Chee4
Member
- May 17, 2021
- 35
- 125
Kwa kuzingatia uongozi wa sheria Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu amefikia muafaka na mfanyabiashara Harbinder Seth kupitia Sheria ya Pre- Bagain na kumuwezesha Sethi kuachiwa huru na Mahakama.
Akiwa Mahakamani akionekana mtu mwenye furaha baada ya kuafikiana makubaliano na DPP Mwakitalu tena kwa muda fupi, Mfanyabiashara Habinder Sethi alieleza Mahakama kuwa ameridhia kwa moyo wake wote kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 26, ambapo kwa hatua za awali ametoa shilingi Milioni 200.
Baadhi ya wananchi wamempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kumteua DPP Mwakitalu ambaye tangu ateuliwe May 13, 2021 moja ya majukumu ambayo ameyafanya na yamegusa hisia za watu wengi ni kuwaachia Masheikh wa uamsho.
Hakika kwa namna ambavyo (DPP) Sylvester Mwakitalu anavyotekelza majukumu yake kwa weledi, ni ishara ya kwamba jicho la Mhe. Rais Samia Suluhu halikukosea kumuamini mbobezi huyu wa sharia.