Rais Samia apokea ripoti ya CAG, deni bado ni himilivu. Mafao yazidi mapato ya mifuko ya hifadhi

Unataka ajikaguwe Wakati Toka ameanza Kutumia Ndege za Atcl Hajalipa Chochote
.
Anajifanya anaumwa Mgongo mbona Wakati Akiwa Makamu Alikuwa anatumia Gari Kwenda Sehemu Zote.
Anaumwa aisee kiti chake chenyewe cha kukalia lazima wamuwekee kagodoro fulani.....
 
Inawezekana hata hilo deni ni kiini macho,huenda deni la taifa kwa sasa ni T 100,watueleze tu ukweli!
 
Tilion 7 zimetumika kufanyanyia kitu gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pesa hii imetumika kwenye Ujenzi wa madarasa,ukamilishaji wa miradi,ajira mpya,upandishaji madaraja watumishi wa umma,ulipaji madeni kwenye mifuko ya jamii,Ujenzi wa miundombinu ya maji nk.nimekaa ajirani 7 years bila kupanda daraja la mshahara,mama kaingia ndani ya three months nikapanda.

Itoshe tu kusema kwamba mama anaupiga mwingi!!
 
Kuwa nami, CAG anasoma mambo muhimu kwenye ripoti yake ambayo anaiwasilisha kwa Rais Samia. Inaanza kwa hali isiyo njema kwa vyama vya siasa.

Endelea...

=========

View attachment 2169838

CAG: Upande wa vyama vya siasa, ADC hati mbaya, Chauma hati mbaya, TLP hati mbaya, UMD hati mbaya, CUF hati yenye shaka, UDP hati yenye shaka, SAU hati yenye shaka, Demokrasia makini hati yenye shaka, AFP tulishindwa kutoa maoni.

=> Nilitathmini utekelezaji wa mapendekezo wa miaka iliyopita, kati ya mapendekezo 31,311 ya miaka iliyopita, mapendekezo 9,975 sawa na asilimia 32 yametekelezwa kikamilifu. Mapendekezo 10,431 sawa na asilimia 33 utekelezaji wake unaendelea, mapendekezo 6284 sawa na asilimia 20 hayajaanzwa kutekelezwa, mependekezo 2890 sawa na asilimia 9 yamerudiwa na mapendekezo 1731 sawa na asilimia 6yamepitwa na wakati.

MAMBO YA MSISITIZO

MWENENDO WA DENI LA SERIKALI

CAG: Kufikia June 30, 2021 deni la Serikali lilikuwa ni trilioni 64.52 ikilinganishwa na trilioni 56.76 mwaka uliopita hivyo kuna ongezeka la shilingi trilioni 7.76 sawa na asilimia 13.7

=> Hata hivyo, kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la taifa kinaonyesha deni hili bado ni himilivu.

MIRADI YA VIWANJA VYA NDEGE
CAG: Kuanzia mwaka 206/17 hadi 2020/21 Serikali ilitumia jumla ya trilioni 1.02 kujenga na kuboresha viwanja vya ndege 12 hapa nchini.

Ukaguzi wangu ulibaini
=> Kuna uingiliano wa mamlaka na majukumu ya uendelezaji wa viwanja vya ndege baina ya TAA na TANROADS unaosababisha mapungufu katika uwajibikaji na utekelezaji wa bajeti za miradi hiyo.

=> Kuna ongezeko la gharama ya Tshs bilioni 22.35 kutokana na kutolipa fidia kaya 1,125 katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere kwa zaidi ya miaka 25, kuna watu pale wanatakiwa kulipwa fidia lakini hawajalipwa kutokana na taratibu kutokamilika.

=>Tathmini inaonesha deni linaongezeka ktoka bilioni 7 hadi bilioni 29.

=> Kuna kuchelewa kwa malipo ya wakandarasi kulikosababisha riba ya Tshs bilioni 14.14 ambapo bilioni 11.39 ni za kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere na bilioni 2.75 ni kiwanja cha ndege cha Mwanza.

View attachment 2169837

MWENENDO WA MABENKI YA SERIKALI

CAG:
Kiwango cha mikopo chechefu kwa TIB kiliongezeka kutoka asilimia 41.5 mwaka 2019 hadi aslimia 51.5 mwaka 2020 kinyume na lengo la benki kuu ambayo ni asilimia 5 pekee.

