Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum kutoka kwa CAG inayohusu matumizi ya fedha zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia Januari hadi Machi 2021. Ripoti imebaini uwepo kwa miradi ambayo haikupangwa na hivyo kufanya malipo nje ya bajeti.