumi na maendeleo ya Taifa hili.

Bwanku M Bwanku

IMG-20220301-WA0005.jpg

ikulu_mawasiliano~p~CahXzzwthVm~1.jpg

IMG-20220228-WA0019.jpg
 
Hongera kwa makubaliano. Tunaomba tija katika utekelezaji wa makubaliano hayo hili changamoto zilizokusudiwa ziondoshwe.
 
Ndio nyimbo zao hawa wakienda nje wakirudi hapa ni yale yale tu
 
Na Bwanku M Bwanku

Leo Jumanne kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan kule Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Jana Jumatatu Februari 28, 2022 alirejea nchini kutoka kwenye ziara hiyo ambayo pamoja na mambo mengine alishiriki matukio mawili makubwa ya Kimataifa akianza kwa kuwa Mgeni rasmi na kuhutubia kwenye Siku Maalum ya Tanzania kwenye maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji Dubai Siku ya Februari 26 pamoja na Kuhutubia kwenye Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji Februari 27.

Kwenye ziara hiyo ya Falme za Kiarabu, tayali Rais Samia amerejea nchini akiwa na makubaliano takribani 36 ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali za maendeleo kati ya Tanzania na Falme hizo yenye thamani ya Trilioni 17.1 itakayotoa jumla ya ajira 204,575 kwa Vijana na Watanzania wote. Pata NAKALA sasa ya Gazeti letu uone namna siku 3 za ziara ya Rais Samia Dubai inavyokwenda kubadirisha Uchumi na maendeleo ya Taifa hili.

Bwanku M Bwanku

View attachment 2135151
View attachment 2135152
View attachment 2135153
Empty promises,mikataba mingi imefikiwa lakini ajira bado tatizo
 
Ama kweli baniani mbaya kiatu chake dawa!!!!! Waarabu hawa hawa ambao wadanganyika wanaoitwa masultani na adui wa muungano. waarabu wanaoshutumiwa kuwa wanaotaka kurudisha ufalme zanzibar ndio hao hao ambao leo serikali ya tanzania imefikiana makubaliano ya ushirikiano katika nyanja 36?
 
Sio rahisi namna hiyo huyu Mama naona mtazamo wake wa kuifungua nchi bado haupo sahihi nimekuwa nikisubiri nione namna gani anazifungua fursa za vijana wanaopigika mtaani waliosoma na wasiosoma kwa kweli sioni jipya zaidi ya uongo uongo.

Kila siku anasaini mikataba ya makubaliano lakini ukiitazama haifungui fursa yoyote kwa raia wa kawaida zaidi ya mabepari, labda aseme anaifungua nchi kwa mabepari.

"Nimeenda safari nimepata vijihela kidogo nimewaletea wanangu"....pure nonsense wote tunajua haiitaji kupanda ndege ili upewe mkopo au ruzuku iliyo kwenye makubaliano.
 
Huu utapeli naufananisha na ule utapeli wa Obama eti kuja na wafanyabishara 700.
 
Ama kweli baniani mbaya kiatu chake dawa!!!!! Waarabu hawa hawa ambao wadanganyika wanaoitwa masultani na adui wa muungano. waarabu wanaoshutumiwa kuwa wanaotaka kurudisha ufalme zanzibar ndio hao hao ambao leo serikali ya tanzania imefikiana makubaliano ya ushirikiano katika nyanja 36?
Inategemea na lugha inayotumiwa mkutanoni.
 
Back
Top Bottom