=>TIB imeshindwa kulia madeni yake ya kodi ya shilingi bilioni 28.4 kwa miaka minne mfululizo kuanzia 2017

MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

=> Mifuko ya hifadhi ya jamii ina changamoto mbalimbali, nizitaje chache.

=> Kwa miaka mitatu mfululizo, mafao ya pensheni ya mfuko wa hifadhi ya jamii wa sekta ya umma yalizidi mapato yatokanayo na michango kwa mwaka husika.

=> Kwa mwaka 2020/21 mafao yalizidi kwa bilioni 767, 2019/20 yalizidi kwa bilioni 232 na mwaka 2018/2019 yalizidi kwa bilioni 307.

=> Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii wa sekta binafsi ulitoa mikopo ya trilioni 1.17 kwa taasisi kumi za Serikali ambayo haijalipwa tangu mwaka 2007.

=> Hadi kufikia June 2021, mfuko wa hifadhi ya jamii sekta ya umma ulikuwa na madeni ya bilioni 323.98 kutoka kwa taasisi za Serikali na taasisi zingine.

MWENENDO WA MASHIRIKA YA UMMA

=>Mashirika ya umma 38 hayakuwa na bodi ya wakurugenzi, kati yake mashirika 26 yalifanya kazi bila bodi kwa zaidi ya miaka 12.

MIRADI YA KIMKAKATI

=> Kuchelewa kwa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kwa asilimia 46.45. Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2021 mradi ulipangwa kukamilika kwa asilimia 94.47, hata hivyo nilibaini mradi ulikamilika kwa asilimia 48.02 ukiwa umechelewa kwa asimilia 46.45.

=> Ucheleweshaji umesababishwa na kuchelewa kuwasilishwa kwa usanifu wa mwisho wa mradi, janga la mafuriko kwenye mto Rufiji pamoja na janga la Uviko.

=> Kukatika katika kwa umeme kwenye eneo la mradi kunasababisha kuongezeka kwa gharama na muda wa kukamilisha mradi.
Ripoti ya kirafiki kabisa hii!

Ngoja tujipigie kwa urefu wetu wa kamba!!
 
Report imesema hilo, isome vizuri kama ilivyoletwa hapo juu, na namba zimewekwa kuhusu hilo.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
@FaizaFoxy napendaga sana hiyo sentensi yako kuhusu shule. Wabongo wavivu sana kusoma vitu in details
 
Serikali haikusanyi Kodi kwa matajiri kwaiyo tegemeo lake ni kukopa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ndio sababu kuu ya nchi kuyumba na uchumi kuteteleka na kuishia kukopa ili kufanya mambo ambayo tungeweza kuyafanya kwa pesa zetu za ndani, lakini kwasasa matajiri hawaguswi na wanaendelea kuwanyonya watanzania masikini wasio na kitu hii nchi hii, lakini ata the end wote tutakufa tu hakuna namna.😂😂😂
 
Ikifika 2024 utasikia kuwa Bwawa litakamilika 2026.Taifa linaongozwa na vibaka🚶🚶🚶
AAXv4U.jpeg
 
Mkuu pesa hii imetumika kwenye Ujenzi wa madarasa,ukamilishaji wa miradi,ajira mpya,upandishaji madaraja watumishi wa umma,ulipaji madeni kwenye mifuko ya jamii,Ujenzi wa miundombinu ya maji nk.nimekaa ajirani 7 years bila kupanda daraja la mshahara,mama kaingia ndani ya three months nikapanda.

Itoshe tu kusema kwamba mama anaupiga mwingi!!
Chawa kama chawa kwenye ubora wenu😂😂😂
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu amemtaka Waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa kuwafukiza Kazi watendaji na watumishi watakaobainika kuiba pesa za umma.

Rais alikuwa akizungumza Kuhusu mishahara hewa na watumishi hewa.

Kazi iendelee 👇

Screenshot_20220330-205613.png


Screenshot_20220330-205349.png
 
Unateua/kuajili watu kwa vimemo, kada, fadhira, nyumba ndogo, nk. hao utaweza kuwafukuza kweli??!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom